DELETED ACCOUNT
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 9,805
- 15,476
Wachezaji wanaojitambua wanastahili heshima ya kipekee.
Wachezaji wengi wa Tanzania hawafiki mbali maana hawajitambui. Wanalipwa mshahara, halafu wanageuka tena wanapokea hongo kukwamisha timu zinazowalipa mshahara. Wakifungwa hawajali, yaani kwao kucheza kwa bidii na maarifa siyo shida zao. Halafu ukute sasa wamezungukwa na viongozi ambao badala ya kuwasimamia wafanye vizuri ndiyo kwanza wanashirikiana nao kuhujumu.
Katika mechi ya Simba vs Yanga, kuna tukio ambalo shuti kali lilikuwa linaenda golini kwa Simba, beki Rushine De Reuck akajitoa mhanga kuupiga kichwa. Hiki kitu niliwahi kumuona Ibrahim Bacca akikifanya. Yale maumivu yakampeleka Rushine chini. Refa hakupuliza filimbi ili kumuangalia hali yake na hatari ikarudi golini kwa Simba.
Rushine alipoona hivyo, akalazimika kusimama kulinda lango huku akiendelea kuugulia. Ni nadra sana kukuta wachezaji wa Simba wanaojituma namna hii.
Huyu jamaa atafika wakati akishaona anajali peke yake na kila aliyemzunguka hajali, na yeye ataanza vituko.
Katika habari zingine, kuna mfanano wowote kati ya haya matukio mawili?