Benaco Ngara: Madereva wa Malori wa Tanzania, wamejichukulia sheria mkononi kuzuia Malori yote kutokea Rwanda kuingia nchini

Benaco Ngara: Madereva wa Malori wa Tanzania, wamejichukulia sheria mkononi kuzuia Malori yote kutokea Rwanda kuingia nchini

Madereva wa Rwanda wanaingiaje kwenye Nchi yenye Corona si na wao wataambukizwa. Wabaki kwao ili kuondoa muingiliano na nchi yenye Corona. Kuwazuia ni sahihi kabisa ili wasiambukizwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unamzuia jirani yako asiingie kwako kwa vile ana corona halafu wewe unamfuata nyumbani kwake!
Ajabu!
Hujasikia hao wakilalamika wanavyonyanyapaliwa? Hujaona hapo wanasema kuwa wakipishana na watanzania wanajipulizia sanitizer?
 
100%

Na tuliwapa eneo la kuzika ndugu zao pale maeneo ya magereza, bado wanatufanya mafala.

Kila mtu na abakie kwao.

No need ya kubembelezana,
Ndio hivo hakuna tena muda wa kubembelezana hapa, ndio mana mzee JK alitakaga kuwatwanga hawa kumbe ni wapuuzi kiasi hiki?
Nilishangaa mtu mpole kama JK lakini anafikia hatua uzalendo unamshinda!!
Hawa watu hawavumiliki hawa!!
 
Nadhani huu ni uzembe wizara ya mambo ya ndani. Walipaswa kuwa wameweka itaratibu.

Kutokuwa na sera ya pamoja kwenye vita na ugonjwa huu itatusumbua sana. A common protocol kwa EAC ingalikuwapo haya yasingetokea.
 
Hujasikia hao wakilalamika wanavyonyanyapaliwa? Hujaona hapo wanasema kuwa wakipishana na watanzania wanajipulizia sanitizer?
Maana yangu ni kwamba ikiwa Rwanda wanazuia watanzania kuingia kwao kwa sababu wana corona, kwa nini wanakuja TZ kwenye corona?
 
picha kubwa (sijui kama utaelewa though)..... katika ushindani wa kibiashara miongoni mwa nchi zenye bandari, ni Tanzania ndiyo inayozihitaji land-locked countries zaidi kuliko kinyume chake.
Hata siku moja serikali ya nchi hii haijawahi kujiendesha kibiashara ingekuwa hivyo tusingekuwa na ukiritimba wa kiasi hiki. Fungua biashara ukutane na TRA,TPA, TMDA,TBS, WAKALA WA MISITU, FIRE,SUMATRA,NSSF, BRELA, HALMASHAURI etc halafu utakuja na mrejesho kama wapo business minded.
 
Unajua kuna mpango wa kujenga Reli kwenda Rwanda? Unajua unapoitaja Rwanda unaitaja Mshariki ya Kongo? Mbali ya hizo nchi nyingine ni Rwanda ndiye inategemewa mizigo mingi kupitia kwake.
Sasa mkuu akigombana na majilani wote atapitisha wapi na yeye mizigo yake.
Uganda hapapitiki kwenda Kenya M7 atawanyuka.
TZ napo ndio hivo wanataka kunyea kambi, watapita wapi sasa?
 
Rwanda hawana shida kivile. wana option ya kutumia bandari ya Mombasa kupitia Uganda.

afterall ni route ambayo ni less risky vs COVID-19 because marais wa Kenya na Uganda wanajua wanachokifanya linapokuja suala la korona.
kwani mpaka wa uganda na rwanda umeshafunguliwa mkuu ?
manake kuna kipindi walifungiana mipaka baada ya pk kumzingua m7

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi sio wapole ni wajinga!

Tangu Madereva wetu walalamike kwamba wanazuiwa kwenda Rwanda zimepita siku ngapi. Uliona kiongozi yeyote wa Tanzania amelizungumzia hilo suala ama hata wanadiplomasia wetu kwenda Rwanda kushughulikia jambo hilo kwa maslahi ya Tanzania?
Mkuu usiseme sisi wajinga, hatuwezi kwenda kulia lia kwao wakati mamlaka zao zipo? Kwani serikali ya Rwanda hawakuona huo unyanyasaji kuwa ni makosa wachukue hatua stahiki? Au hadi tuende sisi kubembeleza?

Tangu wao waje huku kama wakimbizi miaka na miaka lini sisi tuliwanyanyasa mkuu.
 
Mkuu usiseme sisi wajinga, hatuwezi kwenda kulia lia kwao wakati mamlaka zao zipo? Kwani serikali ya Rwanda hawakuona huo unyanyasaji kuwa ni makosa wachukue hatua stahiki? Au hadi tuende sisi kubembeleza?
Kwenye hili ni sisi ndio tulitakiwa tupeleke maafisa wetu wa diplomasia kwa kuwa maslahi yetu ndiyo yanahujumiwa!!
 
Baada ya kunyanyasika vilivyo nchini Rwanda madereva wa malori wa Tanzania wamejichukulia sheria mkononi kuyazuia malori yote kutokea Rwanda kuingia nchini.

Inasemekana baada ya Rwanda kuudhibiti ugonjwa wa Corona vilivyo nchini mwao, kitisho pekee kwa sasa kimebakia kuwa kutokea kwa wageni wanaoingia nchini mwao.

Katika hili inasemekana madereva wa malori kutokea nje wamekuwa ndiyo kitisho kikubwa. Takwimu zinaonyesha kuwa madereva kadhaa tokea Tanzania wamepatikana na virusi hivyo kwenye kuingia huko. Kutokana na hali hiyo, inasemekana Rwanda imebadilisha utaratibu wa malori kuingiza mizigo na sasa kuwataka madereva wa kutoka nje (Tanzania) kuishia mpakani. Utaratibu mpya unawataka madereva walioko (salama) ndani ya Rwanda pekee kuyafikisha malori Kigali na kuwarudishia mpakani.

Utaratibu wa ajabu kabisa. Nani atamwamini mtu asiyemjua na gari lake? Kujibu hilo madereva wa Tanzania nao wamechukua hatua zao na kuanzia jana inasemekana hali huko ni tete. Hakuna lori kutoka Rwanda wanaloliruhusu kuingia nchini. Vinginevyo nao wanawataka waishie mpakani kwa hali ile ile kama inavyotakiwa kwa wetu kufanya.

My take: Serikali inabidi kuingilia kati haraka iwezekanavyo na kuchukua hatua. Yawezekana hawa ndugu tuliowaachia mpaka wazi kwa kuwahurumia ya kwamba watataabika mno, huruma yetu hawaihitaji kabisa!

Kudos madereva wetu si mbaya mkuki kwa nguruwe kuwa ni ule ule kwa binadamu pia.
View attachment 1440166
]

View attachment 1440167
View attachment 1440140
tu



















































































tume tuma kikosi kazi hapo watapata bakora moto moto ndani ya saa moja mpaka wawaruhusu
 
kumbe inapita,sasa tatizo la rwanda ni mizigo ma corona??

Sent using Jamii Forums mobile app
Rwanda wanafanya siasa siasa tu. Hiyo ndiyo inaitwa "Diplomasia ya kiuchumi" inayotokana na "Ujasusi wa Kiuchumi" na nchi inayoathirika zaidi ni ili yenye "Uchumi dola".

Ukisikia vita ya kiuchumi ndiyo hiyo. Ni kama Marekani na China mambo ni kuviziana, atakayezubaa ndiye atakayeathirika.
 
Museveni na Kagame wanajuana kuliko sisi tunavyowajua!
sasa kama wanajuana sana ndo sababu ya kupelekeana majeshi mpakani na kufungiana mipaka.
hivi unajua m7 aliua mwanamke jasusi wa kinyarwanda alitumwa na pk ?
hivi unajua m7 ana wanyarwanda kawahifadhi pk anawataka akawaue ?

maana yangu wangepatana na wakawa na urafiki mkubwa kwa kuwa wanajuana .lkn imekuwa kinyume chake.wamekuwa ndo maadui wakubwa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom