Benki ya Dunia yajitoa Rasmi Kufadhili Mradi wa REGROW Kwa Madai ya Ukiukwaji wa Haki za Wananchi Wanaozunguka Hifadhi ya Ruaha

WB wamefanya vizuri sana.Maana huyu mama amezidi sana kuonea watanganyika Kwa kuwafanya wakimbizi ndani ya Nchi Yao.
 
Jamaa siyo mpumbavu tu, ni kama Malaya wa Sinza. Hapa jukwaani kila siku anamsifia SAMIA.
Masta unajibu vizuri sana. Kubali challenge tu na endelea kujibu in positive. Kwa majibu yako mazuri hukustahili kuandika comment hii dhidi ya ChoiceVariable ... Ni kweli huyu hua ni pro Samia lakini sio kila kitu awe positive kuna vingine lazima atoe maoni yake in negative way inawezekana inamuathiri straight yeye.

By the way huyu jamaa ni pro utendaji kazi wa serikali ila mpaka hili kawa negative pamoja na kuwaingiza Chadema na TLS, basi kuna kitu hapa..
 
Hilo swala la hifadhi ni tofauti na DP World.TLS kazi Yao ni nini?

..hata CCM walitakiwa wawatetee hao wananchi.

..wenyeviti wa vijiji, madiwani, na wabunge wa CCM, wanaowakilishi wananchi waliodhulumiwa ndio waliopaswa kuwa wa kwanza kwenda mahakamani.
 
Mungu wabariki Wazungu
 
Wakati mwingine tufanye yetu bila kutegemea kutoka kwa watu.

Hifadhi ziendelee kuwa hifadhi, wavamizi waondolewe
 
Kwa nini wasishinde? Walifingua kesi wakashindwa?

Hao ni wapuuzi tuu kazi Yao ni kutetea Machadema hawana maana kabisa kulipwa mishahara na Serikali.

CCM na Rais ndio aliwatuma Game Rangers wa TANAPA wawafanyie mambo yasiyofaa Wananchi?
We unamjua Samia vizuri wewe
 
Orders kutoka ngazi za Juu ni Kisingizio,Kwa nini wasifanye kazi Kwa weledi?
Sio kusingizia, thats truth. Askari wa park hawatekelez orders bila amri kutoka kwa superiors wao.
na si hapo, look chaos ya ngorongoro?

ni patern ambayo ipo na ina baraka za viongozi. Deny uwezavyo ndio reality
 
Wakati mwingine tufanye yetu bila kutegemea kutoka kwa watu.

Hifadhi ziendelee kuwa hifadhi, wavamizi waondolewe
Tumejiegemeza sana kwenye misaada ndio maana. Hifadhi zibaki hifadhi lakin serikal ipunguze kuomba omba
 
Sawa mkuu
 
Benki ya Dunia imefuta mradi wa dola milioni 150 wa kuimarisha utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha nchini Tanzania, kufuatia madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu na mamlaka ya hifadhi hiyo. Chini ya mipango ya serikali ya Tanzania ya kupanua Ruaha, watu 21,000 wa eneo hilo wanaweza kuyahama makazi yao.


Taasisi ya Oakland, kikundi cha utetezi chenye makao yake makuu nchini Marekani, kiliita uamuzi wa kufuta mradi huo kuwa "ushindi wa kihistoria" kwa watu wanaoishi ndani na karibu na Ruaha.

Mradi huo unaoitwa Resilient Natural Resource Management for Tourism and Growth ( REGROW ) uliundwa ili kusaidia kuzalisha mapato ya utalii katika hifadhi ya Ruaha na mbuga nyinginezo za kusini mwa Tanzania, zinazopokea wageni wachache kuliko mbuga za Serengeti na Ngorongoro zinazojulikana zaidi kaskazini mwa Tanzania.


Mwaka 2008, serikali ya Tanzania ilitoa amri iliyoongeza ukubwa wa Ruaha mara dufu, na kuthibitisha uamuzi huo tena mwaka 2022. Kufuatia mpango huo kunaweza kuhitaji kufukuzwa kwa makumi ya maelfu ya wanakijiji.


Taasisi ya Oakland na wananchi wa eneo hilo wanadai kuwa askari wa hifadhi ya TANAPA, wakala wa hifadhi za taifa, waliendesha kampeni ya vitisho dhidi ya wafugaji na wakulima ndani ya eneo la upanuzi, kwa kutumia mbinu kama vile kutishia mauaji, kutaifisha ng'ombe, kuharibu mazao na kadhalika.


Mwaka 2023, Taasisi ya Oakland ilisaidia wakazi wawili wa eneo hilo kuwasilisha malalamiko dhidi ya REGROW na Jopo la Ukaguzi la Benki ya Dunia, ambapo walishutumu benki hiyo kwa kushindwa kufuata sera zake za ulinzi wa ndani. Benki ilituma wajumbe kuchunguza madai yaliyotolewa katika malalamiko hayo na kusitisha ufadhili wa REGROW mwezi Aprili 2024. Mnamo Novemba 2024, mradi huo ulifungwa rasmi kwa ombi la serikali ya Tanzania.


"Katika kukabiliana na uchunguzi wa utaratibu wetu huru wa malalamiko, tunatayarisha jibu la usimamizi na mpango wa utekelezaji ili kuhakikisha utiifu kamili wa sera zetu," walisema.


Katika taarifa yake kwenye tovuti yake, Taasisi ya Oakland iliitaka Serikali ya Tanzania kuachana na mipango yake ya kupanua hifadhi ya Ruaha, na kuwalipa fidia wanakijiji kwa ng'ombe waliokamatwa na faini walizolipa kwa TANAPA. Maendeleo ya TANAPA ni ya watu na watanzania wote sio kwa ajili ya serikali wala kikundi kidogo cha watu ndani ya serikali.


"Serikali na Benki ya [World Bank] lazima iwajibike kwa madhara yanayosababishwa na kutozingatia kwao haki za msingi za binadamu kwa madhumuni pekee ya kuongeza mapato ya utalii," aliandika Anuradha Mittal, mkurugenzi mtendaji huyo.
 

Attachments

  • images (91).jpeg
    26.2 KB · Views: 0
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…