Bei za vitu kushuka Kenya, sisi tunakwama wapi?


Kuna jingine liko hapa lakini nalo ni jizi tu kama yale stupid ya dege:

 
Ila mwenye hoja maana mtanzania wewe ukiwa hapo Nanjilinji na bado hujishangai.

"Maana kamili ya kuwa mtanzania ni mjuaji mno!"

Kama wewe kwenye mada, wazi wazi mliangaziwa.
nanjilinji ndiyo nini
 
Walaji hatuko tayari kuchukua hatua, kwa hiyo tuendelee kuumia wenyewe

Wa kwanza kwenye kuona kuwa wananchi wanachukua hatua ni Raila.

Kama sivyo mbona tangu aseme maandamano yanasimama hakuna mkenya aliyemwagika barabarani tena?

Viongozi wetu wa maandamano wako wapi?
 

Raila Kenya kama yeye hana njaa ila kawahamasisha watu vilivyo na akatokea nao pamoja na wenziwe kuandamana.

Raila katokea kutangaza maandamano yanasimama na yakasimama kweli.

"Mbona hakuna mkenya hata mmoja anaandamana tena bila Raila kuridhia, kama kumbe watu hao wako kwenye maandamano kila mmojw kivyake vyake?"

Watu hawa wamehamasishwa vilivyo na wako organized. Hizo ni kazi za viongozi Sasa za viongozi wa vyama vyenye kupigania haki. Viongozi wakishindwa kuzifanya kazi zao hizo zikiwamo kama ndivyo tunavyotaka, watupishe au tuwafurushe madarakani tuweke wengine wenye nia na uwezo huo.

Uongozi si fursa. Uongozi ni wajibu.

Tukubaliane unaingia madarakani kutuhamasisha na kutuongoza kudai haki zetu. Huwezi hayo kaa pembeni. Tatizo liko wapi? Wenye uwezo huo mbona wapo wengi wa kumwaga?

Tuacheni utamaduni huu kuangaliana usoni. Hautusaidii na hautatuvusha. Ukombozi wa nchi hii ni muhimu zaidi kuliko mtu yeyote.

Huu ndiyo ulio ukweli mchungu.

Cc: Zawadini
 
Huyo wala hajielewi, wala haelewi kinachoendelea Kenya zaidi ya kuokoteza story tu

Mwenye kujielewa utakuwa wewe ndugu almaarufu kijana wa hovyo?

"Maana kamili ya kuwa mtanzania ni mjuaji mno!"

Kauli hiyo Iliyopo kwenye mada ndiyo hii sasa.

"Vijana wa hovyo hawana mchango wowote kwenye taifa hili." -- alisikika bwana yule.

Bure kabisa.
 
Naamini huo ujasiri hawajafundishwa na Raila, uko ndani ya nafsi zao.
Hata humu JF watu wengi sana hunasa kwenye mitego kama ya kina johnthebaptist ambao hueneza Propaganda kwamba wenye jukumu la kuwafanya watanzania kuandamana ni CHADEMA. Kwa ivo likitokea jambo watu hudhani wanaotakiwa kuandamana ni CHADEMA ama CHADEMA ndiyo wanaotakiwa kuhamasisha maandamano.

Mtu kaajiriwa na kwa miaka mitano hajapandishwa daraja au mshahara, anataka nani aandamane kwa niaba yake? Magari ya Umma yanabwagwa mitaani kama takataka na mwisho wa siku wakubwa wanauziana, watanzania wanataka nani aandamane?

Ripoti za CAG kila mwaka zinaonesha ni kwa kiasi gani ndani ya serikali kuna wizi na ubadhirifu uliotukuka, wabongo wanasubiri viongozi wa upinzani ndiyo waandamane!! Hoja yako hapa si kwamba hakuna viongozi wa kuhamasisha maandamano bali watanzania wenyewe ndiyo WAOGA!!
 

Usiniwekee maneno mdomoni mjomba. Hivyo jifunze kwanza kusoma mada kabla ya kuchangia.

Kwa msingi huu ulichoandika hakihusiani na mada, uko nje ya mada na hivyo huu wako utatusaidia, tuuite je.

Mada ni kuwa serikali ya Kenya imelazimishwa kushusha na waandamanaji.

Ulinganifu na sisi ni kuwa vipi wenzetu wanafanikiwa lakini siyo sisi.

Jitathimini kama umejikita kwenye mada hiyo. Kama sivyo itapendeza ukijitendea haki mwenyewe kutupa mrejesho kuwa hukuelewa.
 

Hauko sahihi ndugu.

Maandamano yanataka hamasa na organization ya kutosha. Ni jukumu la watu kufanikisha hayo. Hayawezi kuja kama mvua.

Ulichoandika ni visingizio vya kawaida vya viongozi dhaifu wenye kuvitumia vyama zaidi kama fursa za kimapato yao binafsi. Zingatia viongozi hawa wanalipwa.

Kenya bila Raila, hakuna hamasa wala maandamano tunayoyaona sasa.

Raila kaitisha maandamano yakawepo. Alipoitisha kusitishwa yakasimama. Kenya hawajaandamana Kwa sababu tu ya sababu zilizotolewa.

Kama maandamano yalikuwa ni kwa sababu zilizotolewa tu, mbona hayakuanza bila Raila au bila kuyaitisha au hayakuendelea bila yeye baada ya yeye kuyasitisha?

La msingi tufahamu Kenya wamehamasishwa na wako organized vilivyo. Hiyo haikutokea kwao kama ajali na haitatokea kwetu kama ajali.

Hayupo anayemlenga chadema, viko vyama vingi ikiwamo wao. Aliyeshindwa kuwa organize na kuwahasisha watu hata akathubutu kutamka kukosa uungwaji mkono angali vipi ofisini leo?

Kwa nini utaratibu wa kupata viongozi kwenye vyama hivi across the board usiwe huru, haki na kidemokrasia kupitia primaries za wazi kama ilivyo kwake beberu? Watu wakagombea Kwa kuzingatia agenda na malengo yetu ya ukombozi na wakapimwa kwa outputs zao?

Watu wenye uwezo wa kuendesha kwa ufanisi kwenye malengo yetu wapo wengi.

Kwanini tusiwape nafasi hizo walio tayari tuone matokeo?

Zingatia Liz Truss alikaa ofisini Kwa siku 45 Kwa kutokukidhi matarajio.

Tupateje viongozi wasiofika vigezo vyetu Kwa utaratibu huu.

Ya nini kuliita koleo kuwa ni kijiko kikubwa?

Mawazo kama yenu mkuu yanaturudisha nyuma sana.

Cc: Zawadini
 
Kwaiyo we unataka tufanye nini Tuandamane aza wewe kwanza na baba ako kisha wengine tutafuata
 
brazaj mfano wako wa maandamano ya Kenya kumhushisha Laila unakosea sana. Ukijikumbusha vita ya Mau Mau utaona kwamba wala si suala la Laila Wakenya kuwa vile.

Lakini pia unajua ushawishi wa Laila Nairobi unatokana na nini. Tafuta kwa karibu habari za Kibera ujielimishe. Mbona siyo Kenya Nzima walioandamana??

Maandamano huratibiwa kwa watu waliotayari kuandamana ila huwezi kuratibu maandamano kwa watu wasio tayari kuandamana. Watanzania ni waoga wa kuandama dhidi ya serikali. Kenya hata bila ya Raila wataandamana tu maslahi yao yanapotishiwa!!
 
Kwaiyo we unataka tufanye nini Tuandamane aza wewe kwanza na baba ako kisha wengine tutafuata
Eti brazaj ndiyo anataka watu kama nyie mratibiwe kuandamana. Muelezee aelewe kwamba nyinyi watanzania si watu wa kupenda maandamano dhidi ya serikali hata kama hiyo serikali iwatendee jambo gani baya.
 
Halafu brazaj huo mfano wako wa LIz Truss unaourudiarudia unamaanisha nini? Yeye alitoka kwa kuwa ilionekana ndani ya chama chake watu hawamuungi mkono kwa mambo yake ya kibajeti. Unataka kusema hapa CCM wambane Majaaliwa ama Samia hadi wajiuzulu!!??
 
Halafu brazaj huo mfano wako wa LIz Truss unaourudiarudia unamaanisha nini? Yeye alitoka kwa kuwa ilionekana ndani ya chama chake watu hawamuungi mkono kwa mambo yake ya kibajeti. Unataka kusema hapa CCM wambane Majaaliwa ama Samia hadi wajiuzulu!!??

Kwa sababu unaamini kuwa umejibu hoja zangu ungesubiri tujadili kwenye mada moja badala ya hii ya kuruka ruka hapa na pale.

Zingatia pia kuwa tunaandika huku tukichapa kazi. Hivyo majibu yanaweza kuwa kuna ka kuchelewa kidogo, ila yote yatajibiwa.

Upotoshaji si afya, nao ni relative. Unaweza kuufanya kwa kujua au bila kujua.
 
Wala sioni kama ni suala la kuoneana aibu au vinginevyo, kwangu naona tatizo lipo kwetu na ndio maana wengine husema wacha kina Mbowe walambe asali, wameshahangaikia sana watu wasiojitambua badala yake hakuna walichoambulia zaidi ya kufungwa jela wao binafsi.

Kama watanzania tungekuwa tunajitambua, yule Mbowe asingefungwa jela miezi sita, lakini kwa wakenya hali ni tofauti, wakijaribu kumkamata Raila, wakenya wataingia barabarani naturally, ndio maana nakwambia wakenya movement zao zinaanzia inside, wala sio lazima awepo kiongozi wa kuwaamsha.
 
Eti brazaj ndiyo anataka watu kama nyie mratibiwe kuandamana. Muelezee aelewe kwamba nyinyi watanzania si watu wa kupenda maandamano dhidi ya serikali hata kama hiyo serikali iwatendee jambo gani baya.

Nimeamua kuanza na hizi zako nyepesi nyepesi ambazo nashangaa kuwa zote zimejibiwa kwenye mada lakini bado umezileta hapa.

Imo kwenye mada:

"Inafahamika kuwa hata huko walamba asali, wahuni na hata vijana wa hovyo wapo. Kwamba yaliyoko kwetu na kwao yapo. Hata hivyo ujasiri wa viongozi wao wenye misimamo isiyotetereka ni jambo la kupigiwa mfano sana."

Nani anamhutaji huyo Shazili mnali ambaye ni mmoja katika makundi matatu hayo kuandamana achilia mbali kumratibu Kwa lolote.

Tafadhali tujikite kwenye mada kwa majadiliano yenye tija kama unataka.

Hata haya ya kiratibiana sijui unayaokota wapi.

Nisiache kukwambia kwa mawazo mgando ya kutaka madaraka bila wajibu hatutakaa kutoboa.

Acheni kuwalaumu wadau, bila wenyewe kuwajibika.

Tatizo letu liko hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…