Benki ya Dunia yaitangaza Tanzania kuingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati

Benki ya Dunia yaitangaza Tanzania kuingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati

Yaani sielewi hapa kosa au shida iko wapi kwa Jpm kujipongeza. Hivi kosa liko kwa Jpm kusema takwimu walizotoa WB kuhusu uchumi wa Tanzania au kosa ni WB wamedanganya? Kama kosa ziko kwenye takwimu kwa nini tusiwajadili WB kwa kupotosha ukweli na tukatoa Statistical analysis za kiuchumi za kwetu zinazoonyesha uhalisia?

Hapa zinaletwa takwimu, watu wanagoogle huko na kuzileta humu, kwani wasilaumiwe waliotoa takwimu hizi? Na ni lini Tanzania imewahi kuandikwa kama Lower-middle income kabla ya mwaka huu? Kuna ushahidi wowote hizo takwimu kuwahi kuwepo zaidi ya mwaka huu? Nafikiri hapa shida ni hesabu tu watu kuamua kupinga kila kitu. Kama kuna mtu anakumbuka maswali ya LOWER REAL LIMIT na UPPER REAL LIMIT yanapatikana wapi ataelewa nini kinachozungumzwa.

Hivi mtu akisema A itaanzia 75_100 kwa hiyo aliyepata 75-80 hatahesabiwa kama amepata A ila wa 90-100 ? Mbona vitu vidogo tunataka kuvifanya vionekane ni mjadala mkubwa?

Kwa mujibu wa WB ya dunia ili uwe kwenye uchumi wa kati ni lazima watu wa nchi husika waishi kwa angalau 2000-4000 kwa siku. Pia kundi lingine linaloanzia angalau 4000-9000 kwa siku. Hivyo range ya nchi ya uchumi wa kati ni angalau (2000-4000)chini- (4000-9000)juu.

Ninachojua ni kweli tanzania iko uchumi wa kati. Labda niambiwe World Bank wametoa takwimu za uongo na hawa ndio inabidi tuwajadili uongo wao. Lakini kama Word Bank wako sahihi na hii ni taarifa yao basi JPM yuko sahihi na ana haki ya kujipongeza. Hakuna ubaya wa kujipongeza kwa kila hatua nzuri unayoifikia haijalishi ina ukubwa gani.
Pongezi JPM
 
Wao walitaka kusikia Tanzania uchumi umeshuka na haingii uchumi wa kati, yaani uchumi wetu uwe sawa na Zimbabwe huo ndio wimbo wanaoimba kila siku matokeo yakiwa tofauti wanakuja na data zao ohh miaka mitano imeongezeka hivi ohhh tulikuwa hivi Mara vile , hata huu uchumi wakati umepatikana toka 2018 sasa hivi goal wamehamisha wa nakuambia miaka mitano , hapa cha msingi ni kujipongeza kuwa tuko ndani vibaya sana kama taifa.
 
Baada ya Tanzania kutangazwa Rasmi na Bank ya Dunia kufikia Uchumi wa Kati Julai 1st,2020 miongoni mwa Nchi zilizofikia Uchumi huo,Dniani kote imekuwa gumzo kwa pongezi. Sifa zote zimekwenda kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Rais JOHN POMBE MAGUFULI kwa hatua hiyo kubwa ya kukuwa Kiuchumi.

VIVA MAGUFULI ,TANZANIA JUUU ZAIDI
1593683629567.png
 
Wewe ndio uhuze uo ubongo wako, maana kama unabishana na wataharamu, beki ya dunia wametoa data zao kuwa Tanzania imeingia ktk kipato cha kati, wewe unakomalia madeni Ujui kuwa hata America taifa kubwa wanadaiwa deni kubwa,. Narudia tena ukiona unakopesheka jua anayekukopesha ameona unaouweza wa kulipa, kama unanibishia kuwa una kitu nenda Kwa jirani yako mwambie nikope uone jibu lake.

Ww ni kilaza fulani ndio maana hata kuandika kwa ufasaha huwezi. Neno sahihi ni uuze, na sio uhuze. Hakuna kitu kinaitwa wataharamu, bali ni wataalamu. Hapo tu inaonyesha ww ni kilaza wa kiwango cha juu sana. Kaa kushoto tafadhali.
 
Leo 1 of july 2020 Tanzania imeingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati "middle income economies "

Tanzania imeweka rekodi hii haraka kuliko ilivyotarajiwa hapo awali

Benki ya Dunia na taasisi nyingine duniani zimeendelea kumwaga sifa za pongezi kwa Rais Magufuli kwa kuongoza vyema Tanzania kupeleka uchumi wakati

Sisi ni matajiri

Soma pia: World Bank to officially declare Tanzania a Middle Income Country (MIC) on July 01, 2020

============

Hongera awamu ya tano kwa mafanikio hayo makubwa. Nchi zingine ambazo tupo kundi moja unaweza kuziona kupitia hii link World Bank Country and Lending Groups – World Bank Data Help Desk

Ahsante
 
Kwahiyo benk ya dunia wamedanganya?
Mkuu Chige ,nilikuwa nafanya analysis ili niweke hapa maana halisi ya hiki kitu kwa lugha nyepesi,nashukuru hilo umelifanya kwa uhakika kile kinachomaanishwa na report hii.
Mungu akubariki sana.
Kongole mkuu.
Ambaye hataelewa maandisho yako,hakika huyo atakuwa "low - middle mind citizen".
 
Leo 1 of july 2020 Tanzania imeingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati "middle income economies "

Tanzania imeweka rekodi hii haraka kuliko ilivyotarajiwa hapo awali

Benki ya Dunia na taasisi nyingine duniani zimeendelea kumwaga sifa za pongezi kwa Rais Magufuli kwa kuongoza vyema Tanzania kupeleka uchumi wakati

Sisi ni matajiri

Soma pia: World Bank to officially declare Tanzania a Middle Income Country (MIC) on July 01, 2020

============

Uchumi wa kati wa chini, ni tofauti na uchumi wa kati, hata hivyo kuna nchi ndogo nyingi tu ambazo zimeingizwa na si Tanzania tu Afrika Mashariki.
 
Narudia hoja ile ile Team Piga Makofi inayowakera!!!

Kwa takwimu hizo, ni ushahidi tosha kwamba JPM amevuruga uchumi, na JK was far better compared to JPM.

Taarifa hiyo ya Benki ya Dunia inasema kwamba:- Kwa maana nyingine, hatimae ndo tumefika kwenye $1036+!!'

Ukiangalia WB Secondary Data, unakutana na hii kitu (GNI per capita by Atlas Method).

View attachment 1495147

Kumbe, 2015 GNI Per Capita by Atlas Method ilikuwa $980. Kwa maana nyingine, kwa miaka 5 mzima, JPM alikuwa anahangaika kuivusha GNI per capita from $980 to $1036... a difference of ONLY $54.

Kinyume chake, GNI Per capita in 2010 ilikuwa kama ifuatavyo:-

View attachment 1495148

Utaona hapo, in 2010 GNI per capita ilikuwa $720, na kwa maana nyingine, GNI per capita ilipanda from $720 in 2010 to $980 in 2015! Yaani ilipanda kwa $260, wakati miaka 5 ya JPM imepanda around $54+!

On top of that, mwaka 2005 GNI per capita ilikuwa $500, na kwa maana nyingine, miaka yake 5 ya kwanza, Mzee wa Msoga alipandisha GNI per capita from $500 in 2005 to $720 in 2010... yaani $220 wakati JPM miaka 5 yake ya kwanza inaonesha kapandisha for less than $100.

View attachment 1495149

Sio siri tena kwamba, kwa takwimu hizo hapo juu, inathibitisha kwamba Magu ameharibu uchumi!

Na hapana shaka hata kidogo kwamba, mtaji mkubwa JPM ni Jeshi Kubwa la Wajinga lililopo nyuma yake! And JPM anafanikiwa haya kwa sababu ile ile niliyowahi kuitaja siku za nyuma: Tanzania is full of people with average mind, and many more below the average
Kwahiyi WB wamedanganya? Kwamba Tz haipo kwenye hilo kundi la nchi za uchumi wa kati?
Au wewe unachopinga hapa ni kipi hasa? Unawapinga WB au unajaribu kufanyaje yani?
 
Kweli tumepata sifa hiyo lakini safari ya hadhi hiyo kujidhihirisha kwenye maisha ya kila mmoja bado ni ndefu
 
Leo 1 of july 2020 Tanzania imeingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati "middle income economies "

Tanzania imeweka rekodi hii haraka kuliko ilivyotarajiwa hapo awali

Benki ya Dunia na taasisi nyingine duniani zimeendelea kumwaga sifa za pongezi kwa Rais Magufuli kwa kuongoza vyema Tanzania kupeleka uchumi wakati

Sisi ni matajiri

Soma pia: World Bank to officially declare Tanzania a Middle Income Country (MIC) on July 01, 2020

============

Aandika Rais mtarajiwa wa JMT Ndugu Z. Zitto Kabwe "
Zitto: "Mwaka 2015 pato letu lilikuwa USD 1,060, kuingia pato la kati la chini ni 1,090 lengo la nchi ni kufika USD 3,000. Sasa sherehe za nini"

kumbe tulishaingia uchumi wa kati mwaka 2015, maana mpango kasema ni kati ya $1036 mpaka $4045.
 
Kwahiyi WB wamedanganya? Kwamba Tz haipo kwenye hilo kundi la nchi za uchumi wa kati?
Au wewe unachopinga hapa ni kipi hasa? Unawapinga WB au unajaribu kufanyaje yani?
Sasa ningewapinga WB ningetumia data zao?! Au kwani nimesema sio kweli, hatujafika hiyo level according to new data?
 
Ndio mkuu hata bima zao wamekatia makampuni ya nje, pesa wanaweka akaunti za nje sie tumeishia kipata vibarua tu. Ndio maana nikasema takwimu chambua kwa umakini.
Kma ni SGR itaonyesha serikali imewekeza trillion kadhaa aaah mwisho wa siku zimeishia kwa muarabu. Ila kwa nje unaweza shangilia kuwa mtaani imeingia trillion 6!! Hivyo ndio pato la taifa litapigiwa hesabu hasa ikiwa expenditure approach.

Mkuu hivi hushangai Zimbabwe pia ni Uchumi wa kati? Really??
Kwani Zimbabwe ni choka mbaya sana eee?? Kwa rasilimali walizonazo na population yao haishangazi wao kuwa hapo..

Hata Tz tungekuwa na population ya hata 20m tungekuwa mbali zaidi ya hapa.. Watanzania wengi ni useless, tuamke tufanye kazi tuache lawama
 
Huko idhaa ya kiswahili ya sauti ya UJERUMANI DW watu wanamimina simu za pongezi kwa Rais Magufuli kutokana na kutufikisha hapa tulipoonekana na benki ya dunia.
 
Sasa ningewapinga WB ningetumia data zao?! Au kwani nimesema sio kweli, hatujafika hiyo level according to new data?
Sasa unachokifanya hapa ni kipi hasa maana hueleweki!

Mada iliyopo ni benk ya dunia kuiorodhesha tz kwenye nchi za uchumi wa kati!
Sasa wewe mwenzetu hueleweki kama unapinga au unakubaliana na benk ya dunia! Hebu twanbie basi msimamo wako ni upi kwenye hii mada
 
Hivi ni kweli hujaelewa nilichokisema au hutaki tu kukielewa kwa sababu ni hoja ambayo usingependa kuisikia?! Kwa kawaida mimi huwa naandika sana, lakini hapa hoja yangu ina maneno machache sana huku ikiongezewa uzito na graphs!

Sasa kisichoeleweka hapo nini?! Oh! Lemme guess... au unaona mbona sitembei kifua mbele kwa Tanzania kufikia uchumi wa kati sio?!
 
Back
Top Bottom