Benjamin Mkapa: Natamani kuwe na Tume Huru ya Uchaguzi, Wapinzani wahusishwe kwenye kupiga na kuhesabu kura na kutangazwa mshindi

Daah ila taratiibu yetu umekuwa zaidi ya taratiiiibuuuu...
Kuna nchi tulianza nazo pamoja... Nyingine tukazipa support sisi ili waanze... Angalia walipo... Sisi bado tunaangaika na mabadiliko ya majina ya watu ndani ya chama-kongwe!
Daah... Ukifikiria sana unaweza kupata stroke!
Tutafika tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama nakosea Mungu anisamehe. Nachoamini huyu Mkapa ndio alimpora Maalim Seif urais wa Zanzibar.

Pili huyu ndio mwasisi wa ubavu ubavu na ubabe inakuwaje leo katoka madarakani na anaonekana kachoka ndio anatubu.

Kwanini asiwambie aliowaweka madarakani watende haki? Kwanini alazimishe kupendwa?

=====

Dar es Salaam. Rais mstaafu, Benjamin Mkapa amesema kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi ni njia mojawapo ya kuondoa manung’uniko ya vyama vya siasa na kuimarisha demokrasia barani Afrika.

Mkapa, rais wa kwanza wa Tanzania kuchaguliwa katika mfumo wa vyama vingi, ameandika hayo katika kitabu chake cha “My Life, My Purpose (Maisha Yangu, Kusudi Langu)” ambacho kinazungumzia matukio na maamuzi aliyofanya katika utawala wake wa kuanzia mwaka 1995 hadi 2005, akijutia na kukubali kubeba lawama zote kwa baadhi ya matukio, huku akieleza somo alilopata.

Mkapa amesema ili kuwa na usawa katika mfumo wa vyama vingi nchini, ni muhimu kuwa na chombo huru kilichojumuisha vyama vyote.

“Kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi itakayokubalika na vyama vyote vya siasa ndio chachu ya kulea na kukuza demokrasia nchini,” anasema Mkapa, ambaye anasema alipata funzo kubwa la umuhimu wa kushirikiana na vyama vya siasa baada ya mauaji ya wafuasi 22 wa CUF yaliyofanywa na polisi kisiwani Pemba mwaka 2001.

Mkapa anatahadharisha kuwa muundo wa tume umekuwa miongoni mwa masuala yanayopigiwa kelele na kupata upinzani mkubwa kutokana na upatikanaji wa viongozi wake.

Anashauri kuwa mamlaka ya nchi inaweza kubaki na mamlaka ya kuteua mwenyekiti wa tume ingawa lazima vyama vya upinzani vishirikishwe kwa uwazi katika suala zima la kuhesabu kura na kutangaza matokeo.

“Hatua hii itasaidia kupunguza malalamiko na pia vyama vya upinzani vitajenga imani na tume ya uchaguzi,” alieleza Mkapa, ambaye aliwahi kusuluhisha migogoro ya kisiasa katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Kenya, Sudan Kusini na Burundi.

Mkapa anasema kumekuwa na malalamiko mengi ya vyama vya siasa vikidai kutotendewa haki na tume na kilio hicho ni katika nchi nyingi za Afrika.

Ameonya kuwa malalamiko hayo ya kutotendewa haki kwenye uchaguzi ndio yamekuwa kichocheo cha kuzuka kwa machafuko katika nchi nyingi.

Maoni ya Mkapa ni mwendelezo wa kilio cha muda mrefu cha vyama vya upinzani nchini.

Vyama hivyo vinasema mwenyekiti wa tume huteuliwa na Rais, ambaye pia anaweza kubadilisha wakurugenzi wa chombo hicho.

Pia wasimamizi wa uchaguzi wilayani ni wakurugenzi wa wilaya, ambao pia ni wateule na katika kesi iliyofunguliwa na wanaharakati na vyama vya siasa, Mahakama Kuu ilibatilisha mamlaka ya wakurugenzi hao katika uchaguzi baada ya kuridhika kuwa zaidi ya sabini walikuwa ni makada wa CCM.

Hata hivyo, Serikali ilikata rufaa na kushinda.

Mapendekezo ya kuundwa kwa tume ya huru ya uchaguzi yamewahi kupendekezwa na Tume ya Jaji Francis Nyalali mwaka 1991, Tume aliyoiunda Mkapa ya Jaji ya Robert Kisanga mwaka 1998 na Tume ya Mabadiliko ya Katiba mwaka 2012 ambazo zote zilikusanya maoni ya wananchi.

Kwa sasa kuna sintofahamu nchini juu ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliopangwa kufanyika Novemba 24, huku vyama saba vikitangaza kujitoa kupinga uendeshaji wa uchaguzi huo.

Mkapa, ambaye amezungumzia demokrasia kwa ujumla barani Afrika, anapendekeza pia vyama vya siasa kupewa nafasi ya kueneza sera zao na kuitisha mikutano ya hadhara kwa uhuru.

Kuhusu kipindi chake, anasema hakukuwa na malalamiko dhidi ya tume kwa kuwa iliundwa na majaji walioheshimika katika jamii, lakini akasema vyama havikuwa vinaridhishwa na suala la kuhesabu na kutangaza matokeo na ndio maana wakaruhusu wawakilishi wa vyama tofauti kwenye vituo vya kupigia kura.

Uhuru wa mikusanyiko

Mkapa pia anasema katika kitabu chake kuwa angependa kuona vyama vya siasa vikipewa nafasi ya kufanya shughuli zao kwa uhuru.

“Ninapenda kuona vyama vyote vya siasa vikipewa fursa sawa kuhamasisha wanachama, kufanya mikutano ya hadhara na kutangaza manifesto (ilani) zao,” anasema Mkapa.

Anasema tatizo ambalo analiona kwa sasa ni chama tawala kuendesha mambo kama vile kipo katika mfumo wa chama kimoja.

“Tatizo ninaloliona ni kuwa tulipoingia katika mfumo wa vyama vingi tuliiga demokrasia ya nchi za Magharibi ya mshindi kunyakua kila kitu na kuwatenga wengine katika masuala ya utawala,” anasema Mkapa.

“Nadhani si jambo zuri na hasa likija suala zima la kuimarisha umoja wa kitaifa.”

Pia Mkapa, ambaye hakuwa na urafiki mzuri na vyombo vya habari nchini, anashauri vyombo vya habari vya serikali kutoa nafasi kwa habari za vyama vya upinzani.

“Kumekuwa na malalamiko mengi ya chama tawala ya kubebwa kutokana na kutumia nyenzo za Serikali kufanya shughuli zao tofauti na vyama vya upinzani. Ninashauri uwepo kwa usawa sasa kwa vyama vyote katika nchi,” anasema Mkapa.

Mkapa anasema maridhiano ndio njia pekee itakayosaidia kumaliza mivutano ya kisiasa, kukuza demokrasia na kuimarisha umoja wa kitaifa.

Chanzo: Mwananchi
Jamani BWM ameshafanya kazi yake na yeye ndiye aliyemlea na kumfikisha hapo. Sasa kamchoka. Amesema mpira kwenye penalty spot. Ni juu ya Watanzania kama CCM hawataki. Kimsingi BWM hamtaki Jiwe
 
Acha upunguani. Mkapa hana lolote. Kwanini hakuruhusu tume huru alipokuwa na mamlaka. Atulize tako kwenye sofa ale supu ya mafao aache uropokaji. Tume tutaipigania sisi makapuku hata ikibidi tutatiana vilema au kuiangamiza nchi alimradi uhuru na demokrasia vipatikane.

Hatutaki demokrasia ya kupewa kama fadhila za watawala. Demokrasia yetu ni ile tutakayoamua wenyewe baada ya kutiana majeraha na kutoana ngeu. Siyo hii ya kuamrishwa na mjinga mmoja anayejiita jiwe kama mmasai anayechunga mbuzi zake.

Hata Ghadafi alijitia upofu akajiona anamiliki kondoo, ila ilipofika siku ya kufika walimwokota kwenye kalvati kama kenge.
 
Hawa watu akili zao huwa sizielewi kabisa.Yaani wakiwa madarakani wanakuwa vipofu na viziwi kabisa.Yeye si alikuwa Rais,na alichokuwa nacho wakati ule kama tume ya uchaguzi alikiita tume huru ya uchaguzi,which was obviously not.Hivi watumishi wa serikali wataundaje tume huru jamani,let us be serious.Hawa si lazima watetee kitumbua chao?How can they logically be against their master.Mkapa ingekuwa busara akanyamaza,hana moral authority ya ku-demand tume huru,ingawa kweli tunaihitaji.

Let me very clear about this,hakuna uchaguzi huru na haki na uhuru wa kuchaguliwa, kama hakuna tume huru ya uchaguzi,huu ndio ukweli.Frankly, namshangaa sana mtu anayetetea tume tuliyo-nayo sasa kwamba ni huru.

Nampenda sana Magufuli,lakini nataka ionekana kwamba kachaguliwe kwa haki,sio kwa mizengwe mizengwe,hapo ndipo nitakapo kuwa na ujasiri wa kusema Rais wangu wananchi wanampenda.Kwani tunacho ogopa ni nini,kama kweli wananchi wanampenda?
 
Mmm kwani wakati anapiga mabomu pemba hakubakiza mengine huko ghalani
 
Mkapa alikuwa nani, na sasa ni nani? Tuanzie hapo.
Mkapa ni rais mstaafu wa Serikali ya Mwuungano wa Jamhuri ya Mwuungano wa Tanzania, na in kada wa CCM.

Leo amekuwa muumini wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa! I would not believe him. Ana ajenda iliyofichika.

Amekemea yanayoendelea nchini?Hayaoni? Yeye na Disciple wake wanashea common interest. Tuseme anataka kumkana ili kuepuka kikombe cha nyumba za serikali na ubinafsishaji wa viwanda vya Nyerere?
 
Mnafiki tu huyu hana kutubu chochote. Kama yuko serious basi aanzishe petition yeye awe wa mwanzo kusaini. Nafasi aliyonayo anao ushawishi mkubwa tu wa kulifanya hilo likatimia. Yeye si ndio aliyechafua mchakato ndani ya CCM na kuwaambia watu asiyetaka kupiga kura atoke, keshasahau leo? Aache kumfanyia Mungu usanii asubiri tu kifo akaonane uso na macho na asiyechukuwa hongo huko!
 
Hawa watu akili zao huwa sizielewi kabisa.Yaani wakiwa madarakani wanakuwa vipofu na viziwi kabisa.Yeye si alikuwa Rais,na alichokuwa nacho wakati ule kama tume ya uchaguzi alikiita tume huru ya uchaguzi,which was obviously not.Hivi watumishi wa serikali wataundaje tume huru jamani,let us be serious.Hawa si lazima watetee kitumbua chao?How can they logically be against their master.Mkapa ingekuwa busara akanyamaza,hana moral authority ya ku-demand tume huru,ingawa kweli tunaihitaji.

Let me very clear about this,hakuna uchaguzi huru na haki na uhuru wa kuchaguliwa, kama hakuna tume huru ya uchaguzi,huu ndio ukweli.Frankly, namshangaa sana mtu anayetetea tume tuliyo-nayo sasa kwamba ni huru.

Nampenda sana Magufuli,lakini nataka ionekana kwamba kachaguliwe kwa haki,sio kwa mizengwe mizengwe,hapo ndipo nitakapo kuwa na ujasiri wa kusema Rais wangu wananchi wanampenda.Kwani tunacho ogopa ni nini,kama kweli wananchi wanampenda?
Kwanza ujiulize mtu anayeogopa kuwaachia wananchi wajichagulie mjumbe wa mtaa au mwenyekiti wa kijiji atakuachia eti uchague diwani, mbunge au rais?

Kwa Magufuli sahau mambo ya uchaguzi. Ikiwezekana yeye atapita bila kupingwa na asilia 90 ya wabunge na madiwani watapitishwa kwa lazima.

Magufuli hata umpende yeye hapendeki. Ana mawazo ya kimaskini na hofu kubwa ya kuondolewa endapo ataruhusu uchaguzi huru.
 
Kama nakosea Mungu anisamehe. Nachoamini huyu Mkapa ndio alimpora Maalim Seif urais wa Zanzibar.

Pili huyu ndio mwasisi wa ubavu ubavu na ubabe inakuwaje leo katoka madarakani na anaonekana kachoka ndio anatubu.

Kwanini asiwambie aliowaweka madarakani watende haki? Kwanini alazimishe kupendwa?

=====

Dar es Salaam. Rais mstaafu, Benjamin Mkapa amesema kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi ni njia mojawapo ya kuondoa manung’uniko ya vyama vya siasa na kuimarisha demokrasia barani Afrika.

Mkapa, rais wa kwanza wa Tanzania kuchaguliwa katika mfumo wa vyama vingi, ameandika hayo katika kitabu chake cha “My Life, My Purpose (Maisha Yangu, Kusudi Langu)” ambacho kinazungumzia matukio na maamuzi aliyofanya katika utawala wake wa kuanzia mwaka 1995 hadi 2005, akijutia na kukubali kubeba lawama zote kwa baadhi ya matukio, huku akieleza somo alilopata.

Mkapa amesema ili kuwa na usawa katika mfumo wa vyama vingi nchini, ni muhimu kuwa na chombo huru kilichojumuisha vyama vyote.

“Kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi itakayokubalika na vyama vyote vya siasa ndio chachu ya kulea na kukuza demokrasia nchini,” anasema Mkapa, ambaye anasema alipata funzo kubwa la umuhimu wa kushirikiana na vyama vya siasa baada ya mauaji ya wafuasi 22 wa CUF yaliyofanywa na polisi kisiwani Pemba mwaka 2001.

Mkapa anatahadharisha kuwa muundo wa tume umekuwa miongoni mwa masuala yanayopigiwa kelele na kupata upinzani mkubwa kutokana na upatikanaji wa viongozi wake.

Anashauri kuwa mamlaka ya nchi inaweza kubaki na mamlaka ya kuteua mwenyekiti wa tume ingawa lazima vyama vya upinzani vishirikishwe kwa uwazi katika suala zima la kuhesabu kura na kutangaza matokeo.

“Hatua hii itasaidia kupunguza malalamiko na pia vyama vya upinzani vitajenga imani na tume ya uchaguzi,” alieleza Mkapa, ambaye aliwahi kusuluhisha migogoro ya kisiasa katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Kenya, Sudan Kusini na Burundi.

Mkapa anasema kumekuwa na malalamiko mengi ya vyama vya siasa vikidai kutotendewa haki na tume na kilio hicho ni katika nchi nyingi za Afrika.

Ameonya kuwa malalamiko hayo ya kutotendewa haki kwenye uchaguzi ndio yamekuwa kichocheo cha kuzuka kwa machafuko katika nchi nyingi.

Maoni ya Mkapa ni mwendelezo wa kilio cha muda mrefu cha vyama vya upinzani nchini.

Vyama hivyo vinasema mwenyekiti wa tume huteuliwa na Rais, ambaye pia anaweza kubadilisha wakurugenzi wa chombo hicho.

Pia wasimamizi wa uchaguzi wilayani ni wakurugenzi wa wilaya, ambao pia ni wateule na katika kesi iliyofunguliwa na wanaharakati na vyama vya siasa, Mahakama Kuu ilibatilisha mamlaka ya wakurugenzi hao katika uchaguzi baada ya kuridhika kuwa zaidi ya sabini walikuwa ni makada wa CCM.

Hata hivyo, Serikali ilikata rufaa na kushinda.

Mapendekezo ya kuundwa kwa tume ya huru ya uchaguzi yamewahi kupendekezwa na Tume ya Jaji Francis Nyalali mwaka 1991, Tume aliyoiunda Mkapa ya Jaji ya Robert Kisanga mwaka 1998 na Tume ya Mabadiliko ya Katiba mwaka 2012 ambazo zote zilikusanya maoni ya wananchi.

Kwa sasa kuna sintofahamu nchini juu ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliopangwa kufanyika Novemba 24, huku vyama saba vikitangaza kujitoa kupinga uendeshaji wa uchaguzi huo.

Mkapa, ambaye amezungumzia demokrasia kwa ujumla barani Afrika, anapendekeza pia vyama vya siasa kupewa nafasi ya kueneza sera zao na kuitisha mikutano ya hadhara kwa uhuru.

Kuhusu kipindi chake, anasema hakukuwa na malalamiko dhidi ya tume kwa kuwa iliundwa na majaji walioheshimika katika jamii, lakini akasema vyama havikuwa vinaridhishwa na suala la kuhesabu na kutangaza matokeo na ndio maana wakaruhusu wawakilishi wa vyama tofauti kwenye vituo vya kupigia kura.

Uhuru wa mikusanyiko

Mkapa pia anasema katika kitabu chake kuwa angependa kuona vyama vya siasa vikipewa nafasi ya kufanya shughuli zao kwa uhuru.

“Ninapenda kuona vyama vyote vya siasa vikipewa fursa sawa kuhamasisha wanachama, kufanya mikutano ya hadhara na kutangaza manifesto (ilani) zao,” anasema Mkapa.

Anasema tatizo ambalo analiona kwa sasa ni chama tawala kuendesha mambo kama vile kipo katika mfumo wa chama kimoja.

“Tatizo ninaloliona ni kuwa tulipoingia katika mfumo wa vyama vingi tuliiga demokrasia ya nchi za Magharibi ya mshindi kunyakua kila kitu na kuwatenga wengine katika masuala ya utawala,” anasema Mkapa.

“Nadhani si jambo zuri na hasa likija suala zima la kuimarisha umoja wa kitaifa.”

Pia Mkapa, ambaye hakuwa na urafiki mzuri na vyombo vya habari nchini, anashauri vyombo vya habari vya serikali kutoa nafasi kwa habari za vyama vya upinzani.

“Kumekuwa na malalamiko mengi ya chama tawala ya kubebwa kutokana na kutumia nyenzo za Serikali kufanya shughuli zao tofauti na vyama vya upinzani. Ninashauri uwepo kwa usawa sasa kwa vyama vyote katika nchi,” anasema Mkapa.

Mkapa anasema maridhiano ndio njia pekee itakayosaidia kumaliza mivutano ya kisiasa, kukuza demokrasia na kuimarisha umoja wa kitaifa.

Chanzo: Mwananchi
Viongozi wote waliopo sasa, hata wale wa Tume wanasema hii tume ni Huru. Hii inasigana na anachokinena Mzee Mkapa
 
Acha upunguani. Mkapa hana lolote. Kwanini hakuruhusu tume huru alipokuwa na mamlaka. Atulize tako kwenye sofa ale supu ya mafao aache uropokaji. Tume tutaipigania sisi makapuku hata ikibidi tutatiana vilema au kuiangamiza nchi alimradi uhuru na demokrasia vipatikane.

Hatutaki demokrasia ya kupewa kama fadhila za watawala. Demokrasia yetu ni ile tutakayoamua wenyewe baada ya kutiana majeraha na kutoana ngeu. Siyo hii ya kuamrishwa na mjinga mmoja anayejiita jiwe kama mmasai anayechunga mbuzi zake.

Hata Ghadafi alijitia upofu akajiona anamiliki kondoo, ila ilipofika siku ya kufika walimwokota kwenye kalvati kama kenge.
Umeniita punguani bila sababu japo fikra zako na zangu zina and outcome moja. Tofauti ni approach
 
Pole sana. Sijakuita punguani. Nimekushauri usiingie kingi kirahisi kwa hoja ya huyu Mzee. Kwenye demokrasia huyu ni zero kabisa.
 
Umeenda bila kuona tume huru ya uchaguzi bila shaka viongozi walio baki watafanya kama ulivyo tamani iwe.
 
Back
Top Bottom