Ben Saanane: Ninatishwa kuuawa kwa kuikosoa Serikali

Ben Saanane: Ninatishwa kuuawa kwa kuikosoa Serikali

Safari inaendelea. Vitisho. Haya ndiyo maisha yetu ya Kila siku. Mengine tumetoa Ripoti Polisi huko

Kuna watu hawa miongoni mwa wengi. Yeye anaandika "Ben Saanane unachokitafuta ndani ya Serikali hii utakipata. Kwa elimu na uwezo wako hatukutarajia ungefikia hatua ya ajabu kwa namna uliyofikia.

Hujiulizi kwanini upo huru hadi muda huu You are too young to die. Tunajua utaandika na hili. Andika lakini the next post hutaandika ukiwa na uhuru wa kutosha. Andika but your days are numbered. Unajua kuna rafiki yako alipuuza na hutaki kuandika kuhusu yeye labda kwa kuwa alitangulia. Andika Ben. Andika sana, ongea. Sema lakini utajikuta mwenyewe na chatu"

He's such a coward. Muoga. Muaji anayejitangaza nae ana hofu tupu

Nimemshukuru lakini nimemjibu kwa namba yake hii 0768797982 ambayo ipo polisi.

Haya tunasonga mbele Watanzania. Kama ni Uchochezi sidhani kama upo uchochezi mkubwa zaidi ya huu.

As long as tupo hai, Sauti zetu hazitakoma. Tutaandika, Tutasema, Tutahutubia na tutafanya vitendo

Kitu kimoja tu cha hakika ni kuwa Damu ikimwagika hasa damu ya kimapinduzi hutoa mvuke utakaonyesha na kutiririsha mafuriko katikati ya mito na vijito vya haki. Kama itanyesha mvua ya Radi basi itaambatana na mwanga na cheche zitakazowamulika walaghai, watesaji, wakandamizaji wa hakiWatetezi wa haki watapata mwanga katikati ya giza tororo la Unyanyasaji, unafiki na ubakaji wa taaluma na dhamiri zao kitaaluma na kiimani.

Yesu Kristu aliishi miaka 33 tu duniania. Nina Mwaka Mmoja bado. He fought the right cause. Alikuja Duniani kimungu. Kila mtu anaishi kutokana na makusudi ya Mungu. Mwenyezi Mungu huruhusu kila jambo kwa makusudi yake. Sisi ni akina nani tukatae makusudi yake? Hatukujileta Duniani na hatutaishi milele.

Wasichojua watu hawa ni kuwa nilizaliwa na kubatizwa hatari siku hiyohiyo kama Mkatoliki. Ubatizo wa kifo(Hatari) 13 Desemba miaka hiyo, nikapona kwa fadhila zake Muumba. Nimepata fadhila sana Machoni pa Mwenyezi Mungu hadi muda huu. Wanajisumbua! Nimeishi beyond that favour

Oh nakupenda mpenzi wangu Tanzania. I love you more than words can wield the matter, dearer than eyesight, space and Liberty. Oh I love you Tanzania. My Pride, My fountain of inspiration."

Mlale salama marafiki zangu wapendwa.

Mapambano na Yaendelee, Ushindi U Dhahiiri (Aluta Continua, Victory Ascerta)

Pumzika kwa amani Rafiki yangu kipenzi Alphonce Mawazo. Hukukopa, Ulijiandaa kulipa gharama. Ukalipa Deni. Tunasonga Mbele! Nitalitaka Jeshi la Polisi liunganishe ujumbe uliotumwa na kifo chako katika hatua za uchunguzi.

Ben Saanane
Ben Ben Ben!
 
Huu uzi utaendelea kuishi , tatizo lilianza taratibu na wengine wakakebehi na kuchukulia kama mzaha.

Tutaendelea kukumbushana tu kila tatizo lina chanzo haliibuki tu.

Na kila kiongozi atakumbukuwa kwa aliyoyafanya watu wasipangiwe kukumbuka ya upande mmoja tu .
 
Ben acha huu upotoshaji kama unajiita wewe kidume basi endelea ila mimi ni shahidi ndani ya mtandao huu umeshaonywa sana.
Ila mimi nataka kukutabiria jambo. Kama kweli hutobadilika nakuendelea na hii mambo basi kifo chako hutopata nafasi kuja kuandika humu na kwa bahati mbaya watu watakuwa wameshasahau sana sana watajuwa umekufa kama binadam wengine ila kumbuka huna uharakati wowote my dia hata punje ya Dr Ulimboka huna sasa jiangalie usitafute umaarufu wakati kifaru kiponjiani unakizuia kisipite kwa mwili wa nyama utakufa na hao unao walaani wala haiwapati... Take care this is a nation kaa mbali
How do you feel now?
 
Wewe damu ya Ben inakulilia, hautabaki salama ni swala la muda tu.

Note this.
 
Huu uzi utaendelea kuishi , tatizo lilianza taratibu na wengine wakakebehi na kuchukulia kama mzaha.

Tutaendelea kukumbushana tu kila tatizo lina chanzo haliibuki tu.

Na kila kiongozi atakumbukuwa kwa aliyoyafanya watu wasipangiwe kukumbuka ya upande mmoja tu .

Saed Kubenea kupitia gazeti la mwanahalisi alieleza kila kitu kuwa Ben Saanane alitekwa na Mbowe na kwa muda fulani alionekana kwenye vijiwe vya kahawa
 
Unamuuliza Saed Kubenea aliyetafiti na kuandika kupitia gazeti lake la Mwanahalisi ( wakati Kubenea anaandika alikuwa mbunge wa Chadema ubungo) au unaniuliza mimi?
Ninakuuliza wewe hapo.

Huu uzi kuna mahali Ben alimtaja Kubenea au Mbowe ?

Mbowe au Kubenea walikuwa watu ambao Ben aliwakosoa kipindi hicho hadi wamuwinde?

Labda mtoto mdogo na ambaye hakuwa mfuatiliaji ndio hatojua Ben aliyekuwa akimkosoa sana nani.

Huu ndio uzi wa mwisho wa Ben kuandika na hajawahi kuonekana tena wewe unaleta story za kipuuzi hapa .
 
Back
Top Bottom