Benki ya Amana inahujumiwa

Benki ya Amana inahujumiwa

Yaani nahitaji pesa nikanunue passo ya milioni 8 unaninyima ela unaenda kuninunulia hiyo passo na kunidai milioni 10 alafu unaniambia hakuna riba?? Natakiwa niwe mbumbumbu kwanza ndio niamini huo upuuzi, kitu bila riba nipe milioni kumi nikurudishie milioni kumi kwa muda wa miaka mitano, hiyo ndiyo interest free, out of that ni utapeli kama utapeli mwingine

Ni utapeli kama matapeli wengine,tatizo hawa jamaa wanataka kulazimisha uhafidhina na uprimitivu wa mudi katika ulimwengu wa sasa lazima watafeli tu,kukopesha bila riba inawezekana kwa watu binafs ila taasisi haiwezi survive bila riba zaidi ya unafaiki na kucheza na akili za wajinga wao. Riba ipo palepale.
 
Hii ni benki ya mwanzo nchini kuendesha huduma zake kwa misingi ya sharia za kiislamu. Pia ni muendelezo wa mfumo bora wa kibenki unaofanya kazi nchi nyingi duniani.

Benki hii ilipoanza kazi nchini kulikuwa na maneno kutoka kwa baadhi ya watu lakini hatimae ikaanza shughuli zake na kuonekana kukua kwa kasi. Hata hivyo katika siku za karibu kwa mtazamo wa kimteja nimeona kuna shida zisizotatulika.

Katika pita pita yangu nimekutana na jamaa mwenye taarifa za ndani ambaye amethibitisha kuna hujuma za ndani kwa ndani zinazoendeshwa na wafanyakazi ambao kama wametumwa wafanye kazi hiyo.Kwa upande mwengine kuna benki nyengine ambazo zinakiuka sheria za BOT na kuacha ushirikiano na benki hii tena bila kukemewa.

inajulikana benki yoyote ya kiislamu duniani haiwezi kufilisika kwa njia za kawaida.Hata hivyo panapokuwa na hujuma zinazoendelea ndani kwa ndani hilo si ajabu kutokea.

Kuna tetesi kuwa wale waliopigania uanzishwaji wake na kupelekea furaha kwa jamii ya kiislamu na faida kubwa kwa wananchi kwa jumla walipoona wimbi la ufisadi na mbinu zao kuzidiwa na watu hao waliamua kukaa pembeni kuliko kuangalia kinachotokea.

Moja ya matawi muhimu ya benki ya Amana ni pale Tandamti ambapo awali wafanyabiashara wakubwa wa kiislamu walijazana kuweka fedha zao. Mara kadhaa nimekwenda nikakutana na wenzangu na mie wanaokwenda kutoa sh.10,000 za kununulia fungu la muhogo na dagaa. Inasemekana wengi wamekerwa na uzembe unaondelea wanapohitaji huduma kwenye benki hiyo.

Ushauri kama wapo wakereketwa wa benki ya Amana waliobaki katika uongozi wa juu basi wafukuze wapuuzi wote wanaotaka kutukanisha benki hiyo hasa kwenye vitengo ya teknohama na kila inapowezekana waanze kuajiri waislamu wenyewe kwanza wenye taaluma ya vitengo husika mbali mbali vya benki hiyo.
Salamu hizi zimfikie raisi Samia ili apeleke watu wake wakafuatilie mhimili huu wa uchumi iii mwaka wowote atakaondoka asije akaondoka na benki imekufa. Atabezwa kama alivyofanyiwa Kikwete aliyeondoka madarakani akiwawaacha masheikh wamerundikwa kwa makosa yasiyo na mbele wala nyuma.
Ni uongo. Bank ya Amana Asilimia 98 ya waajiriwa ni Waislamu. Umekuja hapa ichafua kwa maslahi ya nani wewe? Umetumwa?
 
Mimi naongelea hisa sio wafanya kazi ata pale amana benki wanao ujumu pale sio waislamu, katika top executive huwezi kukuta mwenye dini nyingine zaidi ya wakatoliki wale walio bobea kabisa.
Nitajie watatu tu. Uache uongo dogo.
 
Hatutaki huruma ya raisi.Ni wajibu wake kulinda vitega uchumi na kuzui mtafaruki wa wateja wa benki.Apeleke watu wataalamu wakafuatilie au awaite ikulu kuuliza kuhusu tetesi hizi na awashauri.
Huku ni kudeka na kutaka huruma. Rais anahusikaje na Bank ambayo si ya Serikali? Kwani taasisi haina organ ya check and balance? Acheni upumbavu wa kutaka kila kitu Rais ahusike. Wewe hata ukigombana na mumeo au mkeo utataka Rais atume mtu kufuatilia. Rais ana mambo mengi ya msingi.
 

Strongest Islamic banks in 2021

World's largest Islamic banks in 2022

Note: Countries include Bahrain, Egypt, Indonesia, Kuwait, Malaysia, Pakistan, Qatar, Saudi Arabia, Turkey, and United Arab Emirates. At end-2013, there were about 410 Islamic banking institutions worldwide, including the fully Shari'ah compliant banking systems in Iran and Sudan.
Nioneshe katika hizi 5 hapa ipi ya kiislamu

 
Amana sina hamu nayo. Benki ya kipuuzi yenye wafanyakazi wapuuzi hakuna mfano. Wanapoteza wateja wenyewe.
Haitashindwa kwa sera.Uislamu utabaki ndio mfumo bora wa masuala ya kifedha mpaka kiama.
Amana wanahujumiwa kimfumo na wameingia watu wasioweza kujitetea na wasiosikiliza ushauri.Hili limekuwa ni furaha kwa maadui wa uislamu ambao tangu mwanzo hawakutaka mfumo huu wa kibenki uingie nchini..
Ndani ya jukwaa hili la JF kuna uzi mrefu uliojaa malumbano ya kuingia mfumo wa benki ya kiislamu Tanzania.
Namna wanavyopoteza wateja kizembe ni kama vile masuala nyeti yanayohusu wateja kuachiwa watoto wanaokwenda field kuyashungulikia.
Leo unaweza ukapigiwa simu kuhusu akaunti yako kuna jambo fulani limeelekezwa na BOT na ukaamua kulitii.Kesho yake anakupigia mtoto mwengine kuulizia na kuelekeza kitu tofauti.Mimi nikaona pamoja na uzalendo wangu sitaki ujinga huo.Na ukiamua kukaa kimya hakuna anayekuuliza mbona hivyo.
Kuna masuala nyeti ya uhai wa kibenki hayatakiwi kuguswa na watoto wa mihemko ya Zuchu.
 
kukopesha bila riba inawezekana kwa watu binafs ila taasisi haiwezi survive bila riba
It seems hauna uelewa kabisa na masuala ya benki hasa islamic banking!! Kuna mapato yanayopatikana kuendesha benki not necessarily mpaka iitwe "riba"!! na pia hiyo huduma ipo benki hata za secular kama CRDB au NMB na zinaingiza faida sana tu sababu wafayabiashara wakubwa wote wana channel pesa zao huko kufanya investments!!
 
Yaani nahitaji pesa nikanunue passo ya milioni 8 unaninyima ela unaenda kuninunulia hiyo passo na kunidai milioni 10 alafu unaniambia hakuna riba?? Natakiwa niwe mbumbumbu kwanza ndio niamini huo upuuzi, kitu bila riba nipe milioni kumi nikurudishie milioni kumi kwa muda wa miaka mitano, hiyo ndiyo interest free, out of that ni utapeli kama utapeli mwingine
@MZAWA JF hiyo ndio biashara sasa ! Riba ni Hela kwa Hela umechukua Milion 8 unarudisha 10 ila gari umeletewa tu we utajua mwenyewe imenunuliwa bei gani. Ila unalipa kwa instalmente mpaka ifike Milion 10.!
 
Islamic banking mbona inatolewa mpaka na benki "zingine" mfano KCB, NMB, CRDB wanaita Sahel banking kama huduma inayojitegemea. Why huko hazifeli? Ni kama tu benki ya mwingira ilivyokufa au ile mkombozi benki iliyotumika kuiba pesa za Tegeta ESCROW wala hakuna uhusiano wa performance ya benki na dini. Ingekua hivyo CRDB ingeporomoka maana MD wake ni muislam

Una akili ndogo sana hasa huo mfano wa md wa crdb,hapa inshu ni uongo na unafiki wa kusema hizo benki hazitozi riba,riba ipo sana na wanachukua ila wameibadili jina.
 
@MZAWA JF hiyo ndio biashara sasa ! Riba ni Hela kwa Hela umechukua Milion 8 unarudisha 10 ila gari umeletewa tu we utajua mwenyewe imenunuliwa bei gani. Ila unalipa kwa instalmente mpaka ifike Milion 10.!
Benki inafanya biashara ya magari? Ni financial institution au car dealer? Kwa nn iseme imenikopesha pesa bila riba isiseme imenikopesha gari?
 
Back
Top Bottom