Ben Saanane: Ninatishwa kuuawa kwa kuikosoa Serikali

Ben Saanane: Ninatishwa kuuawa kwa kuikosoa Serikali

Hakuna kitu kinaniudhi kama kuwa na chama cha upinzani harafu hakiwezi hata kulipiza kisasi

Sent using Jamii Forums mobile app
Kinacho umiza huyu nae ni binadamu, ana familia, anawazazi, ana ndugu na marafik..... Kuna adhabu nyingi ambazo angepewa tofauti na aliyo pewa, wangemfanya hata kama Dr Ulimboka, then angetulia tu.
 
Mbona tunakumbushana maumivu.?
Hatunabudi kukumbuka. Kuna watu wengi hawajui yaliyomkuta Ben yalishapangwa, alikuwa tayari kupambana kwa ajili ya kweli.

Bado wapo leo hii utasikia wakileta utani kwenye mambo haya. Tuna hatari iliyo dhahiri, tulijitakia...tutayapata sawasawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yohana Mbatizaji au Nabii Yahaya alipinga kitendo cha Mfalme Herode kuumnyanganya ndugu yake Mke na kumuoa yeye.
Mfalme aliamua kukubaliana na ombi la ninti yake la kumkata kichwa Yohana Mbatizaji .
Wakati huo wapambe wa Herode walimshangilia sana lakini Karne nyingi sasa bado Herode analaaniwa kwa kumuua Nabii mkubwa sana aliyemtangulia Masihi Issah bin Mariam au Yesu Kristo au Jesus Christ.

Ni jambo baya na kwa wakuu kumwaga damu za wanaharakati mana wengi ni sauti za Mungu kuwarekebisha watawala ambao wanatisha na wana mamlaka makubwa na wanahofiwa na kuogopwa na kila mtu wa kawaida.
Sauti za Mungu pekee zimewekwa kwa watu Jasiri wasiohofia maisha yao kukatizwa.

Hakika Ben alikua ni MTU wa Mungu na atakumbukwa milele lakini waliokatiza maisha yake wamejificha mana wanahofu mana wanajua walichofanya ni uovu na kamwe hawataenziwa wala kuwekwa kwenye kumbukumbu ya huo uovu.
Kumuua mtu lingekua jambo la kishujaa basi wasiojulikana wangejitokeza hadharani na kujitaja kwa majina na kuelezea jamii ili wajulikane.
Wamefanya uhalifu gizani lakini Muumba wa Mbingu na ardhi amewaona.
Roho zao zinajihukumu. Wataishi kwa ujira wa damu. Damu itawaandama hata kizazi cha tatu na cha nne.

R I P. Been Saanane ,mzalendo wa kweli na sauti ya Mungu kwa wanadam.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatunabudi kukumbuka. Kuna watu wengi hawajui yaliyomkuta Ben yalishapangwa, alikuwa tayari kupambana kwa ajili ya kweli.

Bado wapo leo hii utasikia wakileta utani kwenye mambo haya. Tuna hatari iliyo dhahiri, tulijitakia...tutayapata sawasawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Dada yangu ben nilkkuwa nikifahamiana nae kama bro, rafiki wa karibu na zaidi ndugu. Moyo wangu unasononeka kwasababu yake, alie'injinia kumteka MUNGU amlaani yeye na vizazi vyake.
 
Mkuu hujamaliza maisha hapa duniani, acha dhihaka, kumbuka ben anandugu jamaa na marafiki wanaohuzunika. Its better ukabaki silence
Nazungumzia CHADEMA si ndugu zake na angalia niliyemnukuu aliandika nini??
 
Ndio nakwambia acha dhihaka chadema wanamiliki vyombo vya usalama.. Wao hawana option yeyote zaidi ya kupaza sauti sehemu mbalimbali iwe jf au popote.
Umesoma alichoandika? Yeye kasema CHADEMA ni chama dhaifu kinachoshindwa kulipiza kisasi. Mimi nimemuuliza anataka hicho kisasi kilipizwaje?

Unaona maelezo yako yanaoana na mtiririko wa mjadala wetu?
 
Umesoma alichoandika? Yeye kasema CHADEMA ni chama dhaifu kinachoshindwa kulipiza kisasi. Mimi nimemuuliza anataka hicho kisasi kilipizwaje?

Unaona maelezo yako yanaoana na mtiririko wa mjadala wetu?
Nimekuelewa mkuu nilkosea ku'quote kwasababu ya panic ujumbe wangu ulikuwa special kwa huyo jamaa
 
Ben makonda siku hizi anazurura kwenye makanisa kulia Lia tu kaza uzi ukimlilia Mungu mkuu amlipie kisasi hata huyo mtoto wake wakichana apate laana yake hadi kizazi cha nne
 
Back
Top Bottom