Benki ya CRDB yaanza kutoa mikopo ya ada Shule za Msingi na Sekondari

Nchi zenyewe zinakopa zikiwemo matekani na ulaya sembuse mtu binafsi
Hakuna nchi dunia serikali yeyote yenye uwezo wa kukusanya cash bila kukopa kuendesha serikali zao

Kukopa kiwango na kulipa kidogokidogo ndio mtindo wa dunia mzima sasa hivi
Yes unakopa kwa project maalum ambayo tayari unayo mkononi na ukilipwa utarudisha pesa zao zote na raba yao juu - unabaki na faida nzuri

Sasa hii mikopo midogo midogo inaongeza umaskini wa familia - mama mikopo baba mikopo - kwangu siafiki kabisa.

Jaribu kuishi kwa namna uwezo wako ulivyo utaishi kwa furaha saana.
 
Asan
Asante CCM Kwa kutufanya Maskini hadi haiwezekani kulipa ada bila Mikopo
 
Kwahiyo huu mkopo wa riba ya 13% unaotakiwa kulipa ndani ya miezi 6,,,benki wanaita ni huduma,,,hapana hii ni biashara tena yenye faida kubwa kwa benki.
 
Mh riba mlimaaa
Hapo ndio wamekosea, ilibidi rejesho liwe mwaka mzima likutane na mkopo wa mwaka unaofuata, yaani unamaliza deni tu unasaini mkopo mwaka unaofuata, au kama upepo umekaa vizuri unaachana nao.
Miezi sita ni muda mfupi sana mkopo utakuwa wa moto. Kwanini wao walipe ada ya mwaka mzima halafu wewe ulipe mkopo miezi sita? Wakopeshe nusu ada mzazi alipe miezi sita
 
sasa kalipe kama unayo huko shule kidogokidogo
 
Kwanini tunateseka na hili zigo zito la ada lakini.
Na alaaniwe aliyeleta fikra ya kwamba kusomesha watoto shule za serikali ni umasikini na aibu.

Najua walioeneza hiyo imani ni wamiliki wa hayo mashule ya kulipia ili watunyonye vizuri wtz.
 
Benki ya CRDB leo imezindua huduma ya ada loan. Tukikwama sana kulipa ada tukutane kwenye App. It's innovative, malipo yake ni ndani ya mwaka. Inafanya kazi kama advance salary, lakini ada hulipwa moja kwa moja kwa shule husika au chuo from bank!
 
Mi naona hii ni huduma nzuri, ila inavyoshambuliwa hapa!
 
Mi naona hii ni huduma nzuri, ila inavyoshambuliwa hapa!
Huduma nzuri ila ni waongo Yaani wanasema riba ya asilimia 13 ni ndogo tofauti na iliyopo sokoni wakati sokoni benki zote riba 12% except NBC wao ni 13%.

Sijaelewa waliposema kwa wateja wao na wasio wateja wao.
Kwa wasio wateja watawekewa utaratibu upi kulipia
 
Benki zipi riba ni asilimia 12? Au ni aina gani ya mkopo benki nyingi riba zina range 16-17. Wachache 14 na 15.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…