Benjamin Netanyahu: Ukitupiga tunakupiga, hakuna sehemu ndani ya Iran ambayo hatuwezi kufika

Benjamin Netanyahu: Ukitupiga tunakupiga, hakuna sehemu ndani ya Iran ambayo hatuwezi kufika

USSR

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Posts
10,904
Reaction score
26,184
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameionya dunia dhidi ya uchokozi, ugaidi na chuki ya kigaidi ya irani kwenye mkutano wa UNGA unaondelea huko New York.

Bwana Netanyahu anasema Iran haipaswi kuwa na nyuklia kamwe kwa kuwa itatumia kuwauwa waarabu ambao sio mashia kama wao na , wayahudi na wakristo duniani kwa kuwa ndio mipango yake .

Amesema ukitupiga tunakupiga hakuna sehemu ndani ya Iran ambayo hatuwezi kufika kwa kuwa irani ndio ilichora shambulio la October 7 liliuwa waisraeli na kuwashikilia kama mateka .

----------

Neta.jpg

Netanyahu amesema Umoja wa Mataifa lazima "urejeshe" vikwazo dhidi ya Iran na "ni lazima sote tufanye kila tuwezalo kuhakikisha Iran haipati silaha za nyuklia".

Akihutumia Mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa, Waziri huyo mkuu wa Israel amesema amekuwa akiionya dunia dhidi ya mpango wa nyuklia wa Iran, ambao anasema "imeuchelewesha" kwa takriban muongo mmoja lakini hajausimamisha.

"Kwa ajili ya amani na usalama wa dunia nzima, hatupaswi kuruhusu hilo kutokea," anasema, akimaanisha Iran kupata silaha za nyuklia.

"Nina ujumbe kwa wadhalimu wa Tehran," anaongeza. "Ukitupiga, tutakupiga."

Awali alipoanza hotuba yake Netanyahu alisema kwamba "hakuwa na nia ya kuja" kwenye Baraza Kuu mwaka huu kwani nchi yake iko vitani "inapigania maisha yake".

"Niliamua kuzungumza katika Umoja wa Mataifa baada ya 'uongo' kuhusu Israel," asema

Hata hivyo, uamuzi wake wa kufanya hivyo ulifuatia kile alichokiita "uongo na kashfa" kuhusu nchi yake iliyosemwa na watu wengine waliosimama kwenye jukwaa, anasema.

Anaongeza kuwa anataka kuja na "kuweka rekodi" kwamba Israeli inatafuta amani.

Netanyahu alionyesha ramani huku akijaribu kutofautisha "baraka" ya maendeleo ya Israeli na "laana" ya ushawishi wa Iran katika eneo.

Uchokozi wa Iran utahatarisha kila nchi katika Mashariki ya Kati - na dunia nzima, Netanyahu ameuambia Umoja wa Mataifa.

"Iran inataka kulazimisha itikadi kali zaidi ya Mashariki ya Kati, na inatishia ulimwengu mzima."

Ulimwengu umeituliza Iran, anasema, na kufumbia macho ukandamizaji wa ndani wa Iran na uchokozi wa nje.

Pia, soma: Iran yarusha Makombora takriban 200 kuelekea Israel, Rais Biden aagiza Jeshi la Marekani kuyazuia
 
Bwana Netanyahu anasema Iran haipaswi kuwa na nyuklia kamwe kwa kuwa itatumia kuwauwa waarabu ambao sio mashia kama wao na , wayahudi na wakristo duniani kwa kuwa ndio mipango yake .
Hii ni kweli,
Netanyahu aungwe mkono na kila mpenda amani kwa hili
hakuna sehemu ndani ya Iran ambayo hatuwezi kufika
Hahaha,
Hata shimoni anamoishi Ayatollah watamfikia tu
 
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameionya dunia dhidi ya uchokozi, ugaidi na chuki ya kigaidi ya irani kwenye mkutano wa UNGA unaondelea huko New York.

Bwana Netanyahu anasema Iran haipaswi kuwa na nyuklia kamwe kwa kuwa itatumia kuwauwa waarabu ambao sio mashia kama wao na , wayahudi na wakristo duniani kwa kuwa ndio mipango yake .

Amesema ukitupiga tunakupiga hakuna sehemu ndani ya Iran ambayo hatuwezi kufika kwa kuwa irani ndio ilichora shambulio la October 7 liliuwa waisraeli na kuwashikilia kama mateka .

USSR
Wakawavamie sasa Iran
 
Kina vitu vingine vina chekesha
1.Irani kwa ukubwa ni mara 80 ya nchi ya Israel,Hata Mkoa wa Dodoma ni mkubwa mara 2 kuliko Israel.
2.Population ya Taifa la Irani ni mara 10 zaidi ya la Israel.
3.ukija kwenye capability za uwezo wa kijeshi,Irani anapambana na NATO nzima kwenye nyanja hizo.
Sasa wakienda one to one eti Israel ashinde,itakuwa vichekesho vya mwaka.
 
Back
Top Bottom