Benki Kuu (BoT) yadai kuna watu wameficha dola

(𝐈𝐦𝐞𝐚𝐧𝐝𝐢𝐤𝐰𝐚 𝐍𝐚 𝐒𝐚𝐥𝐨𝐦𝐞 𝐊𝐢𝐭𝐨𝐦𝐚𝐫𝐢)

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imesema nchi haina uhaba wa dola, bali baadhi ya watu wamezihifadhi wakitarajia bei itapanda, ikisisitiza hakutakuwa na ongezeko hilo kutokana na hatua za ndani na nje zinazochukuliwa katika kuimarisha upatikanaji wake.

Imezitaja hatua hizo zinajumuisha uamuzi wa Marekani kulegeza masharti ya riba kwenye masoko yake ya fedha, kupungua kwa bei ya mafuta kwenye soko la dunia na ya nchini na kuendelea kutoa bei elekezi na kufuatilia kwa karibu sekta ya fedha nchini.

Meneja Msaidizi Utafiti wa BoT, Dk. Lusajo Mwankemwa, amebainisha hayo alipotoa mada kuhusu majukumu ya taasisi hiyo benki hiyo wakati wa semina kwa waandishi wa habari, ambao walitaka kujua hatua zinazochukuliwa kuimarisha upatikanaji dola nchini.

"BoT tunajua na tunaona dola zipo ila ni ngumu kukufuata kutaka tuchukue dola nyumbani kwako, mimi (BoT) nitasema dola moja ni kiasi hiki (bei elekezi).

NIPASHE
😂😂😂😂😂
Eti hakutakuwa na ongezeko sijui wanadhani dola ni mahindi au mbaazi za Tanzania? Hahahaha
 
Inawezakanaje MTU afiche pesa zake kisha apate Shida kuitafuta?

Pili, kama BOT inaziona pesa, Watu wanalalamika na yeye kakaa kimya basi tuna Tatizo kubwa sana
 
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imesema nchi haina uhaba wa dola, bali baadhi ya watu wamezihifadhi wakitarajia bei itapanda, ikisisitiza hakutakuwa na ongezeko hilo kutokana na hatua za ndani na nje zinazochukuliwa katika kuimarisha upatikanaji wake.

Imezitaja hatua hizo zinajumuisha uamuzi wa Marekani kulegeza masharti ya riba kwenye masoko yake ya fedha, kupungua kwa bei ya mafuta kwenye soko la dunia na ya nchini na kuendelea kutoa bei elekezi na kufuatilia kwa karibu sekta ya fedha nchini.

Meneja Msaidizi Utafiti wa BoT, Dk. Lusajo Mwankemwa, amebainisha hayo alipotoa mada kuhusu majukumu ya taasisi hiyo benki hiyo wakati wa semina kwa waandishi wa habari, ambao walitaka kujua hatua zinazochukuliwa kuimarisha upatikanaji dola nchini.

"BoT tunajua na tunaona dola zipo ila ni ngumu kukufuata kutaka tuchukue dola nyumbani kwako, mimi (BoT) nitasema dola moja ni kiasi hiki (bei elekezi).

"Siwezi kuja nyumbani kwako wewe uliyezihifadhi nikikwambie lazima kuuza kwa bei hii, BoT jukumu lake ni kutoa mwongozo wa kuhakikisha bidhaa hiyo inapatikanaje," amesema.

Pia soma:
- BoT: Mnaoshikilia Dola mziweke sokoni kwenye mfumo rasmi
Na sukari na umeme pia umefichwa?
 
Serikali inasikitisha Sana. Basi tu hakuna Cha kufanya
 
Back
Top Bottom