Benki ya CRDB yaanza kutoa mikopo ya ada Shule za Msingi na Sekondari

Benki ya CRDB yaanza kutoa mikopo ya ada Shule za Msingi na Sekondari

hii ni indicator ya umaskini uliopo Tanzania. kwamba watu hawana uhakika wa kulipa hadi karo za wanafunzi.

Halafu rais anasifiwa kwenye kila kitu hadi ujinga
Hujielewi nchi zilizoendelea ikiwemo Marekani watu wanaishi kwa credit card kila kitu wanakopa

Tatizo lako ulofa na huna exposure ya nje maskini mkubwa wewe na utakufa lofa na kingereza chako cha indicator
 
Miezi 6 mbona ni muda mchache sana. Kuna tofauti gani na program za kulipa kwa awamu zilizopo mashuleni moja kwa moja?

Shida ya huduma nyingi za mikopo ya Tanzania ni muda mfupi unaopewa kulipa.
kwa akili yako ukipewa huo mkopo na ukilipa kidogokidogo kwa miaka miwili huku ukiweza kukopa tena ndio nafuu kwako
 
Mimi kama mzazi naona kwamba....
Kama nimeshindwa kujipanga na kulipia ada ya watoto wangu kwa mwaka mzima, then basi nibora nikawapeleka shule za kayumba.
Inakuwaje hapo mwanzo labda uwezo ulikuwa nao tuseme mtoto yupo darasa la sita, maisha yana changamoto nyingi..inatokea mzazi umepigwa nje ya mfumo? Si ni fursa nzuri hii mtoto aende shule halafu mzazi unajitafuta ulipe mkopo?
Shida niliyoona hapo muda ni mfupi inakuwa kausha damu tu kama kausha damu za mitaani.
 
Nashauri tu mfumo wakulipa ada wangelipa ada ya mwanafunzi mwaka mzima na marejesho mzazi alipe mwaka mzima hadi muda wa kukopa ada ya mwaka unaofata. Riba hata ingekuwa 20% sio mbaya.
 
If you don't Pay for a Product.., You are a Product; apart from hio 13 percent hapo naona recruitment / incentive ya watu kutumia mfumo wao wa malipo na hivyo kuokota transaction fees za hapa na pale...; Which is not bad as the end justifies the means...
 
If you don't Pay for a Product.., You are a Product; apart from hio 13 percent hapo naona recruitment / incentive ya watu kutumia mfumo wao wa malipo na hivyo kuokota transaction fees za hapa na pale...; Which is not bad as the end justifies the means...
VYovyote vile ni sawa , lengo watoto waende shule.
 
Tatizo la hii mikopo unaishi maisha ambayo si yako, kama nimeshindwa kukusanya hela ya ada 6m ya wanangu kwa mwaka je nikikopa nitaikusanyaje niwarudishie bank na riba juu yake.

Dawa ya wazazi wenzangu ukishimdwa kulipa ada mwenyewe basi hamisha mtoto akasome kayumba fc, si dhambi.
 
Back
Top Bottom