Benki ya Dunia: Wanaotumia chini ya Tsh. 7,834 kwa siku ni maskini kupindukia

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚nna mambo mengi. Alafu age go yani kunavit nikivimaliza nitarelax yani nitafanya na kasherehe now acha tu niwe fukara mahesabu ni muhimu sana
Wewe ndio unajisemea kuwa age go. Alafu nikwambie kitu mamii... Wanawake wengi especially wa kiafrika wanazubaa kwa hii kauli ya kujiona age go baada ya 30s na kupunguza munkari wa kujitafuta katika angles zote za kimaisha. Hii imekuwa ni psychological torture kubwa sana kwa wanawake wanaofikisha huo umri wakiwa bado hawajapata watoto au wenza achilia mbali kujipata kimaisha. Ila mimi nawaambia kuwa umri wa mapambano sahihi na kufanya mambo yenye tija zaidi maishani bila majuto ni kuanzia 30 na kuemdelea.
 
Sasa sie tunaoishi kwa buku tatu jero kwa siku tunaitwaje? πŸ˜‚
 
Kwa muktadha huo, mtu yeyote anayeishi kwa kutumia kiasi cha chini ya TSh 7,834 kwa siku sasa atahesabika kuwa anaishi katika umasikini uliokithiri,
Ni ngumu kuweka kipimo kimoja kiwe relevancy kwa watu wote na nchi zote.
binafsi sioni mantiki ya kupima umaskini kwa kuangalia matumizi,nadhani wangeangalia kipato,yaani wangesema "mtu anayeingiza chini ya dola 3 per day huyu ndio maskini" hapo at least inge make sense!

Kicho kipimo chao kipo biased!kwasababu mtu anaweza kuingiza hela nyingi lkn akatumia kidogo,ukitazama hiki kipimo chao,mtu aliyekopa then akafanya matumizi makubwa,ataonekana ni tajiri,hata kama ana negative balance!
Hivi vipimo Ni falsafa za kimarekani,gdp ya nchi ni Kama $ 29T harafu deni la nchi ni $36T,harafu tunasema USA ndio richest country,wakati wapo insolvency.
 
Mama yangu,Tz lazima ktk nchi 5 za mwisho duniani dhoofu lahali itakuwepo
 
Nimeamaanisha kuna vitu nimevipa kipaumbele kwa wakati huu sio vya harrak lakini. Umakini ni muhimu bajet zipangiike vizuri
 
Watu wazima na familia zao
Gosh! No wonder hiyo tafiti imesema hivyo, like how mzee? Tuna safari ndefu kama taifa kufikia Middle class, imagine huyo mtu anasomesha, kulipa kodi n.k.
 
Dah we jamaa umefanya nicheke kama mazuri vile
 
Sidhani kama ni kula tu ..
Chakula
Umeme
Maji
Transport
Mengineyo (10% ya mahitaji)
Nadhani ni kama mtu akuambie naomba budget yako ya siku, huwez kutaja msosi tu
Sasa hawa watu wanaosema wanasurvive kwa elfu 7 and below wanaishije mjini?, bado nawaza...ndio maana nikasema kwenye mchango wangu labda ni hawa young ages ambayo hawana majukumu and they don't pay bills.
 
Unachosema ndio wanaita PPP (purchasing power parity) na kwenye hiyo taarifa yao wamesema wamezingatia PPP tayari na kuja na hiyo hesabu
 
Really? Interesting! Una familia? Unafanyaje fanyaje, ebu tupe experience yako kama hutojali.
Hiyo 7000 wanammanisha kwa MTU mmoja sio familia, ukiwa na familia ya watu 4 unatakiwa usitumie chini ya 28,000 kwa siku (laki 9 kwa mwezi) ili usiingie hilo kundi
 
Hiyo $3 ni thamani ya mahitaji muhimu ya binadamu kwa siku, sio lazima iwe cash.
Halafu uko unakotoka watu hawasafiri kabisa ? hawanunui nguo ? Mahindi wanasagia kwenye mawe? watoto hawaendi shule? Watu hawanuni sukari, chumvi, ngano, sabuni, viberiti, mafuta, vitunguu, nyanya, mchele, matunda??
 
Leo sijatumia hata mia,mimi ni nani
 
Dah we jamaa umefanya nicheke kama mazuri vile
WB wao wanapima maisha kwa standard gani sijui?

Ni uhalisia uliopo maisha ya vijijini.

Ila naamini wao wanadhani watu wote wanakula milo mitatu.

Kuna watu wanakula milo miwili tena siyo iliyokamilika kwa vigezo vyo.

Fikiria unakula ugali wa muhogo na mboga za mahani usiku na mchana kila siku.

Sasa hapi kwa vigezo vyao tunatumia dollar ngapi kwa siku?
 
Mzee unajua maana ya average? Huwezi ukasema MTU amekopa halafu akafanya matumizi makubwa kwa siku akaonekana tajiri, sababu hiyo haiwezekani kwa muda mrefu.

Hesabu inachukulia wastani wa thamani ya matumizi ya MTU kwa siku
 
Hiyo $3 ni thamani ya mahitaji muhimu ya binadamu kwa siku, sio lazima iwe cash.
Halafu uko unakotoka watu hawasafiri kabisa ? hawanunui nguo ? hawanuni sukari, chumvi, ngano, sabuni, viberiti, mafuta, vitunguu, nyanya, mchele, matunda??
Hayo yote nimesema hapo juu, chumvi wanabadirishana yani butter trade, yale mjini mnaita makopa kule tunaita udaga kwa chumvi, nguo na matandio na mengineyo ni kwa kuuza mazao hayo kama udaga, mtama mahindi au usubiri msimu wa pamba.

Ni hii ni kweli siyo story, nimeona kwa macho yangu.

Mahitaji makubwa watauza Ng'ombe au mbuzi kama wapo.

Vigezo vyao huwa standard inayo fit wote.
 
Wala ata mi sijali masikini sijui fukara niiteni mtavojiskia kuniita ila standard yng naijua mwenyewe
 
Unachosema ndio wanaita PPP (purchasing power parity) na kwenye hiyo taarifa yao wamesema wamezingatia PPP tayari na kuja na hiyo hesabu
Huwezi ukaweka a blanket figure wakati matumizi yanatofauti kubwa sana.., UK ka apartment mtu unakaa kama njiwa na bila pesa ya kununua gesi unaganda kwa baridi inawezekana hata ukilipwa dollar 400 kwa wiki huenda ukawa ni masikini wa kutupwa; wakati mmasai ambaye housing its cheaper to free (na kuna sehemu hata nyumba ni tupu) na akitaka chakula akienda gengeni mlo mmoja wa mchana wa mtu wa UK yeye anaweza akala mwezi mzima....

Hence huwezi ukatumia matumizi ya kiasi fulani cha pesa kuonyesha fulani kama ni masikini au hapana....; Hususan hakuna sehemu watu wanaishi sustainably kama vijijini na wanapata all their basic needs na kuishi a fulfilling life
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…