Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mchezaji wa zamani wa Simba SC, Israel Patrick Mwenda, amekamilisha uhamisho wake wa mkopo wa miezi sita kutoka Singida Big Stars kwenda Young Africans (Yanga).
Pia, Soma: Singida Black Stars yasema imemlipa Mwenda Tsh. 140m yamtaka aripoti mazoezini
Beki huyo anauwezo wa kucheza kama beki namba 2 na 3 amekuwa na msimu mfupi na Singida BS, sasa anajiunga na mabingwa mara 30 wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara katika hatua ya kuimarisha kikosi chao kuelekea michuano ya ndani na ya kimataifa.
Beki huyo anatarajiwa kuongeza ushindani kwa Kouassi Attohoula Yao ambaye ndio amekuwa chaguo la kwanza kwa beki wa kulia wa timu hiyo pamoja na Kibwana Shomari ambaye amekuwa akianzia benchi.
Huu ni usajili wa kwanza kwenye dirisha hili la usajili ambalo linatarajiwa kufunguliwa Desemba 15.