Bei za vifurushi kupanda huku waziri mwenye dhamana akikenua meno kwa furaha ni matusi mazito kwa waTanzania

Bei za vifurushi kupanda huku waziri mwenye dhamana akikenua meno kwa furaha ni matusi mazito kwa waTanzania

Mkuu tusiongee mengi.
Sababu ulizoongea ndiyo zilitosha kuchafukwa pasikalike, sababu nchi hii si koloni ama watemi ambao viongozi wanapatikana kwa kurithi, ni ya kidemokrasia.

Serikali kama inaongoza hovyo kwa kukiuka ilani zake na katiba, hata kama ilichaguliwa kihalali, iondolewe tu, haina manufaa kwa watu.

Ukimya wa viongozi(Ccm na upinzani) tayari mie nimewaweka fungu moja.

Hata wewe unayewavumilia ipo siku utawachoka tu, labda wabadilike pakubwa na wajitambue na watambue tunachokitaka wananchi!

Embu kaa utulie uwapime bila mahaba kuanzia ccm na viongozi wa upinzani, kuna yeyote anayekemea uozo tunaofanyiwa raia kwa sasa?

Utetezi kwa viongozi wa upinzani kupigwa tanchi hauna uzito kwa sababu si mikutano pekee ama uwakilishi Bungeni tu, kuna njia nyingi za kuzungumza na umma na kiongozi akaeleweka anakusudia nini na raia tukamsapoti, hasa kwa dunia hii ya kidigital.
Nimekuelewa mkuu
 
Huyo Waziri ni mnafki sana Jiwe alimshtukia akamtosa sijui Sa100 ametokana naye wapi!
Watz smart wapo kibao kumsadia Mama namshangaa anambeba huyu mwenye akili ya kawaida tuu!.
Hewa ingine ni Jenistaa Mhaagama eti naye waziri!.
 
Ananunua mwenyewe kwa fedha anazopewa na Serikali.
Labda tuseme hivyo jinsi allowance za mawasiliano zinavyotumika, kuweza kununua wenyewe ama kughairi na fedha hizo kuzifanyia matumizi mengine.

Maana yake ni kwamba, allowance hizo huingiziwa moja kwa moja kwenye account za mishahara yao, sasa hapo atasema kanunua kifurushi cha bando kwa hela yake?
Hela yake kwa sababu imepitia kwenye account yake siyo?
Aache kudanganya watu na kuona ni wajinga.
 
Huyo Waziri ni mnafki sana Jiwe alimshtukia akamtosa sijui Sa100 ametokana naye wapi!
Watz smart wapo kibao kumsadia Mama namshangaa anambeba huyu mwenye akili ya kawaida tuu!.
Hewa ingine ni Jenistaa Mhaagama eti naye waziri!.
Na alionyesha nia yake ovu kwa nchi pale alipopigia debe mradi wa bwawa la kufua umeme Rufiji usitishwe ati kupisha uchunguzi wa mazingira

 
Ujue mkuu hili tatizo nimegundua ni la kijamii.

Namaanisha waTz wote kwa ujumla wetu tunakubaliana na kuridhika na huu upumbafu, vjnginevyo isingewezekana.

"The late" hao aliwafukuza kama mbwa kwa kuona mapungufu yao kuwa hawafai hata kwa kulumangila, lakini twashangaa Serikali hiyo hiyo kulamba matapishi yake kwa kasi ya upepo baada ya mwamba kudanja, ni nini kilikuwepo mbele ya pazia!

Hapa nadhani wa kulaumiwa si Nape peke yake, ni cyndcate nzima ya Serikali iliyopo madarakani.

Angalia mgao wa umeme na maji unavyotukaanga!

Bidhaa madukani kupanda kila siku bila ya tamko la Waziri husika ama Rais kukemea!

Maana yake ni kwamba haya yote yanayofanyika sasa hivi kudhalilisha watu kwa kupandisha bei za bidhaa za vitu na mgao wa maji na umeme ni baraka za Serikali iliyopo madarakani.

Kwa yanayoendelea nchini ilitosha kwa waTz kwa ujumla wetu kusema "hapana" kwa serikali iliyopo madarakani, "hapana" kwa Chama tawala na "hapana" kwa vyama vya upinzani, maana navyo kama sauti yetu vimelambishwa asali na kunyamazishwa, sasa ni vya nini na vina msaada gani kwetu?

Navyodhani, tuendelee kukandamizwa sana zaidi ya hapa ili uovu zaidi uliojificha katika nafsi za viongozi hawa mumiani uudhi zaidi na kukera mioyo ya wajinga wenye mahaba niue kwa serikali iliyopo madarakani ili mwisho wa siku wajitambue tuweze kuongea lugha moja na kauli moja kudadadeki.
Tutamkumbuka sana mwamba kiukweli.

Yule mzee kweli alikuwa anawapigania watz
 
Airtel wamepunguza tena bundle la internet la 2000 toka Mb 985 hadi Mb 970, shit!
 
Nyie watanzania ni mambumbumbu sana hivi mnajua bundles ni ofa,wao wanatakiwa wakuuzie we we vocha tu uweke utumie kama mwanzo mitandao ilivyoanza, sasa unajua maana ya ofa, ofa kupata au kunyimwa huna uhalali wa kudai.
 
Nyie watanzania ni mambumbumbu sana hivi mnajua bundles ni ofa,wao wanatakiwa wakuuzie we we vocha tu uweke utumie kama mwanzo mitandao ilivyoanza, sasa unajua maana ya ofa, ofa kupata au kunyimwa huna uhalali wa kudai.
Offer au isiwe offer, ni kwamba unalipa pesa na unapata huduma, gharama ya huduma imepanda.., na inapandishwa kila siku wakati bei ya mafuta imeshuka, na wanapandisha kwa kuambizana kitendo ambacho ni kinyume na kanuni za FCC
 
Back
Top Bottom