TANZIA Benjamin William Mkapa, Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tatu afariki dunia

TANZIA Benjamin William Mkapa, Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tatu afariki dunia

Status
Not open for further replies.
Daaah . . . so sad.
Kwangu mimi nitamkumbuka kama mmoja wa wahariri bora wa habari za kiuchunguzi wakati ule akiwa pamoja na mwandishi mwenzie (Nsa Kaisi ambaye naye ni marehemu) kwenye gazeti la the nationalist (kama sijakosea). Alihariri story moja mpaka Nyerere akaukubali mzigo kwa jinsi ulivyosimama...

Tumepoteza mtu haswa [emoji27]
 
benmkapa.jpg
benmkapa.jpg
benmkapa.jpg
benmkapa.jpg


Kwa niaba ya jamii zote mkoani morogoro hususani sisi walima mpunga wa bonde zima la mto kilombero tunaungana na rais magufuri ktk kipindi hiki kigumu kwa nchi yetu kwa kumpoteza rais ben mkapa. Tunawaomba watanzania na rais wetu kwa pamoja tukubali kuwa ni mapenzi ya mungu na sisi tunabaki wanadamu ambao ifikapo swala la uhai na kifo tunakosa mamlaka ya kuhoji uamuzi wa anayekarimu uhai na kifo.

Tunamkumbuka sana kwa ilani ya 2005 aliyomkabidhi jakaya kikwete rais wa awamu ya nne juu ya daraja la mto kilombero sasa daraja la magufuri, huyu mzee alitembelea bonde hili 2003-4 akajionea ugumu na dhiki zetu mpaka malinyi....alikiri kuna haja ya daraja hapa haraka na pia tufikirie sasa kwenda songea kupitia hapa....tunamshukuru sana kwa yote ...morogoro ilipendwa na mkapa hata kwa uteule ...ni zama hizi nyota ya dr. Ngasongwa ,dr chiduo na wengine kadhaaa ziling'aa sanaaa...ni mkapa aliyewafyeka matajiri kuanzia morogoro mpaka mahenge na kuwapa wananchi wa kawaida nafasi za kuomba kura kwa tiketi ya ccm ,,,celina kombani aliingia kwa mkono wa mkapa 2005...dr. Mzeru aliingia kwa mkono wa mkapa...pale mikumi kuna mvidunda fulani alipenya zama za mkapa alinusurika abasy gulamali tu.

Tunakukumuka hasa tulipoona ccm ikiwa na nguvu sana morogoro tena ,tunashukuru warithi wako nao wametembelea bonde hili na sasa umewaacha wanalikarabati kisiasa na kiuchumi ili baada ya 2020 liwe la kijani CCM wameamua huko majimboni...vijana wameamka wanataka kuja na ccm ya magufuri..vijana wa watoto wa masikini toka malinyi ,ulanga,mlimba...wana CCM wameleta vijana naamini kwa msiba huu na historia ya mzee mkapa , wanalo la kujifunza na kuitikia wito wako....wapokeee waende wakisemee ccm waombe kura wangali vijana timamu.

Kwa kuwapa vijana nafasi hizi naamini mzee wangu ben mkapa atalala kwa amani. Mara zote mzee ben anapenda kuvaa u ccm wake ....tumuombee pamoja , nchi itamalaki. Pole mheshimiwa rais kwa msiba wa somo wangu ben mkapa. Asante kwa maisha yake na utumishi wake, mungu ampe pumziko lenye amani mwamba huyu aliyekiri ubiniadamu wake kwa maanmdishi na kutubia makosa yake ....tutamuombea daima .
 
That is true!! Huwa wakati mwingine sisi waswahili tunakuwa wanafiki; unakuta mtu anakufa akiwa na miaka [emoji817]+ eti ndugu wanalia!! Badala ya kumshukuru Mungu kwa upendeleo wa kumpa umri huo, tena inatakiwa ifanyike sherehe kubwa watu wale wafurahi.

Biblia inasema umri wa mtu ni miaka 70 na akiwa na nguvu sana ni miaka 80. Ukivuka hapo mimi huita bonus au miaka ya upendeleo. Mkapa alikuwa ameshavuka 80 hongera zake na waliovuka tayari.

Sisi tuliobaki tutafika huko? Mungu tusaidie. Sasa kwenye historia ndio huwa Kimbembe!
Ameishi miaka 10 ya upendeleo
(IBiblia inasema)
 
Kwa vile mkapa ndio baba wa kapitalism Tanzania (yaani raisi aliye anzisha ubepari Tanzania) tungependa kuona kila kitu kitakacho husika kwenye msiba wake kiwe made in Tanzania.
 
Anaandika Derek R. Peterson






Coda
Mkapa did his first degree at Makerere University, where he read English. In 1960 he spent four weeks in Hawaii with a group of Afro-Asian students, studying 'the role of universities in developing societies'.

Here's a report from a Hawaiian newspaper on their visit.

IMG_20200726_073104.png



IMG_20200726_073108.png


Coda II
In 1962 Mkapa--now graduated from Makerere--enrolled in Columbia University.

On his arrival in New York City he caused a panic: the authorities thought he had smallpox, & they put him in isolation for a week.

As it turned out it was chicken pox. Reports below.

IMG_20200726_073558.png


IMG_20200726_073554.png
 
Kwani alikuwa na mchango gani kwa umoja wa nchi hii, mpaka useme kuondoka kwake kunaweza kuwa tatizo la umoja wa nchi hii? Yeye aliamua kuishi kama MwanaCCM, na hajawahi kujali umoja zaidi ya kuhakikisha CCM ndio inakuwa nchi.

Tuache sifa za uongo kwa watu wasiostahili sifa hizo, eti kisa wamefariki.

Ni kweli amefariki kama binadamu wengine, tunamuombea asemehewe kama anastahili. Lakini hakuwa na jipya lolote ambalo kuondoka kwake watanzania wote watalikosa.
Asamehewe nini, kipi alikosea,mbona mwapenda jihesabia haki?
 
Tutakukumbuka daima Mzee Mkapa, Pumzika kwa amani Rais Wetu Mstaafu wa awamu ya III Mh. Benjamin William Mkapa.
IMG-20200728-WA0008.jpg
 
Mwamba kutokana na ushawishi wake na kutokubaliana na nepotism ya kuridhisha uongozi watoto wa viongozi hasahasa la mwinyi Jr kupewa rithaa ya kuwania urais pale Dodoma nahisi kabisa Polonium 210 ilihusika.
 
Umekufa lkn mateso uliowaachia waja wa Mungu kwa kuwaletea hyu mtu, Mungu na azidi kukuongezea adhabu ya kaburi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom