Bendera mpya ya Syria yapandishwa Leo katika ubalozi wa nchi hiyo Mjini Moscow Urusi

Kwenye diplomasia ubalozi unachukuliwa ni territory ya nchi husika sio ile host state. Kwa hivyo waliopandisha bendera ni wa Syria sio urusi.
Ila kuipandisha ni lazima kwanza serikali ya nchi ambako ubalozi upo itambue serikali inayo tumia bendera hiyo.
 

Wewe ndio hujaelewa. Kidiplomasia pale ni Syria. Nikupe mfano Kipindi cha mauaji ya kimbari pale Rwanda, wale interahanwe walishindwa kuingia kwenye ubalozi wa Tanzania na kuwaua watutsi au watanzania waliokuwa wamejificha mle. Kwa sababu kuvamia mle ingekuwa ni sawa na kuvamia territory ya Tanzania. Kasome kesi ya Kimataifa ya the asylum case Peru v Colombia.
 
Hamna cha chess wala nini Pro NATO mmepigwa chenga za maudhi na DUBU,ngoja mtaona baadae kwamba chui kavishwa ngozi ya kondoo kwanza

Duh! Juzi hapa mlikuwa mnadai Assad hatoki madarakani. Tena Russia alipowashambulia waasi pale Alepo makadai ameingia mzigoni. Leo mmekimbilia kwa Pro NATO kupigwa chenga.
 
Mkifanya hivyo mtakuwa mmetumia hoja ya nguvu badala ya nguvu ya hoja na kuthibitisha kuwa hamna mantiki wala ukweli wa hoja.
 
Hakuna anayepinga Hilo nakubaliana nae kabisa,

Kitendo Cha kusema ubalozi tayari umemaanisha hicho ulichosema au neno ubalozi katika definition yake na hicho Unachosema

Tunapinga jamaa aliposema kuwa huo ubalozi wa Syria haupo urusi
 
Hiki ndicho alichokiandika jamaa kupinga alichokiandika mleta mada, Sasa hii comment halafu linganisha na alichokiandika mleta mada πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡



Hilo eneo ilipopandishwa bendera SIO Russia bali ni Syria. Hivyo Russia HAWEZI kwa namna yoyote kuwazuia Wasyria kufanya chochote kwenye ardhi yao ili mradi tu hawavunji makubaliano ya "The Vienna Convention".
 
Una elimu ndogo juu ya dipromasia huwezi kupandisha bendera kwenye nchi fulani bila serikali ya nchi hiyo kuitambua serikali yenye bendera hiyo bendera.
Na ndio maana ili ubalozi fulani uwe kwenye nchi fulani ni lazima hiyo nchi iwe imeridhia muanzishe mahusiano ya kidipromasia na ana uwezo wa kuamuwa huo ubalozi uondolewe kwenye nchi yake.
 
Mkifanya hivyo mtakuwa mmetumia hoja ya nguvu badala ya nguvu ya hoja na kuthibitisha kuwa hamna mantiki wala ukweli wa hoja.
Yaani hiyo mantiki utajua wewe ila naandaa mpango tukikukamata ni misumari tuu..
Haiwezekani unasumbua wenzako hiviπŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
 
Hahaa. Kwa nini unaandika hivyo mkuu?
Mwenzako anasema ishu ya mantiki.. wee unasema ndo ukweli...
Akisema akubali ni ukweli. Wewe unasema ukweli wa mantiki .

Unakua unamuacha mwenzako njia panda that why nasema kuna siku tutakushika tukupige kwanza πŸ˜„
 
Mwenzako anasema ishu ya mantiki.. wee unasema ndo ukweli...
Akisema akubali ni ukweli. Wewe unasema ukweli wa mantiki .

Unakua unamuacha mwenzako njia panda that why nasema kuna siku tutakushika tukupige kwanza πŸ˜„
Hata ukinipiga kunipiga kwako hakubadili mantiki ya ukweli πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…