Benki ya Dunia yaitangaza Tanzania kuingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati

Pongezi JPM
 

Wao walitaka kusikia Tanzania uchumi umeshuka na haingii uchumi wa kati, yaani uchumi wetu uwe sawa na Zimbabwe huo ndio wimbo wanaoimba kila siku matokeo yakiwa tofauti wanakuja na data zao ohh miaka mitano imeongezeka hivi ohhh tulikuwa hivi Mara vile , hata huu uchumi wakati umepatikana toka 2018 sasa hivi goal wamehamisha wa nakuambia miaka mitano , hapa cha msingi ni kujipongeza kuwa tuko ndani vibaya sana kama taifa.
 
Baada ya Tanzania kutangazwa Rasmi na Bank ya Dunia kufikia Uchumi wa Kati Julai 1st,2020 miongoni mwa Nchi zilizofikia Uchumi huo,Dniani kote imekuwa gumzo kwa pongezi. Sifa zote zimekwenda kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Rais JOHN POMBE MAGUFULI kwa hatua hiyo kubwa ya kukuwa Kiuchumi.

VIVA MAGUFULI ,TANZANIA JUUU ZAIDI
 

Ww ni kilaza fulani ndio maana hata kuandika kwa ufasaha huwezi. Neno sahihi ni uuze, na sio uhuze. Hakuna kitu kinaitwa wataharamu, bali ni wataalamu. Hapo tu inaonyesha ww ni kilaza wa kiwango cha juu sana. Kaa kushoto tafadhali.
 

Hongera awamu ya tano kwa mafanikio hayo makubwa. Nchi zingine ambazo tupo kundi moja unaweza kuziona kupitia hii link World Bank Country and Lending Groups – World Bank Data Help Desk

Ahsante
 
Kwahiyo benk ya dunia wamedanganya?
 
Uchumi wa kati wa chini, ni tofauti na uchumi wa kati, hata hivyo kuna nchi ndogo nyingi tu ambazo zimeingizwa na si Tanzania tu Afrika Mashariki.
 
Kwahiyi WB wamedanganya? Kwamba Tz haipo kwenye hilo kundi la nchi za uchumi wa kati?
Au wewe unachopinga hapa ni kipi hasa? Unawapinga WB au unajaribu kufanyaje yani?
 
Kweli tumepata sifa hiyo lakini safari ya hadhi hiyo kujidhihirisha kwenye maisha ya kila mmoja bado ni ndefu
 

Aandika Rais mtarajiwa wa JMT Ndugu Z. Zitto Kabwe "
Zitto: "Mwaka 2015 pato letu lilikuwa USD 1,060, kuingia pato la kati la chini ni 1,090 lengo la nchi ni kufika USD 3,000. Sasa sherehe za nini"

kumbe tulishaingia uchumi wa kati mwaka 2015, maana mpango kasema ni kati ya $1036 mpaka $4045.
 
Kwahiyi WB wamedanganya? Kwamba Tz haipo kwenye hilo kundi la nchi za uchumi wa kati?
Au wewe unachopinga hapa ni kipi hasa? Unawapinga WB au unajaribu kufanyaje yani?
Sasa ningewapinga WB ningetumia data zao?! Au kwani nimesema sio kweli, hatujafika hiyo level according to new data?
 
Kwani Zimbabwe ni choka mbaya sana eee?? Kwa rasilimali walizonazo na population yao haishangazi wao kuwa hapo..

Hata Tz tungekuwa na population ya hata 20m tungekuwa mbali zaidi ya hapa.. Watanzania wengi ni useless, tuamke tufanye kazi tuache lawama
 
Huko idhaa ya kiswahili ya sauti ya UJERUMANI DW watu wanamimina simu za pongezi kwa Rais Magufuli kutokana na kutufikisha hapa tulipoonekana na benki ya dunia.
 
Sasa ningewapinga WB ningetumia data zao?! Au kwani nimesema sio kweli, hatujafika hiyo level according to new data?
Sasa unachokifanya hapa ni kipi hasa maana hueleweki!

Mada iliyopo ni benk ya dunia kuiorodhesha tz kwenye nchi za uchumi wa kati!
Sasa wewe mwenzetu hueleweki kama unapinga au unakubaliana na benk ya dunia! Hebu twanbie basi msimamo wako ni upi kwenye hii mada
 
Hivi ni kweli hujaelewa nilichokisema au hutaki tu kukielewa kwa sababu ni hoja ambayo usingependa kuisikia?! Kwa kawaida mimi huwa naandika sana, lakini hapa hoja yangu ina maneno machache sana huku ikiongezewa uzito na graphs!

Sasa kisichoeleweka hapo nini?! Oh! Lemme guess... au unaona mbona sitembei kifua mbele kwa Tanzania kufikia uchumi wa kati sio?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…