Benki ya Dunia yaitangaza Tanzania kuingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati

Isijeikawa njama za mabeberu kutukomoa kuwa tumefikia hatua hiyo ili tukose baadhi ya misaada na ruzuku!!!!! Kwa nini serikali yetu tukufu haikuliona hilo na kututangazia mpaka ilipotokea "sapraizi" ya WB?
 
HAwa ndo raia wa midle income
 
TBC si ipo

Hivyo vyombo ulivotaja kabla ya kutangaza habari huwa wanaipima. Kuna kitu kinaitwa news-worthiness. Yaani hii taarifa inafikia kiwango cha kuwa ni habari? Wao wasikilizaji wao ni wa dunia. Jee Tanzania kufikia lower-middle income ni habari au ni taarifa tu? Kuna nchi ngapi nyengine zime achieve hayo au zaidi ya hayo katika ripoti hiyo ya WB? Wazitaje zote au wachukuwe izilizo vuka malengo na zilizoshuka kiwango kuliko matarajio?

Tanzania ilitegemewa kufikia hapa ilipo kutokana na mwenendo wa taarifa za nyuma yake. Kwa hiyo hiyo siyo habari ya level ya kimataifa bali ni ya Local tu. Kwa hiyo tutegemee kutangazwa na TBC na EATV na local TV nyengine!
 
Sisi walalahoi ndio tuseme Kama huo uchumi wa Kati tunauona au labda utsjiri wa Laizer ndio umetupaisha
 
Kama wewe unajiita great thinker na unategemea serikali ikuajiri pole sana, serikali inaboresha mazingira, wewe unayatumia kuchapa kazi unapiga pesa. Over
Acha wenge, kwamba raisi aliyeahidi ajira kwa vijana aliwaongopea?
 
Mimi Naona Tujitangaze sisi ni NCHI ILIYOENDELEA.

Maana awamu hii hakuna kisichowezekana isipokuwa "Kutumia Akili na Maarifa"

Kama tumetengeneza ajira milioni 6.

Viwanda 8,000.

Corona Ipo Kote Isipokuwa Hapa Kwetu.

Ndege Za Watalii Zimejaa Booking, Watalii Wanakuja.

Tunaye yesu wa Lumumba Hapa Wa Kutoa na Kutwaa Vyeo.

Kimebaki Kipi Tena.
 
BBB Swahili wameongelea kwa kina asubuhi hii
 
BBC, CNN na Al Jazeera pia ubarozi wa USA ,UK nao Basi jamani watie neno hatavla kulaani au kupongeza yaani vyovyote vile maana WB huu Ni uminywaji wa democracy na haki za binadamu
 
Isingekuwa kwa yale Mawe ya bwana Laizer ssijui kama tungefika hapa.
 
Machadema yatapinga!
Kumbe nchi kuingia Uchumi wa kati ni kama kuvuka daraja kwenda ng'ambo.Kirahisi tu Mara paap tupo Kigamboni au Magogoni Fery.Tupo na vinchi kama Uswatini,Lesotho, Comoro!!! Yaani,hadi raha.
Mnaonaje sasa tukiweka mipango Wananchi wale bata kidogo?
 
Lower middle economyndio uchumi wa Kati?au ndio hali ya kutapatapa kiuchumi?au karibu na Nchi kuwa fukara
 
Hii ilielekezwa kwa wajinga kadhaa
 
Hongera Rais Magufuli pamoja na watendaji wako wote kwa kuifikisha nchi yetu ktk uchumi wa kati,
Magufuli hana mpinzani, zawadi yetu watanzania tutakupa kura 98% october 2020
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…