Bei za vitu kushuka Kenya, sisi tunakwama wapi?

Naomba nikuulize swali moja tu, huiamini nguvu ya umma kwenye kuleta mabadiliko?
Kwanza jifundisheni kusoma hoja, na kutotoka nje ya hoja, mleta mada ameleta hoja kwamba Kenya wapo vizuri wameshusha bei ya Unga akilinganisha na Tanzania, ila ukiangalia kwa jicho la upana zaidi kenya vitu ni Ghali kuliko kwetu na hata hio bei wanayoitaka ni sawa na kwetu ama ni ghali bado ukilinganisha na kwetu.

Nguvu ya uma inaweza leta mabadiliko, kujibu swali lako
Unaweza pia kunionesha uhusiano uliopo, kati ya kuwa na pesa ya kulipa mishahara na serikali kupunguza bei ya vyakula?
Ufahamu kwanza huu mfumuko ni External factors kupanda kwa bei ya Mafuta na sababu nyengine zifananiazo

1. Serikali ilitoa ruzuku, hii ruzuku ilitoka kwenye mapato ya ndani, walikuwa na uwezo wa kutoa ruzuku zaidi hata 500 kwa kila lita ila kutokana na umasikini wa Nchi yetu na sisi pia tusingeweza kulipa Mishahara.

2. Unapolipa mishahara pia unapunguza Ukali wa maisha, vaa viatu vya Mkenya hajalipwa mshahara na vitu vimepanda bei.
 
Wewe umeleta hoja simamia kwenye Hoja yako, unapoleta msururu wa hoja nyengine unakuwa hater kama hater wengine tu.

Na heading ya Uzi wako unasema vitu kushuka Kenya sisi tunakwama wapi?

Jibu na mimi nakupa Kwetu vitu ni bei rahisi kuliko Kenya.

Karibu tuendeleze mada
 
Mambo ya kitaalamu hayaitaji msuli, umma usiotumia akili, unaweza kutumiwa na wanasiasa for their own political mileage or gain
Unatumiwa vipi na wanasiasa kwenye jambo ulilo na manufaa nalo?

Bei ya vyakula ikishuka baada ya maandamano huko ni kutumiwa na wanasiasa?
 
- Licha ya maneno mengi kujaribu kuzunguka mbuyu, hatimaye mwishoni kabisa umeamini nguvu ya umma inaweza kuleta mabadiliko, kwa jibu lako hilo, vingine vyote ulivyoandika nadiriki kusema havina maana.

- Hoja yako ya pili ni usanii mtupu, simply umejitengenezea mada yako, ukaiacha ya mleta mada, hapa mada inazungumzia vitu kushuka, wewe unatupeleka kwenye kupanda licha ya wao kukosa mshahara, unajiona uko sawa kweli?

Ruto anasema, licha ya wao kukosa mishahara, bei ya unga itashuka kuanzia next week, wacha kujitungia maneno yako.
 
Unatumiwa vipi na wanasiasa kwenye jambo ulilo na manufaa nalo?

Bei ya vyakula ikishuka baada ya maandamano huko ni kutumiwa na wanasiasa?
Je unazijua sababu za kupanda kwa bei za bidhaa, kama unazijua, unadhani maandamano yanaweza ku-influence changes?

Of cause, nobody underestimate the power/strength of fools in large numbers. Ila ukweli utabakia pale pale
 
Licha ya maneno mengi kujaribu kuzunguka mbuyu, hatimaye mwishoni kabisa umeamini nguvu ya umma inaweza kuleta mabadiliko, kwa jibu lako hilo, vingine vyote ulivyoandika nadiriki kusema havina maana.

Pointi yako ya pili ni sawa na umejitengenezea mada yako,
Yani uniulize swali nikujibu useme nimetengeneza mada yangu?
ukaiacha ya mleta mada, hapa mada inazungumzia vitu kushuka, wewe unatupeleka kwenye kupanda licha ya wao kukosa mshahara, unajiona uko sawa kweli?
Mada inazungumzia kitu sio vitu, kitu chenyewe unga, na amesema kinashuka hadi 2000, sisi Tanzania ukiwa na 2000 hupati unga?

Logic aliojibiwa hapa ni kwamba Kenya vitu Ghali kupita maelezo even wakipunguza still ni more expensive kuliko Tanzania. We are in much better position than them.
 
Ruto anazungumzia bei ya unga kushuka kuanzia next week, hapo kuna vitu vingapi?
 
Hivi bei za bidhaa zinawekwa na nguvu ya soko (market forces) au matamko ya kisiasa?
Awali Serikali chini ya Uhuru, iliweka RUZUKU ktk bidhaa na vyakula kupunguza inflation,

Serikali ya Luto iliondoa RUZUKU na kuongeza Kodi Ili kupata pesa ya kulipa mikopo na riba. Jambo Hilo lilisababisha Bei kupanda.

Kama wameamua kurudisha RUZUKU,tafsiri ni kuwa wataenda kukopa.
 
Kimoja unga.
Sasa zile kelele zako zilikuwa za nini!

Muhimu umeshakiri nguvu ya umma inaweza kuleta mabadiliko, na mabadiliko hayo ndio yamesababisha bei ya unga kushuka kuanzia next week, basi tufunge mjadala wetu, mambo mengine mengi unayoandika hayana maana.
 
Any intervention by government inakua short term and not sustainable, mwisho wa siku soko litaamua
 
Hakuna kitu ulichoandika, a misplaced and short sighted opinion
 
Any intervention by government inakua short term and not sustainable, mwisho wa siku soko litaamua
Pamoja na market forces, kuongeza Kodi kwenye domestic products ndilo tatizo kuu la inflation.

So maandamano yamesaidia kuizibua Serikali masikio.
 
Pamoja na market forces, kuongeza Kodi kwenye domestic products ndilo tatizo kuu la inflation.

So maandamano yamesaidia kuizibua Serikali masikio.
Sawa, lakini Ruto amezirithi hizo kodi
 
Mbona hujatuonyesha mchanganuo wa bei zilivyoshuka badala yake unaongea ujinga ujinga tuu.

Tanzania Huwa haiigi upuuzi, uzalishaji na soko ndio vitaamua bei.
Wakati wa uchaguzi kilo ya UNGA ilifika 230kshs sawa na 3910tshs,. Now wanaonunua Kwa 180kshs sawa na 3060tshs.

So wanataka ishuke Hadi 2000tshs sawa na 117 kshs.

Naamini lazimà wakakope Ili kulipa bills na kufidia RUZUKU hiyo.
 
Sawa, lakini Ruto amezirithi hizo kodi
Serikali ya uhuru iliweka RUZUKU na Bado walinunua kshs 230 sawa na 3910, RUZUKU ilikuwepo bt UFISADI haukusaidia reduction in prices,

Tolu alipoingia, kafuta RUZUKU na kuongeza Kodi kwenye domestic goods na bado Bei ilishuka Hadi 180 kshs sawa na 3060ya TANZANIA.

So Kuna jitihada kubwa anafanya. Pia naamini maandamano ni njia nzuri ya kuwakosesha USINGIZI.

IKULU ni ofisi kuu, ni Mahali pa KAZI Si Mahali pa kusinzia.

Tunalo la kujifunza ktk Hilo.
 
Wanabomoa uchumi wao wenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…