Benki Kuu ya Tanzania kuanza kuondoa kwenye mzunguko noti za zamani za shilingi

Benki Kuu ya Tanzania kuanza kuondoa kwenye mzunguko noti za zamani za shilingi

Hapo kuna usanii tu hawana lolote ,nakumbuka kulikua na na noti version mbili kwenye mzunguka ,Kubwa na ndogo ,Kulikuwa na buku ndogo na buku size kubwa pia kwa noti za elfu 10,5,2 na zilishatoka kwenye mzunguko.

Nimeshangaa wanasema wanaondoa note ya Tsh 20 , 200 na 500 mbona hizo hazitumiki kwa muda mrefu sana?

Hapa kuna issue ya kuwatisha mafisadi walioficha vibunda ndani au kuprint fedha za uchaguzi ili tuwe kama Zimbabwe.
 
Wenye fedha kwenye sandarusi wajiandae kisaikolojia.
1wajiandae kwa lipi? Kuziingiza kwenye mzunguko mbona rahisi mno?
Unanunua gari kwa milioni 300 halafu baada ya muda kidogo noti mpya zikiingia unaenda yard kuwauzia unakula hasara ya milioni zisizo zidi 5 halafu unarudisha hela kwenye sandarusi unakausha. Si lazima iwe gari unaweza fanya hivyo kupitia mambo mengine kama casino au kulangua bidhaa kwa jumla na kuziuza kwa bei ya hasara kidogo utakatishaji upo na utaendelea kuwepo.
Watu wanatunzia fedha zao kwenye madini.
Unaona vidole vya doto magari? Vinatembea na fhahabu muda wowote anaenda kuiuza na kupata hela
 
Kivipi wakati izo noti hazipo kabisa mtaani.
Fafanua vizuri tuelewe wote
Kweli BOT waje na ufafanuzi unaoeleweka kuondoa noti za Tsh 20 ,noti za 200 ,noti za 500 kwani nani anazitumia hizo noti kwasasa? Mbona hazipo muda mrefu sana ,nani anatumia note ya 200 yenye sura ya mwinyi? Nani anatumia noti ya Tsh 20 yenye rangi ya zambarau? nani anatumia noti ya 500 yenye rangi ya kijani? Nani anatumia noti ya tsh 10 ya rangi ya kijani?
 
Kweli BOT waje na ufafanuzi unaoeleweka kuondoa noti za Tsh 20 ,noti za 200 ,noti za 500 kwani nani anazitumia hizo noti kwasasa? Mbona hazipo muda mrefu sana ,nani anatumia note ya 200 yenye sura ya mwinyi? Nani anatumia noti ya Tsh 20 yenye rangi ya zambarau? nani anatumia noti ya 500 yenye rangi ya kijani? Nani anatumia noti ya tsh 10 ya rangi ya kijani?
Apo ndio hata mm najiuliza
 
Kama hakuna msukumo wa kisiasa ni jambo jema sana.. Kinyume chake tumekwisha....
Maana si ajabu tukaletewa zenye sura za wanasiasa
Mkuu hivi karibuni kulivuja picha ya noti ya sh. 10,000 rangi ya kijani yenye picha ya Rais Samia.

Baada ya kuvuja kwa picha hiyo, Bank kuu haraka haraka walikanusha.

Nadhani unachohisi chaweza kuwa na ukweli 100%.
 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BENKI KUU YA TANZANIA

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUONDOA KWENYE MZUNGUKO NOTI ZA ZAMANI ZA SHILINGI YA TANZANIA

Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuufahamisha Umma kuhusu zoezi la kuondoa kwenye mzunguko noti za zamani za shilingi ishirini (20), mia mbili (200), mia tano (500), elfu moja (1000), elfu mbili (2000), elfu tano (5000) na elfu kumi (10000) kwa matoleo ya mwaka 1985 hadi mwaka 2003, na noti ya shilingi mia tano (500) iliyotolewa mwaka 2010 zenye sifa zilizoainishwa kwenye Tangazo la Serikali Na. 858 la tarehe 11 Oktoba 2024.

Zoezi la ubadilishaji litarajiwa kuanza tarehe 06 Januari 2025 hadi tarehe 05 Aprili 2025 kupitia Ofisi zote za Benki Kuu na benki zote za biashara kwa kupatiwa malipo yenye thamani sawasawa na kiasi kitakachoasilishwa. Aidha, matumizi ya
For more: Withdrawal of Old Tanzanian Banknotes from Circulation - AjiraCoach
IMG-20241027-WA0009.jpg
 
Wale wenye mabunda waliyoyaanda kwa Ile shughuli yetu pendwa na kuu ya 2025! Imekula kwao🤣maana kuzibadilisha zote awatoweza.
Wewe umeelewaje? Noti zilizopo zilizo orodheshwa hapo nyingi hazipo kwenye mzunguko tangu kitambo sana na zoezi hili wala halita athiri hizi note zilizopo sasa kwenye mzunguko
 
Back
Top Bottom