Benki ya Dunia yaitangaza Tanzania kuingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati

Ripoti ya Benki ya Dunia kutangaza rasmi kuwa uchumi wa Tanzania umepanda na kuwa ni wakati ni pigo kubwa sana kwa vyama vya upinzani.

Miaka 5 ya utawala wa CCM 2015-2020 hiki chama tawala kimedhihirisha wazi kimejirekebisha kwa kiasi kikubwa na kuamua kuwaletetea maendeleo watanzania.

Hongera kubwa ziende kwa Mwenyekiti wa CCM John Pombe Magufuli ambaye ni wazi amekuwa ni mwokozi wa CCM baada ya chama hiki kuwa na hali mbaya kabla ya 2015

Ni wazi tutegemee ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu ujao kwa chama tawala cha CCM
 
Anyamaze watu wazidi kulishwa ujinga? Boss, Karne hii bado unajivunia watu kuongozwa kama vipofu kwa kulishwa propaganda? Halafu unaandika kiswahili na kuchanganya na kiingereza ili uonekane ni msomi, huku ukitetea watu waongozwe bila kujua ukweli!
Dhana nzima ya utawala huu ni kuwatia ujinga watu, na huyo uliyemjibu hapo ndiyo sampuli sahihi ya waTanzania wa aina hiyo.

Kila kitu kinafichwa - COVID-19, hata hawajisumbui, bahati yetu nzuri, kwa sababu ambazo bado hazijulikani ugonjwa ukaishiwa nguvu; na wao bila aibu wanageuza hilo kuwa sifa kwao, hawaoni ujinga walioufanya na kujaribu kujirekebisha..

Lakini bado hawaoni aibu ya kuonekana vituko dunia nzima. Nani dunia hii ya leo anaweza kuamini chochote anachosema Magufuli!
 
Mkuu mimi sio mwanasiasa kabisa ila tu huwa sipendi upotoshaji na sijaanza tu leo ila sijawahi kuamini katika uchumi wa takwimu. Hata kuna paper nilifanya post grad ya kuhoji GDP kma ni kipimo accurate cha maendeleo ya watu. So napoona CCM imeanza propaganda eti ooh tumefika uchumi wa kati ndani ya miaka miwili mara sijui tumevuka malengo ya maendeleo inakuwa inakera kidogo maana najua haiakisi uhalisia.

2. Mie sijawahi kuwa mtu wa matukio hata siku moja hya mambo ya GDP nimehoji wachambuzi kadhaa hata kabla ya Tz kutangazwa sambamba na zimbabwe lol!!

This was 2018 january mind you!!

3. Kuhusu waTz kutopenda kusoma nmesema hilo sana huko JF Intelligence. Ukitaka kuhakiki tafuta thread za yule ccm mwenzio Fahami Matsawile huwa anachambua sana sera ila huwezi kuta comment hta moja thread zake!! Ila tukipata wananchi kma million 1 tu wanaojua kudadisi ndio wanasiasa wataacha kucheza na akili zetu.

4. Kuhusu mtu kuwa mlevi sidhani inahusiana na utendaji kma mtu analewa na ameweza kujenga chama hadi kikaenea nchi nzima then ntamuongezea crate jingine!!! Kwahiyo sijaona cha kubeza hapo ni sawa na kusema tukosoe uongozi wa Jiwe kisa kuhusishwa na mawaziri au ma-DC wake? Tumefikia huko?
 
Salary Slip,

Hatari kweli yaani growth ya $40 kwa Miaka 6!! Yaani kwa Mwaka tunaongeza $ 6.6 kwahiyo ili tufike Pato la $12,000 kutoka tuliopo sasa $1,090 inabidi Y = (12,000-1090)/6.6 = Nimepata Miaka 1600.
Haiendi hivyo mkuu.

At least kwa hilo tuwe wakweli.

Mara nyingi (sio mara zote), kasi (rate) huongezeka kadri kiasi kinavyozidi kuwa kikubwa. Haiwi 'constant' wakati wote kama unavyoifanya katika hesabu yako hapo.

Lakini pia 'rate' hiyo huporomoka, kama mfano unavyoonyesha kwenye bandiko la mbele hapo juu.
 
Leo nchi yetu imeingia kwenye orodha ya nchi zenye uchumi wa katika ndoto ambayo kila mtanzania alikuwa anatamani itimie.

Tanzania tulizoe jambo lolote baya likitokea hapa kwetu hata kama halina mashiko basi lazima hivi vyombo vya habari vikubwa kama BBC, Al JAZEERA, CNN n.k vitatangaza tena kwa kuzipa uzito mkubwa.
Sasa ajabu leo bank ya Dunia imeitaja rasmi kuwa Tanzania ni moja ya nchi zenye uchumi wa kati lakini hawa jamaa wamekuwa kimya kabisa kama hawaoni wala hawajui chochote.

Inamaana wapo tu kusubiri taarifa mbaya ndio waripoti lakini taarifa nzuri kama hizi kwao ni sumu?
Au hili nalo linavunja haki za binadamu na kukandamiza Democrasia?

Ndugu yetu Salim kikeke inamaana hajasikia chochote?

Ukimya huu una maana gani?
Wale wazee wa matamko umoja wa Ulaya hapa nchini vipi hawajatoa tamko lolote kupongeza hatua hii kubwa ambayo nchi yetu imepiga chini ya Rais Magufuli?

Tungetajwa kuongoza kwa madeni je napo wangenyamaza kama hivi?
 
Kwahiyo unataka kusemaje hapo mkuu.
Usikanganye takwimu za uchumi mfano hapo umeambiwa hiyo Dollar haijawa adjusted kwa PPP yaani haipimi nguvu ya pesa kwenye manunuzi kitu ambacho si kweli maana nguvu ya dollar 1 Tz na Dollar 1 zimbabwe sio sawa.

2. Hyo footnote inasema GNI haipimi welfare na Dev't ila yenyewe inachukua tu wastani wa kipato sio mtu mmoja mmoja na hpa ndio takwimu zinapokuwa misleading.

3. Haijawa adjusted kwa income inequality yaani mfano Trillion 6 za SGR zimeenda kwa kampuni ya mturuki basi pato la taifa litasoma kuna Trillion 6 zimeingia bila kujali nani na nani wamepata. Sasa ukienda kichwa kicjwa utaamini trillion 6 zipo kitaa kumbe kabeba mtu mmoja tu maana hta misumari wanaagiza nje!

Nachosema ni kwamba takwimu za kiuchumi hazisomwi kwenye kichwa cha habari bali CONTENT, na ndio maana siku Benki ya maendeleo Afrika ama IMF wakija na takwimu zingine kuonyesha ni Low income msije mkaanza kuwatukana ni mabeberu maana wao watakuja na formula tofauti tofauti so utaelewa nachosema.

NB: Jiulize zimbabwe pamoja na kuporomoka uchumi hadi negative growth kivp ndani ya mwaka wameingia ''uchumi wa kati'' .
Overview
 
Kwa hiyo wewe na hao walio toa hiyo taarifa nani mtaalamu sasa, unadhani kwamba wao hawajui hizo formula mkuu.?
 
Reactions: Oii
Ubishi wangu kwani mimi ndo naandaa data za WB?! Sasa wakati wewe unadai nchi ilishafika hapo since 2018, wenyewe WB wanasema hivi:-
View attachment 1494677

Sasa mimi na wewe mbishi hapo nani?!
Sikiza, huwa ukishafikisha wanakuacha kwa miaka kadhaa kuangalia kama utakuwa consistent, ili wasije kuweka nchi kwenye mid income afu ije kushuka waibadilishe tena.
Usijidanganye kwamba ni right away tumefika iyo tarehe moja July.
 
Anyamaze watu wazidi kulishwa ujinga? Boss, Karne hii bado unajivunia watu kuongozwa kama vipofu kwa kulishwa propaganda? Halafu unaandika kiswahili na kuchanganya na kiingereza ili uonekane ni msomi, huku ukitetea watu waongozwe bila kujua ukweli!
Kwa hiyo wewe Ndugu unasemaje?!
 
Hivi Magufuli ndiye aliyetangaza TZ kuwa middle income au ni WB? Kwa nini anashambuliwa Magufuli?
Hapo sasa ndio ushangae mkuu mana sijaelewa bado, hii taarifa kama ingekuwa ni report ya Prof Mpango kweli tungesema imepikwa, sasa huko WB nako sijui nani aliyeenda kupika hii report?
Kwahiyo huyu Fatma Karume yeye ni mtaalamu wa uchumi kuwazidi WB?
Wanasheria wa Tanzania huwa wanachekesha sana kujifanya wajuaji wa kila kitu.
 
Masikio yangu mabovu?nilichosikia umekua kufikia $4,045
 
Mkuu kwa jinsi ulivyojikamua apo juu kwa akili ya kawaida tu ina maana wewe una akili kuliko hao world bank.

Una miliki mfumo wako wa kipekee kabisa wa kudadavua uchumi wa kati ambao ndani yake una formular za kipekee zinazoonyesha na kutoa majibu kuwa ni Tanzania pekee kwenye hiyo list ya nchi za uchumi wa kati duniani ndiyo uchumi wake wa kati ni wa miguu juu chini,yani yenyewe imekuwa inakuwa kiuchumi kwa kuludi nyuma.

Mwisho kabisa nkuulize kitu??ushawahi kusikia mtu mwenye kipaji cha kuwa na roho mbaya....mkuu wewe ni zaidi ya huyo mtu,na hauko peke yako ni pamoja na hao waliokupa likes
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…