Benki Kuu (BoT) yadai kuna watu wameficha dola

Hata wakati wa kikwete hali ilikuwa hivihivi,,lakininwakati wa mawanza dolla zilikuwa nyingi
 
Mama Samia wanamchezea sana. Kila siku kubadilisha sababu sababu huku uchumi ukiharibika. Nakuona huruma RAIS wangu. Dhamira yake Kwa Taifa ila Hawa aliowapa dhamana akili za Kwenye makaratasi wengi sio wabunifu na wafanya maamuzi
 
Defensive mechanism kwenye management huwa ni upumbavu tu, kiongozi unapaswa kuwa na suluhu na sio kulialia.
 
Sasa kama zimefichwa sisi tufanyeje wakati wao ndio serikali nawanamiliki tools zooote.
Wana mabunduki, vifaru, meli za kivita, majet fighter na majeshi yoote, watoke wakazitafute zilikofichwa.
 
Sisi tunapaswa kuona dola mitaani, sukari, umeme, maji nk na sio excuse na blah blah.

Mama toa kauli Moja kama Amir Jeshi Mkuu.
 
Kama ndo hivyo basi magufuli alikuwa sahihi kuban huu ujinga wa bureau de change.

Huwezi kuwa na ofisi au taasisi ambazo huwezi kudhibiti uendeshaji wao hasa wanapoenda kinyume na taratibu..
Mtanikumbuka 😂🔥
 
Tatizo ni sera.
Wekeni soko huria,kusiwe na masharti kwa muuzaji na mnunuzi.(Kuweka dola benk sio shida,mtu akitaka kutoa dola benki inakuwa na masharti).
Serikali idhibìti mfumuko wa bei,na bei za bidhaa zisipande kiholela.(ili kuwa na imani na kuondoa hofu ya mabadiliko ya thamani ya fedha na bidhaa miongoni mwa wafanyabiashara).
 
Kama unanunua na kuagiza Kila kitu hiyo dola utaiona wapi?

Sukari ambayo tungeweza kuzalisha na kuuza nje na kuingiza hizo dola nayo leo tunaagiza nan kulipa dola kwa wenye akili na uwezo wa kuzitumia.

Umeme ambao tulikuwa na uwezo wa kuuza nje na kuingiza dola nao hatuna.

Yaani tumeshindwa hata kuzalisha cemet ikatosheleza soko la ndani na excess tukapelekaa visiwani huko Comoro, Madagascar, usherisheri nk.

Tumeshindwa hata kuuza mawe na mchanga huko visiwani na uarabuni tukapiga dolali.

Haya madini yetu, dhahabu, tanzanite, almasi nk yanatusaidia nini Sasa.

KIPI TUNAWEZA SASA.?
 
Hizo ndio faida za uchumi wa fremu, frameconomics. Kila kitu kinaagizwa, hakuna kitu kinachozalishwa. Hakuna uzalishaji wa bidhaa au huduma.
Kama nchi haiuzi bidhaa na huduma, je dollar zitatoka wapi?

Frameconomics
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…