Benki ya Dunia yaikopesha Tanzania Tsh. 2.3 trilioni

Kumbe na wewe umeona eh?

World Bank hawatoi mikopo ambayo inawajengea uwezo wa kujitegemea, wanatoa pesa kwa miradi hewahewa ili muwe watumwa wa deni

Hii mikopo ingekuwa ya reli, umeme, maji ingekuwa ya maana ,maana hivyo vitu vinadumu na vinachangia kwenye uchumi

Samia awe makini siyo anakopakopa tu, deni la Taifa limeshakuwa kubwa sana hatuhitaji kukopa kwa vitu visivyokuwa na tija ya direct kwenye uchumi!

tushapigwa tayari.

si kuna uzi huku ulikuwa unauliza mzunguko wa pesa!!ndio zarudishwa sasa.
 
Wamekopa trillion 2 kwa miradi ya kipuuzi kabisa.

Miradi yote hamna hata mmoja unaoiwezesha nchi kujitegemea.
Kuna tatizo bado

Ni Sawa na kukopa pesa ukanunue suruali
 
View attachment 1810912

Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Dunia imeidhinisha mikopo minne yenye masharti nafuu yenye jumla ya dola za Marekani bilioni 1.017 (sawa na shilingi trilioni 2.3391) kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wakati akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma.

Mhe. Dkt. Nchemba alisema kuwa miradi iliyopata idhini ya Bodi hiyo ni mradi wa kuboresha barabara za vijijini (RISE) wenye mkopo wa dola za Marekani milioni 300 na mradi wa kuimarisha mazingira ya ufundishaji na mafunzo katika taasisi za elimu ya juu (HEET) wenye mkopo wa dola za Marekani milioni 425.

“Miradi mingine ni mradi wa kuongeza upatikanaji wa huduma bora za mtandao (DTP) wenye mkopo wa dola za Marekani milioni 150 na Mradi wa kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma bora za umeme visiwani Zanzibarwenye mkopo wa dola za Marekani milioni 142,” alisema Mhe. Dkt. Nchemba.

Alieleza kuwa mradi wa kuboresha barabara za vijijini utahusisha ujenzi wa jumla ya kilomita 535 kwa kiwango cha lami katika wilaya sita za mikoa ya Iringa, Lindi, Geita na Tanga na ukarabati wa maeneo korofi ya barabara za vijijini nchi nzima.

Alisema kuwa mradi wa kuimarisha elimu ya juu utaimarisha mazingira ya ufundishaji katika Taasisi za Elimu ya Juu katika fani za kipaumbele cha Taifa, kupitia upya na kuboresha mitaala ya vyuo vikuu ili kuwa na wahitimu wanaoendana na soko la ajira na kuchangia maendeleo ya nchi na uchumi kwa ujumla.

“Mradi wa kuongeza upatikanaji wa huduma bora za mtandao utasaidia kuongeza upatikanaji wa huduma bora za mtandao wa intaneti na kuboresha huduma za umma kwa kutumia digitali kwa kustawisha ekolojia ya digitali nchini, kuhakikisha uunganishaji wa kidigitali kwa Watanzania wote na kuboresha jukwaa la huduma za kidigitali,” alifafanua Mhe. Dkt Nchemba.

Alisema kuwa Mradi wa kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma bora za umeme visiwani Zanzibar utasaidia upatikanaji wa huduma bora na za uhakika za umeme visiwani humo ikiwa ni pamoja na kujenga mitambo yenye uwezo wa kuzalisha umeme wa kiwango cha MW 18 kupitia nishati jadidifu ya nguvu ya jua na msongo wa kV132 wa kusafirishia umeme katika visiwa hivyo.

Waziri Dkt. Nchemba aliishukuru Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Dunia, Menejimenti ya Benki ya Dunia Ofisi ya Tanzania, pamoja na Watumishi wote wa Serikali walioshiriki katika kufanikisha upatikanaji wa fedha hizo.

Akizungumzia kuhusu Deni la Taifa alisema kuwa mpaka sasa deni la Serikali ni dola za Marekani milioni 26,416.8 (sawa na Tshs 60.719.01 bilioni) ikijumuisha deni la nje dola za Marekani milioni 18,907.7 na deni la ndani ni dola za Marekani milioni 7,509.1 (sawa na sh. bilioni 17,259.9 na kwamba deni hilo ni himilivu.

Kwa upande wa makusanyo ya mapato ya Serikali Mhe. Dkt. Nchemba alisema yanaendelea vizuri ambapo lengo la makusanyo kwa kipindi cha miezi mitatu toka Februari 2021 hadi Aprili, 2021 lengo la makusanyo limefikiwa kwa zaidi ya asilimia 82.

“Mwezi Februari 2021, lengo la makusanyo lilifikiwa kwa silimia 82.9, Machi 2021, asilimia 84.1 na mwezi Aprili 2021, lilifikiwa kwa asilimia 83.2,” alifafanua Mhe. Dkt. Nchemba

Kuhusu akiba ya fedha za kigeni Mhe. Dkt. Nchemba alisema kuwa hadi kufikia aprili 30, 2021, akiba ilikuwa dola za Marekani milioni 4,969.7 ambayo inatosha kuagiza bidhaa kutoka nje kwa miezi 5.8 zaidi ya lengo la nchi la miezi 4 na pia zaidi ya lengo lililowekwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) la miezi 4.5.
Kimsingi hizo hela zipelekwa sehemu husika. Zitumike sehemu lengwa
Note
Juzi huyu mweguli alikubwa na kashifa kubwa ya upotevu wa hela kwenye wezera yake .je ?? Ataweza ku- manage hizo hela bila ubadhirifu kweli.

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Hizo white elephants projects hazichochei ajira kw wananchi wala kipato , ni upigaji Tu WA kipumbavu
 
Nimeuona huo mkopo nikabaki nashika kichwa...mabeberu hawajawahi kutaka kujitegemee...wanakupa mikopo itakayokufanya uendelee kuwategemea ili iwe rahisi kwako kupenyeza agenda zao.
Mkuu unazungumzia swala la sisi kujitegemea

Kama una ndoto hizo ktk Karne hii amka hapo usingizini
 
wala la ubakaji halipo,katika makosa yote yaliyosomwa sijui ni mangapi yanahusika na kuporwa haki raia wa kawaida.

hapo ndio utajua gia kumbwa ndio dhaifu zaidi.
Sabaya ni CCM na wanamhenyesha CCM wenzako
 
Mapato yameongezeka kidogo. Ukusanyaji ni zaidi ya 81% zamani ilikuwa chini ya 79%.
Hakuna kitu Kama hicho...hizo ni cooked figures....mwishowe mtasema na ujambazi umepungua kidogo wakati Mambo ni magumu mitaani na hakuna kutangazwa...
 
Zamani ndo ilikuwa coocked figure zinatolewa ndo maana hata takwimu zilidhibitiwa ili watoe wenyewe wanachotaka. Usiri mkubwa na ukatili vilificha maovu mengi sana.
 
Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Dunia imeidhinisha mikopo minne yenye masharti nafuu yenye jumla ya dola za Marekani bilioni 1.017 (sawa na shilingi trilioni 2.3391) kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wakati akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma.

Mhe. Dkt. Nchemba alisema kuwa miradi iliyopata idhini ya Bodi hiyo ni mradi wa kuboresha barabara za vijijini (RISE) wenye mkopo wa dola za Marekani milioni 300 na mradi wa kuimarisha mazingira ya ufundishaji na mafunzo katika taasisi za elimu ya juu (HEET) wenye mkopo wa dola za Marekani milioni 425.

“Miradi mingine ni mradi wa kuongeza upatikanaji wa huduma bora za mtandao (DTP) wenye mkopo wa dola za Marekani milioni 150 na Mradi wa kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma bora za umeme visiwani Zanzibarwenye mkopo wa dola za Marekani milioni 142,” alisema Mhe. Dkt. Nchemba.

Alieleza kuwa mradi wa kuboresha barabara za vijijini utahusisha ujenzi wa jumla ya kilomita 535 kwa kiwango cha lami katika wilaya sita za mikoa ya Iringa, Lindi, Geita na Tanga na ukarabati wa maeneo korofi ya barabara za vijijini nchi nzima.

Alisema kuwa mradi wa kuimarisha elimu ya juu utaimarisha mazingira ya ufundishaji katika Taasisi za Elimu ya Juu katika fani za kipaumbele cha Taifa, kupitia upya na kuboresha mitaala ya vyuo vikuu ili kuwa na wahitimu wanaoendana na soko la ajira na kuchangia maendeleo ya nchi na uchumi kwa ujumla.

“Mradi wa kuongeza upatikanaji wa huduma bora za mtandao utasaidia kuongeza upatikanaji wa huduma bora za mtandao wa intaneti na kuboresha huduma za umma kwa kutumia digitali kwa kustawisha ekolojia ya digitali nchini, kuhakikisha uunganishaji wa kidigitali kwa Watanzania wote na kuboresha jukwaa la huduma za kidigitali,” alifafanua Mhe. Dkt Nchemba.

Alisema kuwa Mradi wa kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma bora za umeme visiwani Zanzibar utasaidia upatikanaji wa huduma bora na za uhakika za umeme visiwani humo ikiwa ni pamoja na kujenga mitambo yenye uwezo wa kuzalisha umeme wa kiwango cha MW 18 kupitia nishati jadidifu ya nguvu ya jua na msongo wa kV132 wa kusafirishia umeme katika visiwa hivyo.

Waziri Dkt. Nchemba aliishukuru Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Dunia, Menejimenti ya Benki ya Dunia Ofisi ya Tanzania, pamoja na Watumishi wote wa Serikali walioshiriki katika kufanikisha upatikanaji wa fedha hizo.

Akizungumzia kuhusu Deni la Taifa alisema kuwa mpaka sasa deni la Serikali ni dola za Marekani milioni 26,416.8 (sawa na Tshs 60.719.01 bilioni) ikijumuisha deni la nje dola za Marekani milioni 18,907.7 na deni la ndani ni dola za Marekani milioni 7,509.1 (sawa na sh. bilioni 17,259.9 na kwamba deni hilo ni himilivu.

Kwa upande wa makusanyo ya mapato ya Serikali Mhe. Dkt. Nchemba alisema yanaendelea vizuri ambapo lengo la makusanyo kwa kipindi cha miezi mitatu toka Februari 2021 hadi Aprili, 2021 lengo la makusanyo limefikiwa kwa zaidi ya asilimia 82.

“Mwezi Februari 2021, lengo la makusanyo lilifikiwa kwa silimia 82.9, Machi 2021, asilimia 84.1 na mwezi Aprili 2021, lilifikiwa kwa asilimia 83.2,” alifafanua Mhe. Dkt. Nchemba

Kuhusu akiba ya fedha za kigeni Mhe. Dkt. Nchemba alisema kuwa hadi kufikia aprili 30, 2021, akiba ilikuwa dola za Marekani milioni 4,969.7 ambayo inatosha kuagiza bidhaa kutoka nje kwa miezi 5.8 zaidi ya lengo la nchi la miezi 4 na pia zaidi ya lengo lililowekwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) la miezi 4.5.
Ukiacha kuboresha barabara za vijijini miradi iliyobaki huwezi kuona matokeo yake zitakua hela za kuliwa na wajanja. Magu asingekubali mikopo ya kubembelezewa na benki ya dunia. Hii benki ni ya kimkakati kwa mabeberu kuhakikisha nchi changa ni wadeni wa mabeberu daima.
 
Mbona shetani Ngosha alikuwa anakopa hela na kuishia kuweka kwenye account zake binafsi.

Dikteta alikuwa jambazi wa Mali za umma
Kwani account yake ilikufa? Mkachukue sasa kmaa kuna hela zisizohalalo
 
Deni la Taifa ambalo ni zaidi ya 65 trillions sasa litakuwa linakaribia 70 trillions.

Back
Top Bottom