Benki Kuu (BoT) yachukua usimamizi wa Benki ya China kwa kushindwa kulinda vigezo

Benki Kuu (BoT) yachukua usimamizi wa Benki ya China kwa kushindwa kulinda vigezo

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,716
Reaction score
9,051
Benki kuu ya Tanzania leo imechukua usimamizi wa Benki ya kibiashara ya China kwa kushindwa kulinda vigezo vya kuendeleza kuwepo ikiwemo mtaji. Benki kuu kwa mamlaka iliyonayo kwenye sheria ya mabenki na taasisi za fedha imechukua uongozi wa benki hiyo kutoka leo tarehe 19 Novemba 2020 kwa kumteua Neema Koka kuwa meneja kwenye benki hiyo.

Pia kulingana na sheria benki ya China haitafungua ofisi kwa ajili ya biashara za kila siku kwa siku zisizozidi tisini.

E8ED2B6F-8278-48EA-A685-BC7B2523AE39.jpeg
 
Kujenga uchumi imara sio kazi ndogo
 
Kweli hizo benki za kihuni wazifungiage hivyo hivyo.
Kwamaana kuna benki zingine unaenda unakuta hadi karatasi za kuandikia wanakuambia hawana.
Au kama umeme umekatika unakuta wanahesabia hela mikono ukiuliza wanakuambia jenereta haina mafuta na hela ya kununulia mafuta hawana.
 
Kuna kadudu kengine pia kanajulikana kama Yetu bank... siuji mpaka leo kanafanya nini.
... viko kadhaa vya aina hiyo; huwezi kujua ni benki. Kwa mfano kuna kamoja kako pale Manzese, ghorofa la kushoto just before daraja la waenda kwa miguu kama unaelekea Ubungo, kanaitwa Letshego Bank. Jina lake sijui ni muunganiko wa Let-she-go yaani hata halieleweki!
 
Back
Top Bottom