Ben Saanane: Ninatishwa kuuawa kwa kuikosoa Serikali

safi sana mkuu!
 
Dah mtu anatishiwa uhai wewe unakuja kumkebehi,yu wapi sasa ben saanane?
 
mkuu u hali gani?
Huyo member nae alishafariki pia , kwa kipindi hicho Magufuli apologists akiwemo huyo member ulikua huwaambii kitu kuhusu kupotea watu wao waliamini ndio wana funguo za uhai wa maisha ya watu na wakitaka kukuondoa tu wanaweza kufanya muda wowote wawezavyo na hakuna wa kuwauliza

Leo hii ni mwaka wa 10 Ben alishafariki , na Kabendera aliweza kutueleza namna gani Ben aliuwawa kikatili na sasa Magufuli amefariki na huyo member nae aliyekebehi hapo naye amefariki.

Ni somo kubwa tunatakiwa tulipate kuwa uhai wa mtu hauthaminishwi na daraja la kilomita 10, wala barabara ya lami, wala reli ya mwendokasi.
 
Upo sahihi mkuu lakini hii dhana inamgogoro,

Wema hawafi? wenye kuhurumia wengine hawafi?

KWanini muovu au mtu anayechekelea uovu akifariki baada ya muda mfupi hua jama ni furaha ? Wakati katika kipindi hiko wema nao wanakufa?
 
Upo sahihi mkuu lakini hii dhana inamgogoro,

Wema hawafi? wenye kuhurumia wengine hawafi?
Mimi siungi mkono hii kauli ya Makamba, ninachoamini kila mtu atakufa awe mwema au awe mkatili , nilichomaanisha ni kuwa hao makatili wanaoua watu huwa wanajisahau sana kwamba wakidhani wao wataishi daima.

Mimi nakupa mfano rahisi tu mkuu , Polepole pale alipokua amekaa kavamiwa kapigwa na kuuwawa tumeona michirizi ya damu tu.

Anakuja mtu na hoja kwamba hakuwepo Tanzania mara alirudi lini, hivi mkuu kama mama yake anawaambia mwanae alikuwepo pale siku zote na tunaona hadi meza , kiti na vitu kadhaa ambavyo amewahi kuonekana navyo bado mtu anasimama na kusema yupo kajificha Sweden na ni mwezi wa 3 sasa familia inamtafuta?

Ukinisoma hapo vizuri utaelewa kwamba huu mtindo ulioanzishwa wa kuteka na kuua watu sio mzuri , hao walioenda kumteka na kumuua walitumwa wamemaliza kazi wamelipwa , nini kinafuata hizo pesa zitawasaidia kununua oxygen ya kutosha wasiwahi kufa??

Jibu ni hapana , ni lazima kama nchi watu wote waamke na wawe sober kukataa huu upuuzi mtu kama amekosea afikishwe kwenye vyombo vya sheria na si kumuua , mimi sioni sababu ya kumuua mtu ili mawazo yake aidha yawe mazuri au mabaya yasisikike .

Mimi nimefanikiwa kufika katika nchi kadhaa na kuona jamii zilizoathirika kwa madhara ya visasi vya vizazi hadi vizazi hilo ninakuhakikishia kwa wanaoona kwa sasa sawa kupoteza watu watawaachia mbeleni mzigo wa mateso watoto hadi wajukuu zao mimi nimeshuhudia baadhi ya koo zikifutwa kabisa uzao mzima kwa sababu ya kulipia madhila waliyotenda watangulizi wao wa kifamilia , hivyo kama haya mambo yanaonekana kawaida mbeleni muda utakua hakimu mzuri kutupa majibu na huenda hizi familia zinazoonekana zina nguvu na kila kitu kutishia watu na kuwaua usalama wao utakua kwa kuomba hifadhi na kuhama kabisa nchi.

Hivyo hii habari ya kutekana na kuua watu wala siikubali hata kidogo iwe leo kesho hata keshokutwa.
KWanini muovu au mtu anayechekelea uovu akifariki baada ya muda mfupi hua jama ni furaha ? Wakati katika kipindi hiko wema nao wanakufa?
Nimekujibua kwa kirefu hapo juu mkuu.
 


Kuhisi wanaofanya maovu hawajui kama na wao watakufa ni dhana potofu
 
Ulishawahi kuwasikia hao jamaa wakitamba?

Nenda kasikilize mahojiano ya Mello na Khalifa.

Wasipotamba wanabadilisha chochote?

Imagine watu wanasikia gari la polisi limepata ajali wanashangilia kweli kweli,

Unauhakika gani pale kama hakuna polisi wema na waliokua wanasupport mapambano?


Akifa tunayempenda sisi unasikia masikini alikua na watu wanamtegemea, wale polisi tunauhakika gani hakuna watu wanaowategemea?
 
Wasipotamba wanabadilisha chochote?
Kwa maoni yako uko sawa kwao si sawa.
Imagine watu wanasikia gari la polisi limepata ajali wanashangilia kweli kweli,

Unauhakika gani pale kama hakuna polisi wema na waliokua wanasupport mapambano?
Unafikiri watu walifikaje hapo kuanza kushangilia vifo vya wanaccm, polisi na watu wanaohusishwa na hicho chama?

Mkuu kila tatizo lina chanzo , watu wanatekwa, kuuwawa, kulawitiwa na kundi lenye mamlaka, amri, pesa na silaha unafikiri wao wasio na silaha wapi watatatuta namna ya kuonyesha machungu yao ??

Ukifikiri kwa kina utajua kabisa hilo tatizo halina muda mrefu na chanzo chake kinajulikana na watu nao wakaja na njia ya kutolea machungu yao.
Akifa tunayempenda sisi unasikia masikini alikua na watu wanamtegemea, wale polisi tunauhakika gani hakuna watu wanaowategemea?
Ndio maana nikasema tatizo wakati limeanza kumea mizizi lilitakiwa serikali ichukue hatua .

Serikali ina rasilimali zake za kutosha tu kuweza kuzuia watu wake wasitekwe, kuuawawa, kulawilitiwa.

Sasa fikiria mtu anachoma picha ya mtu aliyochora mwenyewe anapotea takriban mwaka wa 2 sasa na unataka uwaaminisheje familia yao , wakuchekee?

Mtu anavamiwa na watu wanakwambia walioingia hapa walikua wanasema ni polisi wakampiga na nyundo kichwani wakaondoka nae na michirizi inaonekana ya damu.

Halafu wanaotakiwa kuchunguza wanasema uchunguzi unaendelea inapita wiki, miezi ,mwaka , miaka kimya.

Hadi hapo huyo mtu unataka marafiki, mke , watoto, wajomba, n.k wakuchekee??

Tusizunguke , tabia ya kushangilia vifo ina chanzo chake na chanzo ni rahisi tu kukijua kua kuna kundi limeonekana linatekwa, kupotea , kulawitiwa, kuuwawa na kundi lingine lenye dola na wala halijali sasa kundi linaloonekana halina vyote hivyo likaja na njia ya kuonyesha machungu kwa kushangilia vifo vya kundi lingine ili nao wakati wa majonzi wapate kusikia kile wanachosikia wakipotelewa na ndugu zao.
 
Reactions: Lax
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…