Raila Kenya kama yeye hana njaa ila kawahamasisha watu vilivyo na akatokea nao pamoja na wenziwe kuandamana.
Raila katokea kutangaza maandamano yanasimama na yakasimama kweli.
"Mbona hakuna mkenya hata mmoja anaandamana tena bila Raila kuridhia, kama kumbe watu hao wako kwenye maandamano kila mmojw kivyake vyake?"
Watu hawa wamehamasishwa vilivyo na wako organized. Hizo ni kazi za viongozi Sasa za viongozi wa vyama vyenye kupigania haki. Viongozi wakishindwa kuzifanya kazi zao hizo zikiwamo kama ndivyo tunavyotaka, watupishe au tuwafurushe madarakani tuweke wengine wenye nia na uwezo huo.
Uongozi si fursa. Uongozi ni wajibu.
Tukubaliane unaingia madarakani kutuhamasisha na kutuongoza kudai haki zetu. Huwezi hayo kaa pembeni. Tatizo liko wapi? Wenye uwezo huo mbona wapo wengi wa kumwaga?
Tuacheni utamaduni huu kuangaliana usoni. Hautusaidii na hautatuvusha. Ukombozi wa nchi hii ni muhimu zaidi kuliko mtu yeyote.
Huu ndiyo ulio ukweli mchungu.
Cc:
Zawadini