Benki ya Dunia yaitangaza Tanzania kuingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati

Benki ya Dunia yaitangaza Tanzania kuingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati

Chifu, nimelinganisha data za miaka mitano mitano!

From 2005 to 2010, From 2010 to 2015, from 2015 to 2020. Mbona hujahoji hiyo ya kuanzia 2005?! Btw, hata hiyo miaka 4 ya JPM kuna nini wakati gni ilishuka from $980 to $970?!

Halafu unadai figures za 2019 na 2020 zikitoka kutakuwa na mafanikio mazuri... figures zipi tena! Hebu shusha pumzi kisha tafakari! WB wamesema low middle income inaanzia 1036, lakini 2018 figure ni 1020! Sasa wameiwekaje kwenye low middle income kama figures za 2019 hazijatoka wakati za 2018 zisingeifanya nchi kuwa kwenye Low Middle?!

Na hapa usisahau kwamba tunazungumzia fiscal year.... kwahiyo figures kuanzia July 2020 zitakuwa accounted kwenye next fiscal year. Za 2019 zimeshatoka na ndizo zimeifanya Tz kutoka kwenye 1020 to Low Middle
figures za 2019 ndio zimeifanya nchi kuingia mid income?
 
Kuna document ya WB Tz iko kwenye kinfolk moja na Zimbabwe na IMEANDIKWA (SIN Seriously severely Indebted
 
Hivi Magufuli ndiye aliyetangaza TZ kuwa middle income au ni WB? Kwa nini anashambuliwa Magufuli?
JPM NDO KATANGAZA. Kwa kuondoka neno Lower kule World bank wametangaza Lowermiddle income
 
LOWER MIDLE INCOME NAONA NENO LOWER LIMEONDOLEWA KWA SabABU ZA KIUFUNDI
Neno LOWER limeonekana linaondoa ladha ya kutapeli raia.
Serikali yetu imefikia mahali ipo kama zuzu afanyaye kazi kwa Baniani mjini akipata salary increment tuu habari zitatangazwa kwao kijiji kizima kwa ndelemo.
Taarifa hii ya WB usishangae UVCCM wakaitisha maandamano nchi nzima kuipongeza ccm na jpm bila wao kuelewa maana halisi.

IMG_20200623_122420.jpg
 
Tanzania GNI Per Capita 1990-2020
Hizi data wengi wana zinatufundisha nini? GNI ilikuwa vizuri zaidi miaka 1995 hadi 2005 wakati wa mkapa, pia wakati wa kikwete lakini pia GNI ilikuwa kwa1% tu mwaka 2015, maana yake kulikuwa na anguko/ mdororo wa uchumi mwaka 2015 ambapo effect hiyo iliendelea hadi mwaka 2016 ambapo GNI ilikuwa kwa hasi ndio tena ika pick up in 2017 na 2018, suala la kujiuliza ni kwanini GNI uchumi uliyumba mwaka 2015 hadi kupelekea kuwa na effects katika miaka iliyofuata? so tukisema kikwete uchumi ulipaa ndio na tujue pia mdororo ulianza katika kipindi hicho hicho cha mwisho wa uongozi wake na hivyo aliyempokea lazima kutakuwa na ugumu wa kuanza kufufua uchumi na kuweka musingi upya.

Mkapa Ukiangalia data zote ndio Rais pekee aliye rithi uchumi mbovu na kuleta mageuzi makubwa , ni kipindi chake tu ambapo GNI ilikuwa hadi by 22% lakini mwaka 2001 pia ulishuka nadhani kwa sababu ya effects za uchaguzi za mwaka 2000 na issue za zanzibar , so Magufuli tayari amesha ufufua uchumi kinachotakuwa ni kuongeza kasi na kumantain asishuke.
Uchumi wa kikwete ulikuwa na msingi mbovu, ilibidi kuanza tena vizuri, ndio maana unashuhudia hilo anguko
 
Cdm walishaamka kwenye dunia ya giza boss. Wanapoambiwa kitu hawatii kama mbuzi, lazima wapime na kuujua ukweli ili kujiridhisha.
Lkn mbowe kudanganya kapigwa mkatii kama nyumbu mlivyo.
Kumbe alilewa.
 
Usikanganye takwimu za uchumi mfano hapo umeambiwa hiyo Dollar haijawa adjusted kwa PPP yaani haipimi nguvu ya pesa kwenye manunuzi kitu ambacho si kweli maana nguvu ya dollar 1 Tz na Dollar 1 zimbabwe sio sawa.

2. Hyo footnote inasema GNI haipimi welfare na Dev't ila yenyewe inachukua tu wastani wa kipato sio mtu mmoja mmoja na hpa ndio takwimu zinapokuwa misleading.

3. Haijawa adjusted kwa income inequality yaani mfano Trillion 6 za SGR zimeenda kwa kampuni ya mturuki basi pato la taifa litasoma kuna Trillion 6 zimeingia bila kujali nani na nani wamepata. Sasa ukienda kichwa kicjwa utaamini trillion 6 zipo kitaa kumbe kabeba mtu mmoja tu maana hta misumari wanaagiza nje!

Nachosema ni kwamba takwimu za kiuchumi hazisomwi kwenye kichwa cha habari bali CONTENT, na ndio maana siku Benki ya maendeleo Afrika ama IMF wakija na takwimu zingine kuonyesha ni Low income msije mkaanza kuwatukana ni mabeberu maana wao watakuja na formula tofauti tofauti so utaelewa nachosema.

NB: Jiulize zimbabwe pamoja na kuporomoka uchumi hadi negative growth kivp ndani ya mwaka wameingia ''uchumi wa kati'' .
Overview
Una uthibitisho misumari wanaagiza nje?
 
Pongezi kwa watanzania na serikali yao, japo maisha ya raia mmoja mmoja bado magumu sana
 
Juzi nilitafuta Sana kuona wale watalii waliojaza ndege zetu na za kimataifa kwa booking zimejaa Hadi mwezi wa nane. Cha ajabu mbughani watalii Ni Kama hawapo na kingine mtu kufanya booking bila kusafiri.
 
Hivi Magufuli ndiye aliyetangaza TZ kuwa middle income au ni WB? Kwa nini anashambuliwa Magufuli?
Usihangaike na wajinga aliovaa majoho ya kugraduate.
Labda Magu kawahonga mabeberu watangaze?
Kama mtu unatumia akili zote hata hivyo huwezi calculate growth kwa kugawa ongezeko la Usd 40 kwa 6.
Huo ni ukilaza wa hesabu za uchumi.
Utatumia factor zipi?
 
Dhana nzima ya utawala huu ni kuwatia ujinga watu, na huyo uliyemjibu hapo ndiyo sampuli sahihi ya waTanzania wa aina hiyo.

Kila kitu kinafichwa - COVID-19, hata hawajisumbui, bahati yetu nzuri, kwa sababu ambazo bado hazijulikani ugonjwa ukaishiwa nguvu; na wao bila aibu wanageuza hilo kuwa sifa kwao, hawaoni ujinga walioufanya na kujaribu kujirekebisha..

Lakini bado hawaoni aibu ya kuonekana vituko dunia nzima. Nani dunia hii ya leo anaweza kuamini chochote anachosema Magufuli!
Covid 19 bado Ni tishio Niko hospitali moja huku bila barakoa huingii getini. Halafu mdada mmoja aliniambia mzee wake aliugua, familia yote wakaugua
 
Back
Top Bottom