Benaco Ngara: Madereva wa Malori wa Tanzania, wamejichukulia sheria mkononi kuzuia Malori yote kutokea Rwanda kuingia nchini

Benaco Ngara: Madereva wa Malori wa Tanzania, wamejichukulia sheria mkononi kuzuia Malori yote kutokea Rwanda kuingia nchini

That is the point. Hawa ma-failures hawalioni hilo. kazi yao ni kupiga kelele barabarani kama kwenye hizo video. Wanataka nchi zisilinde watu wake kama Rais wao anavyofanya. Kama Tanzania tumeshindwa kudhibiti ugonjwa, Kagame na wengine wana haki ya kutufungia mpaka.

Mathalani Malawi ina wagonjwa wa corona 41, kati ya hao, 13 ni madereva wa malori Watanzania. Na wengine wengi ni Watanzania wasiokuwa madereva wa malori. Sasa Malawi ikichukuwa hatua za kujilinda, hawa vilaza wanakasirika! Ni sawa na yule anayekasirikia misikiti na makanisa kufungwa. Kweli mtoto wa nyoka ni nyoka.
I meant exactly every word.

Rwanda ana options za kutumia Mombasa, Beira or even Durban or Angola.

Tanzania akisusiwa na all landlocked countries kwa sababu za kizwazwa maana yake bandari zake zitakuwa zina operate under capacity na kwa hasara, etc.
 
Sasa wanaingia Tanzania kufanya nini kama wanaona kuna Corona.
 
Bwana dereva, Wanyarwanda hawana kosa lolote hapa. Kuna visa vingi sana vya madereva wetu vya corona huko Uganda, Malawi na Rwanda. Malawi mpaka sasa, kati ya wagonjwa 41 wa corna, 13 ni maderva kutoka Tanzania. Sasa mnataka nchi zote ziwe kama ya kwenu. Kama ndio mawazo yenu haya, kumbe huyu Rais wenu pia alitakiwa kuwa dereva. Mnafikiri nyie ndio mna bandari tu? Ngoja waende Mombasa na Beira muone. Yaani nchi kuchukuwa hatua sitahiki za kujilinda, nyie inawakera. Mlitaka iwe kama Tanzania, siyo? watu waanze kuzika usiku Rwanda, Uganda, Malawi.... Siyo sahihi kabisa.
Sasa wanafata nini huku kwenye corona rais wao awaambie na wao mizigo yao wapitishie na wa waifate huko ambako hamna corona...unazuia wa huku kuingia huko wakati na wewe watu wako wanakuja hukuhuku kwenye corona sasa hapo si workdone 0 tu....hio ingekua na maana kama na madereva wa Rwanda wangekua hawaji huku mizigo toka Tanzania inaishia boda na wao wanaichukua boda kuelekea kwao baaaas
 
Mpaka na Uganda walitibuana wakafunga kabla hata ya Corona sasa akijifaragua na huku tunafunga unalazimika kupitia Burundi.

Kama ni hofu ya Corona hata madereva wake kuendelea kuja Tz ni tishio kwa nchi yake so bora mpaka ufungwe halafu tuone Nani atapoteza.
 
corona yenyewe itafanya natural selection,kama ilivyofanya kwa US baada ya china,hawaamui wahanga bali yenyewe,ni corona ndio itamchagua bwana wake.

mpaka sasa visa rwanda ni 261.unaweza ukaona ni jinsi gani corona ndio inaongea haipangiwi.mwisho watafunda mipaka yote visa vinazidi tu,halafu itabidi waseme upepo unaipeperusha kuelekea kwao kutokea bahari ya hindi[emoji16][emoji16].

Sent using Jamii Forums mobile app

Hao wamepima watu zaidi ya 30,000 so far na visa vyao ni hivyo 261,hebu tuwekee nasi tumepima watu wangapi na matokeo yake yakoje.
 
Hao wamepima watu zaidi ya 30,000 so far na visa vyao ni hivyo 261,hebu tuwekee nasi tumepima watu wangapi na matokeo yake yakoje.
kwa ratio hiyo ni kama useme kwa tz kwa kila watu 6,4 wana corona,good.

wacha tuamini hivi mkuu,unashauri tufanyaje,tununue mashine za kupumulia au tuchimbe makaburi???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bwana dereva, Wanyarwanda hawana kosa lolote hapa. Kuna visa vingi sana vya madereva wetu vya corona huko Uganda, Malawi na Rwanda. Malawi mpaka sasa, kati ya wagonjwa 41 wa corna, 13 ni maderva kutoka Tanzania. Sasa mnataka nchi zote ziwe kama ya kwenu. Kama ndio mawazo yenu haya, kumbe huyu Rais wenu pia alitakiwa kuwa dereva.

Mnafikiri nyie ndio mna bandari tu? Ngoja waende Mombasa na Beira muone. Yaani nchi kuchukuwa hatua sitahiki za kujilinda, nyie inawakera. Mlitaka iwe kama Tanzania, siyo? watu waanze kuzika usiku Rwanda, Uganda, Malawi.... Siyo sahihi kabisa.

nenda kawaambie waende haraka,wakienda beira tutafanya nao biashara vizuri kabisa barabarani[emoji23].

kama case ni corona kwa madereva,watwambie madereva wao wakija huku kwenye corona watafanyaje wasiipeleke huko kwao,haya mambo hamtakiwi mfikiri kama mko ndotoni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uamuzi Wa Rwanda uko sahihi.Nchi lazima ilinde watu wake kwa nguvu zote
usahihi uko wapi iwapo dereva mwenye corona kaendesha gari mpaka Rwanda na kufika mapakani ashushwe na dereva wa Mnyawanda aingie kwnye gari lile lile aliendeshe na asiambukizwe na ubaya wanayarejesha baadhi ya vitu havimo poli kama kuna maambukizi tanzania kwanini madereva wao wanaoingia na kutoka huku aao wasifanyiwe treatment ya kukomea mpakani pia kama si njia ya kutengeneza ajira kupitia mgongo wa cororna nimemsikiliza mkuu wa wilaya kupitia DW kuwa alijaribu kuwasiliana na upande wa Rwanda wakashindwa kuelewana hivyo ameomba mamlaka za juu ziingilie
 
Bwana dereva, Wanyarwanda hawana kosa lolote hapa. Kuna visa vingi sana vya madereva wetu vya corona huko Uganda, Malawi na Rwanda. Malawi mpaka sasa, kati ya wagonjwa 41 wa corna, 13 ni maderva kutoka Tanzania. Sasa mnataka nchi zote ziwe kama ya kwenu. Kama ndio mawazo yenu haya, kumbe huyu Rais wenu pia alitakiwa kuwa dereva.

Mnafikiri nyie ndio mna bandari tu? Ngoja waende Mombasa na Beira muone. Yaani nchi kuchukuwa hatua sitahiki za kujilinda, nyie inawakera. Mlitaka iwe kama Tanzania, siyo? watu waanze kuzika usiku Rwanda, Uganda, Malawi.... Siyo sahihi kabisa.
Swali linabaki palepale ni kwa nini madereva wao waingie nchi yenye corona? Inamaana na wao hawajali afya zao?
 
Bwana dereva, Wanyarwanda hawana kosa lolote hapa. Kuna visa vingi sana vya madereva wetu vya corona huko Uganda, Malawi na Rwanda. Malawi mpaka sasa, kati ya wagonjwa 41 wa corna, 13 ni maderva kutoka Tanzania. Sasa mnataka nchi zote ziwe kama ya kwenu. Kama ndio mawazo yenu haya, kumbe huyu Rais wenu pia alitakiwa kuwa dereva.

Mnafikiri nyie ndio mna bandari tu? Ngoja waende Mombasa na Beira muone. Yaani nchi kuchukuwa hatua sitahiki za kujilinda, nyie inawakera. Mlitaka iwe kama Tanzania, siyo? watu waanze kuzika usiku Rwanda, Uganda, Malawi.... Siyo sahihi kabisa.

Pamoja na kuwa Tanzania imezisadia sana nchi jirani kwa hali na mali, lakn hizo nchi zimekuwa zikinyanyasa raia wetu, na pia huwa hawatuongelei zuri kwa lolote. Hivyo, kusema nusu ya cases zao ni maderva wa Tanzania siyo jambo la kushngaza.

Kosa lao Rwanda ambao wanajiona wako salama zaidi, ni kunawa mikono kisha kushika matope kwa kuja Tz.

Hawana Corona, lakn wanataka madereva wao walio salama, waje kujiambukiza Tanzania kuliko chafuka. Kwani hao maderva wao wakija Tanzania hawato ambukizwa Corona na kisha kwenda kuusambaza kwao?

kama jibu ni ndiyo, kuna tofauti gani na dereva aliyetoka tz na lory na kwenda kwao?
Kwahiyo, chako ni cha kwako ila chetu huku pia unataka?

Mm sio dereva, ila tumechoka kuona raia wetu wakinyanyaswa kwny nchi za kijinga, wakt raia wao wakija hapa nchini tunaishi nao kama ndgu bila manyanyaso.
 
Kagame ana akili.

Namuunga mkono sana kwenye hili
Yaani mimi nisacrifice kuthibiti Korona hadi kufikia kuwapunguzia watumishi mishahara halafu mijitu ya nchi nyingine ije iharibu sacrifice yoote eti tu. kwa sababu raisi wao anatafuta shortcut ya tatizo

Kagame tuko pamoja, uko sahihi mara mia na nakushauri ili kulinda Afya za Wanyarwanda pitisha mizigo Mombasa mpaka ujiridhishe kuwa Tanzania ni salama.

Endeleeni kujilinda sana ili sisi watanzania tukishakufa kwa korona sababu ya uzembe wa serikali yetu nyie mje mkalie na muishi katika ardhi hii maana nyie ni waafrika wenzetu. Bora nyie waafrika wenzetu mje muirithi nchi hii kuliko Wachina na Wazungu
Halafu wewe ni mjinga tu hujitambui

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa ratio hiyo ni kama useme kwa tz kwa kila watu 6,4 wana corona,good.

wacha tuamini hivi mkuu,unashauri tufanyaje,tununue mashine za kupumulia au tuchimbe makaburi???

Sent using Jamii Forums mobile app
Usinunue mashine wala kuchimba kaburi.
Nawa mikono kwa maji safi na tiririka hata ilibidi kunawa mara Mia au Mia mbili kwa siku fanya hivyo.
Tumia vitakasa mikono mara kwa mara kila unapogusa mahali unapopatilia shaka.
Vaa barakoa kila mara unapotoka nyumbani na usikubali kukaribiana na mtu asiyevaa barakoa.
Zingatia umbali kati yako na jirani yako.
Epuka misongamano.
Baki nyumbani kama huna sababu ya maana ya kutoka.
Fanya mazoezi ya mwili mara kwa mara na epuka kuwa mtu wa kukaa kwenye kiti kwa muda mrefu bila kutembea tembea.
Hakikisha kabla hujalala unakunywa walau glasi moja ya maji vuguvugu.
Corona ipo, jilinde wewe na familia yako na usikubali kusikiliza taarifa zilizojikita kwenye upotoshaji.
Na mwisho kuwa na Corona si kuwa ni lazima ufe, watu wanapata na wanapona kwa nini isiwe wewe?
 
Back
Top Bottom