Benki Kuu ya Tanzania kuanza kuondoa kwenye mzunguko noti za zamani za shilingi

Nonsense hivi kuna noti za sh 20 au 500 labda hiyo 10000 na hiyo imebadiridhwa mara ngapi what logic for
 
Wewe umeelewaje? Noti zilizopo zilizo orodheshwa hapo nyingi hazipo kwenye mzunguko tangu kitambo sana na zoezi hili wala halita athiri hizi note zilizopo sasa kwenye mzunguko
1000117360.jpg

Asilimia kubwa zinazo ongelewa ni hizi na zile za zamani sana ambazo baadhi ya watu wanazo tu ndani.
 
Kwani noti za shilingi 20 na 200 zilikuwepo kwenye mzunguko? Mbona hazijaonekana muda mrefu sana? Au sijalielewa tangazo? Aliye elewa anisaidie ufafanuzi tafadhali.
Hizo noti ni zamani sana na hazipo!
 
Benki Kuu ya Tanzania inatarajia kuanza kuondoa kwenye mzunguko noti za zamani za shilingi ishirini (20), mia mbili (200), mia tano (500), elfu moja (1000), elfu mbili (2000), elfu tano (5000), na elfu kumi (10000) za matoleo ya mwaka 1985 hadi 2003, pamoja na noti ya shilingi mia tano (500) iliyotolewa mwaka 2010. Hii ni kufuatia Tangazo la Serikali Na. 858 la tarehe 11 Oktoba 2024.

Katika taarifa iliyotolewa leo, Oktoba 26, 2024, na Gavana wa Benki Kuu, Emmanuel M. Tutuba, zoezi la ubadilishwaji linatarajiwa kuanza tarehe 06 Januari 2025 hadi tarehe 05 Aprili 2025. Badiliko hili litafanyika kupitia ofisi zote za Benki Kuu na benki za biashara, ambapo wananchi watapewa malipo yenye thamani sawasawa na kiasi kitakachowasilishwa.

Aidha, matumizi ya noti hizo yatafikia ukomo wa kuwa fedha halali za Tanzania kuanzia tarehe 06 Aprili 2025. Baada ya tarehe hiyo, mtu yeyote au taasisi yoyote inayomiliki fedha hizo haitaruhusiwa kuzitumia kufanya malipo popote duniani. Vilevile, benki zote hazitaruhusiwa kulipa wala kupokea amana au maombi ya kubadilisha noti zilizoondolewa kwenye mzunguko.

Kufuatia zoezi hilo, Benki Kuu inatoa rai kwa wananchi wote wenye akiba ya noti hizo za zamani kuzibadilisha au kuziweka amana kwenye benki yoyote ndani ya kipindi kilichotolewa.
View attachment 3136008
Vitu vilishaondoka zamani wanakuja kusema sasa kua wataviondoa.

Noti za TZS 20/-, TZS 200/- na TZS 500/- zilishaondoka kitambo tu sijui hata mwaka gani.
 
Sidhani hizo noti wanazotoa ni za muda sana na nyingi zimeshapotea kwenye mzunguko kabisa labda mia tano ya noti kwa mbali ndio unaweza ibahatisha.
Nadhani wanahitimisha rasmi sasa.
Hapa mkuu ndo nimeelewa,
BOT nao wamezingua, ilibidi waweke na hizo picha za noti. Ona sasa inavyoleta ukakasi kwa wananchi.

Kila mtu ameanza kuweka tafsiri yake. Hapa tu ni kwa watu wenye uelewa. Tunaamini hivyo walau kila member amemaliza kidato cha 4.

Sasa kwa wakulima wetu, machinga na hawa bodaboda itakuwaje.
We acha tu mkuu, namna wana JF wanavyoutafsiri huu uzi, inasikitisha sana
 
Kwani noti za shilingi 20 na 200 zilikuwepo kwenye mzunguko? Mbona hazijaonekana muda mrefu sana? Au sijalielewa tangazo? Aliye elewa anisaidie ufafanuzi tafadhali.
WAache watu wapige pesa za operesheni ondoa noti za kale
 
Marais waislam na pesa za Tanzania hawajambo, kila jambo lina mwisho acha inyeshe
 
Naona wanaochimbia hela chini wamefikiwa
Benki Kuu ya Tanzania inatarajia kuanza kuondoa kwenye mzunguko noti za zamani za shilingi ishirini (20), mia mbili (200), mia tano (500), elfu moja (1000), elfu mbili (2000), elfu tano (5000), na elfu kumi (10000) za matoleo ya mwaka 1985 hadi 2003, pamoja na noti ya shilingi mia tano (500) iliyotolewa mwaka 2010. Hii ni kufuatia Tangazo la Serikali Na. 858 la tarehe 11 Oktoba 2024.

Katika taarifa iliyotolewa leo, Oktoba 26, 2024, na Gavana wa Benki Kuu, Emmanuel M. Tutuba, zoezi la ubadilishwaji linatarajiwa kuanza tarehe 06 Januari 2025 hadi tarehe 05 Aprili 2025. Badiliko hili litafanyika kupitia ofisi zote za Benki Kuu na benki za biashara, ambapo wananchi watapewa malipo yenye thamani sawasawa na kiasi kitakachowasilishwa.

Aidha, matumizi ya noti hizo yatafikia ukomo wa kuwa fedha halali za Tanzania kuanzia tarehe 06 Aprili 2025. Baada ya tarehe hiyo, mtu yeyote au taasisi yoyote inayomiliki fedha hizo haitaruhusiwa kuzitumia kufanya malipo popote duniani. Vilevile, benki zote hazitaruhusiwa kulipa wala kupokea amana au maombi ya kubadilisha noti zilizoondolewa kwenye mzunguko.

Kufuatia zoezi hilo, Benki Kuu inatoa rai kwa wananchi wote wenye akiba ya noti hizo za zamani kuzibadilisha au kuziweka amana kwenye benki yoyote ndani ya kipindi kilic
 
Kwani noti za shilingi 20 na 200 zilikuwepo kwenye mzunguko? Mbona hazijaonekana muda mrefu sana? Au sijalielewa tangazo? Aliye elewa anisaidie ufafanuzi tafadhali.
Kama vile kuna mipapa nguva na mijizi inatafutiwa namna ya kuhalalisha mipesa yao ya uwizi iliyo fukiwa chini, kuwekwa kwenye ndoo na uvunguni kuingia kwenye mzungungo halali vile? Afu ukivuta picha miaka yenyewe hii !!

Sijui nimefikiri kupita kiasi?!

Nayeyuka kama kasongo mbona wewo, mombali nanga.............
 
Zinaletwa noti zenye pocha ya Mama Abdul, Baba Abdul, Mchengelwa, Abdul kwa upande wa mbele na nyuma kumewekwa alama za Msikitini na picha ya Shehe Kipoozeo, Mazinge, Dr. Sulle bila kumsahau Mufti mkuu.

Zile picha zilizotrend mtandaoni za mama abdul akiwekwa kwenye noti na mremba mwekundu zilikuwa za kweli na walizileta makusudi kupima upepo. Zile ndio zinakuja rasmi.
Punguza chuki mkuu, hizi ya habari za kubuni haziwezi kumsaidia yoyote.
 
Tuwekee tupicha twa hizo noti zitakazotolewa kwenye mzunguko, ili kama tunazo tujiandae kuzibadilisha.
 
Kama vile kuna mipapa nguva na mijizi inatafutiwa namna ya kuhalalisha mipesa yao ya uwizi iliyo fukiwa chini, kuwekwa kwenye ndoo na uvunguni kuingia kwenye mzungungo halali vile? Afu ukivuta picha miaka yenyewe hii !!

Sijui nimefikiri kupita kiasi?!

Nayeyuka kama kasongo mbona wewo, mombali nanga.............
Duu! Hii ndio inaitwa kufikiria nje ya boksi!
 
Back
Top Bottom