Ben Saanane: Ninatishwa kuuawa kwa kuikosoa Serikali

Ben Saanane: Ninatishwa kuuawa kwa kuikosoa Serikali

Mnaoweka RIP this guy is no more au mnakisia !

"poleni Sana familia ya huyu Kijana "
 
Kwenye kitabu cha Kabendera ameandika jiwe alimfyatua jamaa .

Nilihoji humu kama PhD ya jiwe ilikuwa na uhalali kwanini ifichwe?

Professor George Saitoti PhD yake aliyopata 1975 London tasnifu yake imebandikwa mtandaoni.

Hata William Ruto alitumia miaka 6 kupata PhD yake baada ya kutotimiza vigezo sahihi vya kupata PhD yake na akasisitiza hajutii kwani ndio ilibidi afikie vigezo sahihi ndio apewe na alifuata hatua zote hadi kufanya defence na tasnifu yake iko wazi mtandaoni.

Kwanini tasnifu ya jiwe imetiwa kapuni?

Kama viongozi wanaghushi taaluma wananchi wa kawaida wangapi watakuwa wasomi makanjanja?

R.I.P Ben Saanane
 
Yote hayo ni ujinga tu mkuu! Magufuli alishafikia kiwango cha kuwa Rais kwahiyo hata Ben angehoji vipi asingeweza kuacha kuwa rais sababu ya ben kuhoji PhD yake.

Kwa afrika hii huwa nasema ni upumbavu kwa kijana kuhatarisha maisha eti unapigania haki!

Ona sasa leo hii Ben hayupo na Mbowe ndio huyo tunasanuka kwamba kumbe ni mamluki wa ccm.
 
Yote hayo ni ujinga tu mkuu! Magufuli alishafikia kiwango cha kuwa Rais kwahiyo hata Ben angehoji vipi asingeweza kuacha kuwa rais sababu ya ben kuhoji PhD yake.
Unaweza ukaonyesha ujinga wangu kwa kuonyesha tasnifu ya jiwe ilipo kama ilivyo desturi ya machapisho ya kitaaluma kuwa wazi kwa ajili ya rejea au najadiliana na mtu aliyeishia kidato cha nne na akapiga bashite maana hawezi kujua umuhimu wa hivi vitu.
Kwa afrika hii huwa nasema ni upumbavu kwa kijana kuhatarisha maisha eti unapigania haki!
Kwahiyo ni halali viongozi kukandamiza raia kwa kigezo Africa hakuna haki sasa kile kiapo cha "Nitaihifadhi na kuilinda katiba kwa mujibu wa sheria zilizowekwa" kina umuhimu gani?

Hujui Tanzania kama mwanachama wa umoja wa mataifa ilisaini mikataba ya haki za binadamu na inatakiwa iifuate?

Kwani hujiulizi Makonda alivyofungiwa kwenda Marekani unafikiri walikaa tu wakabuni?
Ona sasa leo hii Ben hayupo na Mbowe ndio huyo tunasanuka kwamba kumbe ni mamluki wa ccm.
Kwahiyo kupotea kwa Ben kumekufurahisha?

Na kuhusu Mbowe kuwa mamluki wa CCM inakuwa ni kesi tofauti , aliyemuu Ben sio Mbowe ni Magufuli umamluki wa Mbowe tutaujadili ila hapa ni issue ya aliyemuua Ben na aliuwawa ikulu sasa Mbowe aliwahi kuishi ikulu 2016?
 
Safari inaendelea. Vitisho. Haya ndiyo maisha yetu ya Kila siku. Mengine tumetoa Ripoti Polisi huko

Kuna watu hawa miongoni mwa wengi. Yeye anaandika "Ben Saanane unachokitafuta ndani ya Serikali hii utakipata. Kwa elimu na uwezo wako hatukutarajia ungefikia hatua ya ajabu kwa namna uliyofikia.

Hujiulizi kwanini upo huru hadi muda huu You are too young to die. Tunajua utaandika na hili. Andika lakini the next post hutaandika ukiwa na uhuru wa kutosha. Andika but your days are numbered. Unajua kuna rafiki yako alipuuza na hutaki kuandika kuhusu yeye labda kwa kuwa alitangulia. Andika Ben. Andika sana, ongea. Sema lakini utajikuta mwenyewe na chatu"

He's such a coward. Muoga. Muaji anayejitangaza nae ana hofu tupu

Nimemshukuru lakini nimemjibu kwa namba yake hii 0768797982 ambayo ipo polisi.

Haya tunasonga mbele Watanzania. Kama ni Uchochezi sidhani kama upo uchochezi mkubwa zaidi ya huu.

As long as tupo hai, Sauti zetu hazitakoma. Tutaandika, Tutasema, Tutahutubia na tutafanya vitendo

Kitu kimoja tu cha hakika ni kuwa Damu ikimwagika hasa damu ya kimapinduzi hutoa mvuke utakaonyesha na kutiririsha mafuriko katikati ya mito na vijito vya haki. Kama itanyesha mvua ya Radi basi itaambatana na mwanga na cheche zitakazowamulika walaghai, watesaji, wakandamizaji wa hakiWatetezi wa haki watapata mwanga katikati ya giza tororo la Unyanyasaji, unafiki na ubakaji wa taaluma na dhamiri zao kitaaluma na kiimani.

Yesu Kristu aliishi miaka 33 tu duniania. Nina Mwaka Mmoja bado. He fought the right cause. Alikuja Duniani kimungu. Kila mtu anaishi kutokana na makusudi ya Mungu. Mwenyezi Mungu huruhusu kila jambo kwa makusudi yake. Sisi ni akina nani tukatae makusudi yake? Hatukujileta Duniani na hatutaishi milele.

Wasichojua watu hawa ni kuwa nilizaliwa na kubatizwa hatari siku hiyohiyo kama Mkatoliki. Ubatizo wa kifo(Hatari) 13 Desemba miaka hiyo, nikapona kwa fadhila zake Muumba. Nimepata fadhila sana Machoni pa Mwenyezi Mungu hadi muda huu. Wanajisumbua! Nimeishi beyond that favour

Oh nakupenda mpenzi wangu Tanzania. I love you more than words can wield the matter, dearer than eyesight, space and Liberty. Oh I love you Tanzania. My Pride, My fountain of inspiration."

Mlale salama marafiki zangu wapendwa.

Mapambano na Yaendelee, Ushindi U Dhahiiri (Aluta Continua, Victory Ascerta)

Pumzika kwa amani Rafiki yangu kipenzi Alphonce Mawazo. Hukukopa, Ulijiandaa kulipa gharama. Ukalipa Deni. Tunasonga Mbele! Nitalitaka Jeshi la Polisi liunganishe ujumbe uliotumwa na kifo chako katika hatua za uchunguzi.

Ben Saanane
Hii thread kila nkiisoma na kuitafakari machozi hunitoka.
Unamuua mwenzako leo kesho kutwa unakufa kwa ugonjwa.
Betting wanaita "All team to score-GG"
 
Unaweza ukaonyesha ujinga wangu kwa kuonyesha tasnifu ya jiwe ilipo kama ilivyo desturi ya machapisho ya kitaaluma kuwa wazi kwa ajili ya rejea au najadiliana na mtu aliyeishia kidato cha nne na akapiga bashite maana hawezi kujua umuhimu wa hivi vitu.

Kwahiyo ni halali viongozi kukandamiza raia kwa kigezo Africa hakuna haki sasa kile kiapo cha "Nitaihifadhi na kuilinda katiba kwa mujibu wa sheria zilizowekwa" kina umuhimu gani?

Hujui Tanzania kama mwanachama wa umoja wa mataifa ilisaini mikataba ya haki za binadamu na inatakiwa iifuate?

Kwani hujiulizi Makonda alivyofungiwa kwenda Marekani unafikiri walikaa tu wakabuni?

Kwahiyo kupotea kwa Ben kumekufurahisha?

Na kuhusu Mbowe kuwa mamluki wa CCM inakuwa ni kesi tofauti , aliyemuu Ben sio Mbowe ni Magufuli umamluki wa Mbowe tutaujadili ila hapa ni issue ya aliyemuua Ben na aliuwawa ikulu sasa Mbowe aliwahi kuishi ikulu 2016?
Leta picha tuthibitishe magufuli alimuua Ben saa nane sababu yote tunaona maandishi tu ambayo hata Mimi naweza kuapka nikaandika lasivyo ni uzushi na chai hizi hatunywi
 
Leta picha tuthibitishe magufuli alimuua Ben saa nane sababu yote tunaona maanadishi tu ambayo hata Mimi naweza kuapka nikaandika lasivyo ni uzushi na chai hizi hatunywi
Ukiletewa picha utasema edited ama Ai watu wa namna yako hawajawai kukosa vijisababu ili kuficha adhma zao .
 
Ukiletewa picha utasema edited ama Ai watu wa namna yako hawajawai kukosa vijisababu ili kuficha adhma zao .
Leta picha kelele za nini hatuwezi kuamini maandishi ambayo hata Mimi naweza kuamka nikaandika na anaeandikiwa ni marehemu hawezi kujitetea leta picha tuamini
 
Leta picha tuthibitishe magufuli alimuua Ben saa nane sababu yote tunaona maandishi tu ambayo hata Mimi naweza kuapka nikaandika lasivyo ni uzushi na chai hizi hatunywi
Na mimi nakupa kazi nyepesi mletee Ben Saanane utegue kitendawili hiki maana mtu hajaonekana tangu 2016 na hatujui alipo halafu mtu kasema aliuwawa wewe unabisha basi tueleze alipo ikiwezekana umlete.

Na huu uzi ni anaeleza anatishiwa kuuwawa huwezi kutumia akili ya kuzaliwa baada ya tishio la kuuwawa na mtu mwaka wa 8 hajaonekana ameenda wapi kama hajauwawa.?
 
Back
Top Bottom