Benki ya Dunia yaikopesha Tanzania Tsh. Trilioni 1.2 za Miradi ya Maji na Afya

Benki ya Dunia yaikopesha Tanzania Tsh. Trilioni 1.2 za Miradi ya Maji na Afya

Hii nchi ni kama haina mwenyewe make na raia tushageuka kuwa mashabiki wa wapigaji, kwamba mkopo wa WB unaenda kufanya kazi ya usafi wa mazingira vijijini, aisee inachekesha sana kuhuzunisha sana.

Nchi inaliwa sana hii na mbaya zaidi sisi raia tunashangilia ila hii mikopo haitalipwa na Mwigulu wala Samia wala Majaliwa bali ni sisi choka mbaya ndio tutapandishiwa bei ya vitu kulipa hii mikopo.

Haiingii akilini kwamba hizo pesa zipo zitakazoenda vijijini kuboresha usafi wa mazingira.

View attachment 2533055
Wanaenda kusafisha Mazingira vijiji gani wakati Majiji yetu yote Machafu yamewashinda!
 
Tatizo hujaimgia kiundani ukajua inakuwaje. Iko hv hiyo fedha inaenda kuboresha Mambo matatu.
1. Ushambazaji wa maji vijijini. Kwanini maji? Kwa sababu kama Hamna maji Hamna usafi kwenye taasisi na kaya zetu hususani kwenye ishu ya sanitation
2. Uboreshaji miundombinu ya vyoo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya na kwenye Shule za msingi
3. Uboreshaji wa hali ya usafi kwenye taasisi za elimu na afya. Lakini lazima ujue huu mpango hautafaidisha wote kwa kiwango sawa kwenye halmashauri zetu Bali Halmashauri zitakazokuwa na watendaji wenye bidii kutimiza vigezo vya uboreshaji hiyo miundombinu na usambazaji wa maji ndio watakaovuna fedha kwa ajili ya kupanua huduma. Yaan unavuna kwa kadri utakavyo perform. Kwa uchache ndio hvyo
Acha siasa Jiji la Mwanza lipo karibu na Ziwa lakini ukienda Kisesa,Magu,Kayenze,Usagara na ata pia sehemu zingine za pembeni ya mji hazina maji,leo ukaseme wanaenda kuboresha vijijini kama sio utapeli ni nini?
 
Hivi hiyo #2 ninyi ccm huwa hamsikii aibu kuitaja?

Yaani dunia ipo 21 century lakini ninyi hela ya kuboresha vyoo tena vya sehemu muhimu kama hospital mnaandika kabisa proposal kwa mzungu mpewe hela ya kwenda kuvikarabati,nitakuwa wa mwisho kuamini kwamba huwa mnaandika kweli dhumuni la matumizi ya hizo hela then muweke sababu hizo.
Hizo pesa tukisimamia Mapato ya Utalii na Bandari kikamilifu,tunazipata vizuri tu.
 
Kwahyo tuache watoto wetu wajisaidie vichakani?
Kwanini kuacha watoto kujisaidia vichakani?hizo V8's mnazogawana mpya kila mwaka mkisema muache mwaka mmoja tu hivyo vyoo havitatengenezeka?

Hivi kweli unatetea waziri anayejipambanua ni msomi na Dr wa uchumi akiwa amevaa suit na tie ya kizungu kwenda kusainishwa mkataba wa kukopa hela ya kujengea vyoo karne hii???tena na picha mmepiga?
 
Nina Imani mpaka Samia anaondoka madarakani, huduma za afya zitakuwa zimefika Kila Kona, maji ndio usiseme, yatajaa Kila mahali kama mate mdomoni

Na deni litakua 200trillion. Zile Tozo zinakwenda wapi??
 
Bwawa la Julius Nyerere liko asilimia 85 ujenzi, valvu ya tatu kwa ukubwa duniani kupelekwa hapo, mtambo mkubwa wa tani 79 unaitwa runner umepelekwa ktk bwawa, Daraja la Jp Kigongo Busisi spidi kali, madaraja huoni Chang'ombe, Uhasibu, Kurasini, meli ya Mv Mwanza Hapakazi chombo kiko majini.

Huduma za maji, afya na nyingine hadi vijijini. Nchi kubwa hii ndugu yangu na kila Mtanzania anataka maji, umeme, barabara, afya, elimu nk. [emoji120][emoji120][emoji120]

Ukarabati wa kivuko kilichopelekwa kenya. Mv magogoni
 
Kuhusu kusafisha mazingira....ni sawa!! Ila
Je,
Kuna jambo huko....
Je wamekurupuka au kukurupushwa kuhusu viwanda na utengenezaji wa malighafi na utupaji wake taka vinaonekana kuwa vinachangia uchafuzi wa mazingira huko vijijini?

Au ni Migodi?

Au ni Mazingira machafu yanayotengenezwa na Hospitali, zahanati, dispensari n.k

Titaelewa.
 
Nina Imani mpaka Samia anaondoka madarakani, huduma za afya zitakuwa zimefika Kila Kona, maji ndio usiseme, yatajaa Kila mahali kama mate mdomoni
Huo utakua ukame, mdomoni hakunaga mafuriko ya maji.
 
Swali langu ni dogo tu; je, hii mikopo huwa inaidhinishwa na Bunge au Cabinet kabla ya kuomba au ni utashi wa Rais/Waziri wa Fedha? Budget yake kwenye matumizi na marejesho inajulikana kabla ya kuombwa?
 
World Bank imeidhinisha mkopo was Trillioni 1.3 Kwa Tanzania.

Haya sasa wale wenye kamba zenu mzigo wa pasaka huo umetua.
 
World Bank imeidhinisha mkopo was Trillioni 1.3 Kwa Tanzania.

Haya sasa wale wenye kamba zenu mzigo wa pasaka huo umetua.
Under the arrangement, the World Bank will extend $300 million in credit and $4.93 million in grant funding to improve access to water supply and sanitation in Tanzania.

"We expect up to 10 million Tanzanian citizens will gain access to improved water supply and 9 million to improved sanitation facilities. Also, up to 2,500 healthcare facilities and over 1,600 primary schools will be provided with adequate sanitation and hygiene services," Mr Belete said.

Wacha wazungu wafanye biashara ya Vikoba kukopesha walalahoi. Eti 10 milioni tanzanians will have access to clean water. Kama miaka 61 hakuna maji,unadhani hizi ndizo zitasalimika, tena leo ambapo mteule anaonekama legelege katika kukemea WIZI! Mtu mwenyewe Nchemba? Time will tell!
 
Ushoga ndio unaingilia kwenye mikopo hyohyo
 
Nina Imani mpaka Samia anaondoka madarakani, huduma za afya zitakuwa zimefika Kila Kona, maji ndio usiseme, yatajaa Kila mahali kama mate mdomoni
Unazungumzia maji gani? Unaishi mkoa gani? Maji na umeme vinazidi kua kero
 
Mikopo ni mizuri hasa kama ina masharti nafuu...ila awamu hii wapigaji ni wengi balaa kitakachofika kwa wananchi ni % 50 yaani pasu kwa pasu kudadek!.
 
Tatizo hujaimgia kiundani ukajua inakuwaje. Iko hv hiyo fedha inaenda kuboresha Mambo matatu.
1. Ushambazaji wa maji vijijini. Kwanini maji? Kwa sababu kama Hamna maji Hamna usafi kwenye taasisi na kaya zetu hususani kwenye ishu ya sanitation
2. Uboreshaji miundombinu ya vyoo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya na kwenye Shule za msingi
3. Uboreshaji wa hali ya usafi kwenye taasisi za elimu na afya. Lakini lazima ujue huu mpango hautafaidisha wote kwa kiwango sawa kwenye halmashauri zetu Bali Halmashauri zitakazokuwa na watendaji wenye bidii kutimiza vigezo vya uboreshaji hiyo miundombinu na usambazaji wa maji ndio watakaovuna fedha kwa ajili ya kupanua huduma. Yaan unavuna kwa kadri utakavyo perform. Kwa uchache ndio hvyo
Mbona mlituambia zile za uviko zimemaliza tatizo la vyoo maeneo yote hayo!!!???

Ila bado kwa Nchi kukopa pesa kwa ajili ya vyoo ni aibu,nadhani wewe utakuwa umeweka maneno yako tu siyo kusudio la serikali kukopa mapesa yote hayo kwa ajili ya vyoo

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
View attachment 2532600 Waziri wa Fedha Mwigulu akisaini mikataba miwili ya mikopo ya masharti nafuu ya USD milioni 550 (sh. trilioni 1.264) kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya utelekezaji miradi ya afya ya mama na mtoto na mpango wa uendelevu wa maji na usafi wa mazingd
Kukopa siyo tatizo, tatizo ni kule kupokea taarifa za CAG zikibaini upigaji kwenye fedha za mikopo na kuyapuuza mapendekezo yake. Anyway mbuzi wa bwana heri nisisahau CAG kweli nae analipwa kwa fedha hizohizo anazoo-odit asante.
 
Back
Top Bottom