Benki Kuu ya Tanzania kuanza kuondoa kwenye mzunguko noti za zamani za shilingi

Benki Kuu ya Tanzania kuanza kuondoa kwenye mzunguko noti za zamani za shilingi

Kidagaa kimemwozea

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
3,680
Reaction score
6,554
Benki Kuu ya Tanzania inatarajia kuanza kuondoa kwenye mzunguko noti za zamani za shilingi ishirini (20), mia mbili (200), mia tano (500), elfu moja (1000), elfu mbili (2000), elfu tano (5000), na elfu kumi (10000) za matoleo ya mwaka 1985 hadi 2003, pamoja na noti ya shilingi mia tano (500) iliyotolewa mwaka 2010. Hii ni kufuatia Tangazo la Serikali Na. 858 la tarehe 11 Oktoba 2024.

Katika taarifa iliyotolewa leo, Oktoba 26, 2024, na Gavana wa Benki Kuu, Emmanuel M. Tutuba, zoezi la ubadilishwaji linatarajiwa kuanza tarehe 06 Januari 2025 hadi tarehe 05 Aprili 2025. Badiliko hili litafanyika kupitia ofisi zote za Benki Kuu na benki za biashara, ambapo wananchi watapewa malipo yenye thamani sawasawa na kiasi kitakachowasilishwa.

Aidha, matumizi ya noti hizo yatafikia ukomo wa kuwa fedha halali za Tanzania kuanzia tarehe 06 Aprili 2025. Baada ya tarehe hiyo, mtu yeyote au taasisi yoyote inayomiliki fedha hizo haitaruhusiwa kuzitumia kufanya malipo popote duniani. Vilevile, benki zote hazitaruhusiwa kulipa wala kupokea amana au maombi ya kubadilisha noti zilizoondolewa kwenye mzunguko.

Kufuatia zoezi hilo, Benki Kuu inatoa rai kwa wananchi wote wenye akiba ya noti hizo za zamani kuzibadilisha au kuziweka amana kwenye benki yoyote ndani ya kipindi kilichotolewa.
FB_IMG_17299561778292358.jpg
 
Zinaletwa noti zenye pocha ya Mama Abdul, Baba Abdul, Mchengelwa, Abdul kwa upande wa mbele na nyuma kumewekwa alama za Msikitini na picha ya Shehe Kipoozeo, Mazinge, Dr. Sulle bila kumsahau Mufti mkuu.

Zile picha zilizotrend mtandaoni za mama abdul akiwekwa kwenye noti na mremba mwekundu zilikuwa za kweli na walizileta makusudi kupima upepo. Zile ndio zinakuja rasmi.
 
Back
Top Bottom