Beki wa zamani wa Simba SC, Israel Mwenda atua Yanga kwa Mkopo akitokea Singida Big Stars

Beki wa zamani wa Simba SC, Israel Mwenda atua Yanga kwa Mkopo akitokea Singida Big Stars

Mchezaji wa zamani wa Simba SC, Israel Patrick Mwenda, amekamilisha uhamisho wake wa mkopo wa miezi sita kutoka Singida Big Stars kwenda Young Africans (Yanga).
Pia, Soma: Singida Black Stars yasema imemlipa Mwenda Tsh. 140m yamtaka aripoti mazoezini

Beki huyo anauwezo wa kucheza kama beki namba 2 na 3 amekuwa na msimu mfupi na Singida BS, sasa anajiunga na mabingwa mara 30 wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara katika hatua ya kuimarisha kikosi chao kuelekea michuano ya ndani na ya kimataifa.
Beki huyo anatarajiwa kuongeza ushindani kwa Kouassi Attohoula Yao ambaye ndio amekuwa chaguo la kwanza kwa beki wa kulia wa timu hiyo pamoja na Kibwana Shomari ambaye amekuwa akianzia benchi.

Huu ni usajili wa kwanza kwenye dirisha hili la usajili ambalo linatarajiwa kufunguliwa Desemba 15.
Yanga hii haina tofauti na Harmonize mzee wa mipira iliyokufa, demu akishaburuzwa na wengine akiachwa yeye ndiyo anajiokotea tu.
 
Waende KMC kumchukua yule Lamso Angalau anaweza kum challenge Yao.
 
Sasa sii ndio unaenda kuchukua huyo wa first 11 mwanawane maana yule kazi ya kiume kweli kweli.
Si rahisi kama unavyodhani, haina afya kuwa na mabeki wawili wa upande mmoja wote wa kigeni, labda wamwache Yao Yao. Kwa maoni yangu kuna beki wa kulia pale KMC labda Yanga wangemsajili,yule ni mzuri kuliko Israh
 
Ndo kusema wameishiwa pesa za usajili!?.
Hapana, huyo Israh Yanga walimhitaji tangu akiwa Simba, kwenda SBS ilikuwa ni janja tu kama ya Ramadhani Wasso mwaka 2004 aliyewaaga Simba amepata timu Ubelgiji walipomruhusu akaibukia Jangwani.
 
Ukitoa Tanzania Kuna nchi nyingine wanayomjua ?
Hawa ni Wasouth Africa,hivi ndivyo wanavyomjua. CAF wenyewe katika events zao zote kubwa huwa wanampa mwaliko rasmi.
 

Attachments

  • Screenshot_20241211-150046.png
    Screenshot_20241211-150046.png
    765.9 KB · Views: 2
Si rahisi kama unavyodhani, haina afya kuwa na mabeki wawili wa upande mmoja wote wa kigeni, labda wamwache Yao Yao. Kwa maoni yangu kuna beki wa kulia pale KMC labda Yanga wangemsajili,yule ni mzuri kuliko Israh
Kwa hiyo kiugupi hawana hela ya kumnasua pale sbs
 
Kwa hiyo kiugupi hawana hela ya kumnasua pale sbs
Unaweza kuwa na hela lakini muuzaji akagoma kukuuzia, Ni kama Simba tu wanavyomhitaji Feitoto lakini Azam hawataki kumuuza.Swala la kuuza linategemea uamuzi wa muuzaji zaidi kuliko mnunuzi
 
Back
Top Bottom