sikuwa namfuatilia huyu jamaa
Ben Saanane lakini nilishangaa kila nikipita kununua gazeti naona kupotea kwa Ben saanane.Nimeamini kuna watu wakiamua kukuwinda huwezi vuka hata umbali wa kiwanja,,ukifuatilia uzi huu na wachangiaji unaweza pata picha kuwa kuna waliokuwa wanaelewa ambacho kingempata Ben Saanane na walianza kumuonya mapema,,achilia mbali waliokuwa wanamwona mpuuzi;Kama kuna sehemu watu wenye ajenda kama za Ben wanafichwa,basi huyu Mtanzania atakuwa hai lakini kwenye mateso yasiyoelezeka,lakini kama alishazimisha jumla apumzike kwa amani,hata watesi wake watamkuta huko ahera.