Benki ya Dunia yajitoa Rasmi Kufadhili Mradi wa REGROW Kwa Madai ya Ukiukwaji wa Haki za Wananchi Wanaozunguka Hifadhi ya Ruaha

Benki ya Dunia yajitoa Rasmi Kufadhili Mradi wa REGROW Kwa Madai ya Ukiukwaji wa Haki za Wananchi Wanaozunguka Hifadhi ya Ruaha

WB wamefanya vizuri sana.Maana huyu mama amezidi sana kuonea watanganyika Kwa kuwafanya wakimbizi ndani ya Nchi Yao.
 
Jamaa siyo mpumbavu tu, ni kama Malaya wa Sinza. Hapa jukwaani kila siku anamsifia SAMIA.
Masta unajibu vizuri sana. Kubali challenge tu na endelea kujibu in positive. Kwa majibu yako mazuri hukustahili kuandika comment hii dhidi ya ChoiceVariable ... Ni kweli huyu hua ni pro Samia lakini sio kila kitu awe positive kuna vingine lazima atoe maoni yake in negative way inawezekana inamuathiri straight yeye.

By the way huyu jamaa ni pro utendaji kazi wa serikali ila mpaka hili kawa negative pamoja na kuwaingiza Chadema na TLS, basi kuna kitu hapa..
 
Hilo swala la hifadhi ni tofauti na DP World.TLS kazi Yao ni nini?

..hata CCM walitakiwa wawatetee hao wananchi.

..wenyeviti wa vijiji, madiwani, na wabunge wa CCM, wanaowakilishi wananchi waliodhulumiwa ndio waliopaswa kuwa wa kwanza kwenda mahakamani.
 
Kwa mujibu wa taarifa ya Oakland Institute kama ilivyonukuliwa na MongaBay ni kwamba Wananchi wa eneo la hifadhi ya Ruaha walipeleka malalamiko Benki ya Dunia Kisha kufunguliwa Kwa kesi Kwa manyanyaso waliyofanyiwa na maafisa wa TANAPA ikiwemo kuporwa mifugo Yao kwenye zoezi la kutaka kupanua eneo la hifadhi ya Ruaha ambapo zaidi ya wana Vijiji 21,000 wangepoteza Makazi Yao pamoja na Mali nyingine.

World Bank cancels $150m tourism project in Tanzania after abuse claims World Bank cancels $150m tourism project in Tanzania after abuse claims

Swali:
Yaani Kituo Cha Haki za Binadamu Tanzania na TLS hawaoni haya Ili wawasaidie Wananchi Hadi Wazungu ndio waje? Au hizo taasisi wenyewe kwao Wanasiasa wa CHADEMA ndio wanastahili Huduma zao pekee?

Mradi wa REGROW ulikuwa ni ufadhili wa Benki ya Dunia wa $150mln( Takribani Bilioni 350) uliolenga kukuza Utalii hifadhi za Kusini.

Soma zaidi hapa Kamati ya Bunge Yaridhishwa na Mradi wa REGROW Hifadhi ya Taifa Ruaha

My Take:
Kama taarifa hii ni kweli basi naishauri Serikali kama inataka kuongeza Ukubwa wa eneo la hifadhi ya Ruaha iwahamishe Wananchi Kwa Staha kama wanavyofanya huko Ngorongoro badala ya kuwafurusha.

Ngorongoro wanahamishwa kaya pamoja na mifugo Yao ,wanalipwa fidia na wanapewa maeneo,Kwa nini wasifanye hivi Ruaha?

Aidha Serikali iwachukulie hatua Askari wa TANAPA ambao walishiriki kuwatendea ndivyo sivyo Wanavijiji Hadi kutufikisha hapa Kwa kukosa weledi.

Pia soma Benki ya Dunia Yatoa "Ultimatum" ya Siku 30 Kwa Tanzania Kumaliza Mgogoro wa Ukiukwaji wa Haki za Binadamu kwenye Mradi wa Regrow
Mungu wabariki Wazungu
 
Wakati mwingine tufanye yetu bila kutegemea kutoka kwa watu.

Hifadhi ziendelee kuwa hifadhi, wavamizi waondolewe
 
Kwa nini wasishinde? Walifingua kesi wakashindwa?

Hao ni wapuuzi tuu kazi Yao ni kutetea Machadema hawana maana kabisa kulipwa mishahara na Serikali.

CCM na Rais ndio aliwatuma Game Rangers wa TANAPA wawafanyie mambo yasiyofaa Wananchi?
We unamjua Samia vizuri wewe
 
Orders kutoka ngazi za Juu ni Kisingizio,Kwa nini wasifanye kazi Kwa weledi?
Sio kusingizia, thats truth. Askari wa park hawatekelez orders bila amri kutoka kwa superiors wao.
na si hapo, look chaos ya ngorongoro?

ni patern ambayo ipo na ina baraka za viongozi. Deny uwezavyo ndio reality
 
Wakati mwingine tufanye yetu bila kutegemea kutoka kwa watu.

Hifadhi ziendelee kuwa hifadhi, wavamizi waondolewe
Tumejiegemeza sana kwenye misaada ndio maana. Hifadhi zibaki hifadhi lakin serikal ipunguze kuomba omba
 
Hamna kitu kama hicho. Jambo kama hulijui vizuri ni Bora ukawa msomaji. Kama kuzuia kununua mashati hayo na kama yangehitajika hamna kitu wangezuia maana katika USD Bil 150 walishatoa USD 125 Bil na zimetumika kujenga airstrip Kwa ajili ya ndege za Kitalii kule Nyerere National Park na Mikumi. Zimejenga njia za utalii za kupanda Kwa kwamba za umeme kule Udzungwa, zimejenga barabara za ndani ya Hifadhi ya Ruaha, zimejenga miundombinu za Umwagiliaji katika baadhi ya Skimu za Umwagiliaji kule Ruaha na zimeanzisha ujenzi wa kituo Cha Utafiti wa Wanyama na kituo Cha Utalii kusini pale Kihesa, Iringa.
Sawa mkuu
 
Benki ya Dunia imefuta mradi wa dola milioni 150 wa kuimarisha utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha nchini Tanzania, kufuatia madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu na mamlaka ya hifadhi hiyo. Chini ya mipango ya serikali ya Tanzania ya kupanua Ruaha, watu 21,000 wa eneo hilo wanaweza kuyahama makazi yao.
images (94).jpeg


Taasisi ya Oakland, kikundi cha utetezi chenye makao yake makuu nchini Marekani, kiliita uamuzi wa kufuta mradi huo kuwa "ushindi wa kihistoria" kwa watu wanaoishi ndani na karibu na Ruaha.

Mradi huo unaoitwa Resilient Natural Resource Management for Tourism and Growth ( REGROW ) uliundwa ili kusaidia kuzalisha mapato ya utalii katika hifadhi ya Ruaha na mbuga nyinginezo za kusini mwa Tanzania, zinazopokea wageni wachache kuliko mbuga za Serengeti na Ngorongoro zinazojulikana zaidi kaskazini mwa Tanzania.
images (92).jpeg


Mwaka 2008, serikali ya Tanzania ilitoa amri iliyoongeza ukubwa wa Ruaha mara dufu, na kuthibitisha uamuzi huo tena mwaka 2022. Kufuatia mpango huo kunaweza kuhitaji kufukuzwa kwa makumi ya maelfu ya wanakijiji.
images (90).jpeg


Taasisi ya Oakland na wananchi wa eneo hilo wanadai kuwa askari wa hifadhi ya TANAPA, wakala wa hifadhi za taifa, waliendesha kampeni ya vitisho dhidi ya wafugaji na wakulima ndani ya eneo la upanuzi, kwa kutumia mbinu kama vile kutishia mauaji, kutaifisha ng'ombe, kuharibu mazao na kadhalika.
images.jpg


Mwaka 2023, Taasisi ya Oakland ilisaidia wakazi wawili wa eneo hilo kuwasilisha malalamiko dhidi ya REGROW na Jopo la Ukaguzi la Benki ya Dunia, ambapo walishutumu benki hiyo kwa kushindwa kufuata sera zake za ulinzi wa ndani. Benki ilituma wajumbe kuchunguza madai yaliyotolewa katika malalamiko hayo na kusitisha ufadhili wa REGROW mwezi Aprili 2024. Mnamo Novemba 2024, mradi huo ulifungwa rasmi kwa ombi la serikali ya Tanzania.
images (89).jpeg


"Katika kukabiliana na uchunguzi wa utaratibu wetu huru wa malalamiko, tunatayarisha jibu la usimamizi na mpango wa utekelezaji ili kuhakikisha utiifu kamili wa sera zetu," walisema.
images (87).jpeg


Katika taarifa yake kwenye tovuti yake, Taasisi ya Oakland iliitaka Serikali ya Tanzania kuachana na mipango yake ya kupanua hifadhi ya Ruaha, na kuwalipa fidia wanakijiji kwa ng'ombe waliokamatwa na faini walizolipa kwa TANAPA. Maendeleo ya TANAPA ni ya watu na watanzania wote sio kwa ajili ya serikali wala kikundi kidogo cha watu ndani ya serikali.
images (86).jpeg


"Serikali na Benki ya [World Bank] lazima iwajibike kwa madhara yanayosababishwa na kutozingatia kwao haki za msingi za binadamu kwa madhumuni pekee ya kuongeza mapato ya utalii," aliandika Anuradha Mittal, mkurugenzi mtendaji huyo.
 

Attachments

  • images (91).jpeg
    images (91).jpeg
    26.2 KB · Views: 0
Back
Top Bottom