Ni uongozi uliogubikwa na ujinga na kutojali. Na ndiyo hatari yake kwa nchi. Mauaji mengi ya kisiasa, wizi mwingi wa kura, pia viamefanywa na watawala wengi barani Afrika. Tofauti ni kuwa hapa kwetu hayo yanafanyika bila kutumia akili. Si kuwa nahalalisha mauaji yeyote ya binadamu, ila mauaji ya kijinga yanaweza pia kusababisha matatizo ya chuki za kijamii zinazoweza kupelekea kwenye mpasuko hasa wa jamii.
Angalia Kenya, hadi leo watu bado wanabishana juu ya nani alimwua Tom Mboya, Josiah Mwangi Kariuki, Ronald Ngala, Robert Ouko….ingawaje kwa jumla inajulikana ni serikali, ila ni vigumu kusema wazi wazi, maana katika visa vyote hivyo, angalau serikali ilifanya uchunguzi, ikajifanya kutoa taarifa na hata kuwapa rambi rambi ndugu na jamaa! Aidha, mauaji yenyewe yamefanywa ki 'janja'. Hivyo hivyo wizi wa kura. Ama hapa kwetu, yeyote anayejitambua ataweza kukwambia nani aliyehusika kumpiga risasi Lissu, nani kampoteza Saa Nane, kamwua Mdude Nyagali, Azory Gwanda.
Ni hii 'carelessness' ya kumwaga damu za watu ndiyo inatishia Zaidi mustakbali wa Tanzania kama taifa lenye jamii iliyoshikana. Huyo anayefanya hivi lazima atakuwa ima ni mgonjwa wa akili, ana chuki ya kupita kiasi na Watanzania, au tu ni katili asiye na huruma, asiyejali sheria wala kumjali Mwenyezi Mungu
! Ugonjwa wa akili ni pamoja na kuwa 'delusional' kwamba ayafanyayo ni kwa manufaa mapana ya Tanzania!