Ben Saanane: Ninatishwa kuuawa kwa kuikosoa Serikali

Ben Saanane: Ninatishwa kuuawa kwa kuikosoa Serikali

Unajua kuna rafiki yako alipuuza na hutaki kuandika kuhusu yeye labda kwa kuwa alitangulia.Andika Ben.Andika sana ,ongea.Sema lakini utajikuta mwenyewe na chatu"

Ben Saanane

Kuna mtu mmoja juzi juzi tena ni mwana ccm kindakindaki aliniambia kwamba yule mtesaji mkuu kama mnamkumbuka aliyemtesa Dr. Ulimboka anaitwa Ramdhani Igondu hii mbinu ya kuwapeleka watu chumba cha giza chenye chatu ndo huwa anaitumia. Kwa hiyo kilichoandikwa hapo siyo utani, watu kabla hawajafa wanapitia torture za hali ya juu.
 
Kipindi unaandika haya ulikuwa hujui hata kwamba kuna namba zinakwambia ile ela tuma kwa namba hii? Au haukujuwa kwamba kuna namba zinatumika mtu au kikundi cha wahalifu kujifanya customer care wa tigo? Je msimamo wako leo ni upi?
 
Ben Saanane wa.se.nge hawakutaka wakosolewe. Yaliyoko gizani siku moja yatawekwa mwangani.
 
Hiki ndicho kilichomuua Ben Saanane. Watu wasiojulikana ndio walifanya haya mauaji. Mtu ukihoji tu, wasiojulikana wanakuja kukuua! Hakuna kiumbe kitakachoishi milele. Hata wauaji nao ipo siku watakata roho (kwa sababu yoyote ile).
 
Nmepitia huu uzi mwazo mpaka mwisho. Baada ya comment ya GENTAMYCINE nilitegemea kuja kuona comment yake ya pili aidha akileta ushahidi wa kumuumbua @bensaanane au akiomba samahani na kurekebisha kauli yake. Mpaka sasa yupo kimya.
 
Ben acha huu upotoshaji kama unajiita wewe kidume basi endelea ila mimi ni shahidi ndani ya mtandao huu umeshaonywa sana.
Ila mimi nataka kukutabiria jambo. Kama kweli hutobadilika nakuendelea na hii mambo basi kifo chako hutopata nafasi kuja kuandika humu na kwa bahati mbaya watu watakuwa wameshasahau sana sana watajuwa umekufa kama binadam wengine ila kumbuka huna uharakati wowote my dia hata punje ya Dr Ulimboka huna sasa jiangalie usitafute umaarufu wakati kifaru kiponjiani unakizuia kisipite kwa mwili wa nyama utakufa na hao unao walaani wala haiwapati... Take care this is a nation kaa mbali
Halafu Polisi wanamuweka ndani Max Melo kwa kutaa kutoa details za mtu ambaye alikuwa yupo kimaslahi ya nchi, lakini wauwaji kama huyu Polisi haina habari nao wala haiwahitaji.
Republic of Gangstars.
 
ANAYEUA KWA UPANGA NAYE ATAUWAWA KWA UPANGA. MALIPO NI HAPAHAPA DUNIANI.
 
Alphonce Mawazo (rip) ameuwawa kinyama na hakuna mtuhumiwa wala uchunguzi wo wote. Ben Sanane ametoweka katika mazingira tatanishi na hakuna mtuhumiwa wala uchunguzi wo wote. Tundu Lissu amemiminiwa risasi kuliko afanywavyo jambazi sugu na hakuna mtuhumiwa wala uchunguzi wo wote. Leo hii libinadamu linaamka asubuhi na kutangaza eti linajivua uanachama na ubunge wa CDM ili kuunga mkono jitihada za sijui nani!!! Nisingekuwa naogopa ban, ningeyatukana matusi ya nguoni.
 
Kama damu yake imemwagwa basi ni dhahiri inalia, na kilio chake ni kikali mno, haiwezi kunyamaza mpaka ipatiwe haki yake, ole wao waliotenda waliyoyatenda juu yake, hawatapata amani mioyoni mwao kamwe, wataweweseka na kuweweseka siku zote!
 
Nmepitia huu uzi mwazo mpaka mwisho. Baada ya comment ya GENTAMYCINE nilitegemea kuja kuona comment yake ya pili aidha akileta ushahidi wa kumuumbua @bensaanane au akiomba samahani na kurekebisha kauli yake. Mpaka sasa yupo kimya.
Post yake naikumbuka sana huyu jamaa, hujifanya mjuaji kwa kila jambo,anapenda sana attention. Hana tofauti na britanicca yule tapeli alie kula dolali za watu akijifanya agent, eti nae siku hizi ni mtoa mada mkuu jukwaa la siasa
 
Ben, ulitimiza wajibu wako... Hukuogopa kifo hata kilipokuraribia, ulitetea ukweli. Na rekodi za dunia zinaonesha, hakuna mtetezi wa ukweli aliyeishi bila misukosuko na/au kifo kutoka kwa watawala wa dunia. Popote pale ulipo, Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema akurehemu... Kama walikuua kweli, damu yako iwe laana yao wao na vizazi vyao vyote...
 
Back
Top Bottom