Ben Saanane: Ninatishwa kuuawa kwa kuikosoa Serikali

Siku zote suluhu ya Mtu asiyejiamini ni kutopambana kwa hoja anataka kuutafuta uhai wa mpinzani wake. Long Live Ben. Mi nadhani ile sheria ya Makosa ya mtandao ioneshe mashiko yake hapa na so kwa wale wanaogusa maslahi ya watawala tu.
Ova!
Kwa kwl man hii ni hatari Sana naona sheria inageuka na kuwa panga likatalo sehem moja sio tena msumeno
 
Wanataka kumchafulia heshima mtani wetu Foreman...
 
Ben Sanane aboreshe mbinu za kujitangaza, hii style ya kujidaia anatafutwa ni ya zamani sana na ya kipuuzi.
 
duh, hizi kiki hizi! unajitumia SMS ili uje uandike makala zisomwe na watu wengi
 
Hitman afanyi kazi kibwege hivo yaani akupe taarifa wewe nani...halafu hakuna cha ajabu na ulichoandika ambacho kinaweza kuifanya serikali itetereke
After all Tanzanian we don't kill for nothing sana sana tuna kutesa kisaikolojia tu.
 
Si uwasiline na muuaji mkuu kuna no yake pale. Usipinge tu moja kwa moja. Lisemwalo lipo mkuu

Muuaji ni nani?

Mnataka tu kuingia nyumba ya mtu halafu mnataka mpitie dirishani?

Nendeni mlango mkubwa mbishe hodi.
 
Ben, una uhakika gani kuwa huyo aliyekutishia ni mtu kutoka serikalini? Isije ikawa umechezewa tu na vijana wa mtandaoni nawe umekimbilia huku kutafuta kiki. Nijuavyo mimi hakuna hitman mjinga aandike vitisho hivyo na namba ya simu juu.

Daima kumbuka kuwa ili chuma kiwe imara ni lazima kipite kwenye fukuto. You will be OK na huko mbele utakuwa mpinzani aliyekomaa. Siasa zina gharama. Good luck!
 
Kuhisi ni HAKI yako iwe umekosea au haujakosea.

So GO AHEAD
 
Ndugu wana JF, ndugu zetu wa Kisomali wana usemi, " MUONGO HUFICHA USHAHIDI WA UONGO WAKE MBALI SANA" hapa Ndugu Ben katuwekea number ya simu inayotumika kumtishia, na ameripoti polisi, kwa hivyo sidhani kama ni habari za kutengeneza.

Japo kuwa nina imani ya kuwa huyo anayemtishia ni mjinga na mtu asiyejua analofanya, kwani amefanya mambo ya kitoto sana. Mwenye nia mbaya na mtu hamshtui mtu bali anatimiza ubaya wake. This is a very cheap act by the culprit.
 
Haha movie za ukawa zimeshaanza. Aisee hawa watu hawaishi vioja.
Mkuu,
Meseji kama hii inaweza kutumwa na mtu mwenye chuki binafsi na Ben au mgonjwa wa akili.

Vile vile kuna watu wengi wanachuki na serikali ya sasa hivi hasa waliokuwa mafisadi wanaweza kufanya jambo lolote la kupuuzi ili kashfa ziende kwa serikali.

Cha muhimu kapeleka polisi na wao wanatakiwa wafanye kazi yao kwa umakini na kumfikisha mtuhumiwa kwenye mikono ya sheria au apelekwe Mirembe kutibiwa.
 
Waafrika hatujijui kwanini tupo duniani.

Hamna hasara kubwa kama kuishi na mjinga.

Ujinga hasara, isikubali hilo
 
Si uwasiline na muuaji mkuu kuna no yake pale. Usipinge tu moja kwa moja. Lisemwalo lipo mkuu
Kuwasilia na aliyekutumia meseji ya vitisho sio jambo la busara hasa kama hujui ni nani aliyekutumia. Kama ni mgonjwa wa akili utakuwa umempa attention ambayo anaitafuta na kuweza kufanya kweli.

Hata polisi wenyewe wakijua unawasiliana na aliyekutumia meseji inaweza kuwapunguzia nguvu ya kufuatilia na mahajamani inaweza kumsaidia mtuhumiwa.
 
we ben acha porojo,kwanza we zulumati mkubwa,siku ya kwanza umejoin hapa jukwaani baada ya wiki alikuja manamke hapa kulalama ulimkopa huko kariakoo,we sasa hizo za kugandia n upambe hazikufikishi kokote laghai mkubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…