Ben Saanane: Ninatishwa kuuawa kwa kuikosoa Serikali

Ben Saanane: Ninatishwa kuuawa kwa kuikosoa Serikali

Kila nikiona hili bandiko naishiwa nguvu,naitafakari nchi yangu na sipati majibu!Nawaza kama ningepewa super powers na nikawajua wahusika,walah hakuna mtu angerudia kufanya unyama kama huu!
Mungu yupo, ndio maana wengine tunaamini kuna siku ya hukumu
 
Hakuna kuonesha utu kwa mpuuzi nilimshauri sana ben mara makamba hakusoma mara mwigulu mara magufuli alijifanya yeye ndio kasoma .pumbavu zake yule dogo
Onesha utu wako Mkuu. Sio kila jambo ni la kutumia nguvu, mengine ni akili tu. Unatumia resources na nguvu kubwa kwa vitu ambavyo unaweza kuvidhibiti na kuvipotezea. Whoever bado wewe binadamu sio mnyama.
 
Hakuna kuonesha utu kwa mpuuzi nilimshauri sana ben mara makamba hakusoma mara mwigulu mara magufuli alijifanya yeye ndio kasoma .pumbavu zake yule dogo
Killings haijawahi kuwasilence watu.

Faida ipi imepatikana zaidi ya kuwa uchi kwenye Jamii.

Kuuwa mtu hakuzui kuvuja kwa Siri.Ujanja ni kuuwa Siri na sio kuuwa mtu.

Ukiuwa mtu ile laana inatembea kwenye uzao wako kuanzia watoto,hata wauaji wengi kiasili wanatoka Koo zenye laana ya mauaji ni laana itembeayo kwenye ukoo.
 
Jamani hivi huyu Kijana ndiyo washamuua ama? mwaka wa nne sasa hawamwachi tu..... if that is the case its too sad!! kuna watu watakuwa kuni siku ya kiama.
 
U kill one rise 10 U kill 10 rise 1000.
Educated and civilized man aogopi criticism Wala kelele za mlango au mbwa kubweka.
 
Hako kadogo GENTAMYCINE kalianza kukurupuka kitambo ila Naona angalau nowdays kamejifunza baadabysie wakongwe kumfunza adabu hapa barazani.
Bila ya Kumzungumzia 'Mumeo' na hata 'Kumtaja' tu hapa husikii raha kabisa. au ndiyo unataka Kuwapiga 'Mikwara' wanaonitaka hapa ili usinikose?
 
Ni uongozi uliogubikwa na ujinga na kutojali. Na ndiyo hatari yake kwa nchi. Mauaji mengi ya kisiasa, wizi mwingi wa kura, pia viamefanywa na watawala wengi barani Afrika. Tofauti ni kuwa hapa kwetu hayo yanafanyika bila kutumia akili. Si kuwa nahalalisha mauaji yeyote ya binadamu, ila mauaji ya kijinga yanaweza pia kusababisha matatizo ya chuki za kijamii zinazoweza kupelekea kwenye mpasuko hasa wa jamii.

Angalia Kenya, hadi leo watu bado wanabishana juu ya nani alimwua Tom Mboya, Josiah Mwangi Kariuki, Ronald Ngala, Robert Ouko….ingawaje kwa jumla inajulikana ni serikali, ila ni vigumu kusema wazi wazi, maana katika visa vyote hivyo, angalau serikali ilifanya uchunguzi, ikajifanya kutoa taarifa na hata kuwapa rambi rambi ndugu na jamaa! Aidha, mauaji yenyewe yamefanywa ki 'janja'. Hivyo hivyo wizi wa kura. Ama hapa kwetu, yeyote anayejitambua ataweza kukwambia nani aliyehusika kumpiga risasi Lissu, nani kampoteza Saa Nane, kamwua Mdude Nyagali, Azory Gwanda.

Ni hii 'carelessness' ya kumwaga damu za watu ndiyo inatishia Zaidi mustakbali wa Tanzania kama taifa lenye jamii iliyoshikana. Huyo anayefanya hivi lazima atakuwa ima ni mgonjwa wa akili, ana chuki ya kupita kiasi na Watanzania, au tu ni katili asiye na huruma, asiyejali sheria wala kumjali Mwenyezi Mungu

! Ugonjwa wa akili ni pamoja na kuwa 'delusional' kwamba ayafanyayo ni kwa manufaa mapana ya Tanzania!
 
Tanzania yangu alafu wanatokea wapuuzi,wajinga , wapumbavu wanakuambia eti hii ni nchi ya amani .
 
Lissu huku walimmiminia risasi za kutosha lakini hakufa, na sasa yuko uhamishoni kunusuru roho yake.
 
Back
Top Bottom