Ben Saanane: Ninatishwa kuuawa kwa kuikosoa Serikali

[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
 
Humu kuna watu wana akili ndogo, Mimi mpaka kesho naamini hakuna nguvu kubwa iliyihusika kumpoteza huyu

Pengine ni michezo ya Chadema

Sent using Jamii Forums mobile app
Ina maana michezo ya chadema wapo huru kufanya jambo lolote na bila shida wala kuhofia mamlaka na sheria zilizopo kwenye hii nchi ?
 
Uliambiwa hutaandika tena na imekuwa kweli.
 
Kama umeshatangulizwa mbele za haki ambapo wengi wetu bado hatuamini ni kwamba yule jamaa aliyetuma watu wakutende na yeye kashachomolewa huku ! we mcheki cheki huko kwenye msongamano utamwona pembeni kabisa kajisumata tena mwenye huzuni kali.
 
Endelea kupumzika kwa amani Ben
 
Huyu ben saa nane muongo kama viongozi wake wanataka kuanza kama enzi za akina zitto akiwa chadema yeye mwenyewe ben walikuwa wanajiteka halafu wanasema wametekwa.
Rudia kusoma ulichokiandika halafu linganisha na kilichotokea. Mnataka mtu mpaka afe ndo muamini ???
 
HATUJUI ulipo, kama upo jitokeze, kama kuna aliyekutoa uhai na yeye hayupo huenda yupo pembeni yako anatokwa machozi ya damu.
Hakuna anayeishi milele.
 
Kupotea kwa Beni inasikitisha sana ila pia kulikuwa na ulazima gani kuhoji elimu ya mtu tena kwa lugha kali kiasi kile? Mtu mwenyewe ni Rais ambaye kikatiba hashtakiwi. Mbowe na wakubwa wengine wa CHADEMA walishindwa kumshauri kijana kuachana na hilo suala? Au alishauriwa akakataa? Ninawalaani waliohusika na kupotea kwa Beni ila pia ninawalaani CHADEMA kwa kumwacha kijana aingie kwenye mtego mbaya kama ule. Hakuna ushujaa wowote ukishapotezwa. Vijana kuweni makini sana na upotoshaji wa viongozi wa CHADEMA. Wao wakiona hatari mara moja wanakata tiketi za ndege na kukimbilia kwa mabwana zao. Kumdhalilisha rais wa nchi ni hatari kwa maisha yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…