Benki ya FNB - Tanzania imesitisha kufungua akaunti za Forex

Benki ya FNB - Tanzania imesitisha kufungua akaunti za Forex

Izzi

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2016
Posts
553
Reaction score
1,144
Habari wana jukwaa;

I must declare; Mimi bado ni mwanafunzi katika tasnia ya FOREX. Sasa jana nilienda pale FNB Ohio st. ili nifungue akaunti ambayo ingekuwa mahsusi kwaajili ya FX tu. Lakini zoezi halikufanikiwa kwasababu niliambiwa kuwa hivi sasa wameamua kutofungua tena akaunti za FOREX. Wanasema chanzo ni kuwa akaunti nyingi za FOREX zilizofunguliwa na watu before zilikuwa zinatumika kidogo sana halafu watu wanazitelekeza, kwa hiyo inakuwa ni hasara kwa benki.

So, kama una mpango wa kufungua akaunti FNB this time kwa dhamira ya kuitumia kwa shughuli za FOREX - they won't allow you. ALTERNATIVE: Uwaambie una ajira, kwa hiyo akaunti ni kwaajili ya mshahara na transactions zingine, au uwathibitishie kuwa una shughuli zingine za kibiashara zaidi ya FOREX.

Binafsi alternative zote hazikunifaa kwasababu although nina shughuli zingine za kibiashara lakini nina akaunti CRDB, NBC na BANK ABC kwaajili hiyo. Nilihitaji akaunti ya FNB ndo iwe mahsusi kwa FOREX,... unfortunately. Kwa majibu yao inaonesha traders wengi Tanzania either hawako serious au wanachoma sana akaunti au ni janja janja nyingi mpaka wameziba milango ya wengine kufungua akaunti.

Siwalaumu benki kwa maamuzi waliyochukua, hata ningekuwa mimi ndo in charge of FNB I would do the same.
 
Una uelewa mdogo sana! Actually huwa hakuna account kwa ajili ya forex! Fungua acount bank yeyote ile ila mradi hiyo account iruhusu online transaction unakuwa umemaliza kazi! Mimi mbona natumia CRDB na NMB kufanya forex na sijawahi kukutana na ugumu wowote?!
 
Labda muelekeze how do you receive your money from Forex trading account into your local bank account.
Kulipia kitu nje ya nchi ni rahisi unaruhusu kufanya online payment kutumia VISA au MasterCard kwenye hizo bank account zako za local banks..
 
Nashukuru kwa kunikadiria kuwa na uelewa mdogo ukilinganisha na wako. Japo sina uhakika kama una uelewa mpana zaidi yangu.

Hata mimi nina akaunti CRDB na ninaitumia kwa online transactions bila shida yoyote. The issue is; FNB wanakamilisha miamala kwa kasi zaidi kuliko benki zingine. Ukitoa pesa kwenye akaunti yako ya forex chap wanakamilisha muamala compared to other banks. Kwahiyo sikutaka kudanganya jamhuri; nilipoulizwa unataka kufungua akaunti kwaajili ya nini? Sentensi yangu haikupinda pinda, ilinyooka - kwamba nataka kufungua akaunti ambayo itahusika zaidi na miamala ya forex... full stop.
 
Umeongea vitu ambavyo hata wewe mwenyewe huvijui, hakuna akaunti ya forex baba. Uliza vizuri kwa wanaojua watakuelekeza.

Cc. Behaviourist
Cc. Daud1990
Unadhani kuna anaejua vizuri zaidi ya mhudumu wa benki ya FNB nilieongea nae kwa mapana na marefu? Labda kama yupo anaejua jinsi ya 'kufanya udanganyifu' ili ufungue akaunti bila kutaja neno forex (something which I could do if I wanted to). Na uzuri yule mhudumu alinieleza wazi kuwa hata ukifungua kwa kudanganya kuwa unafanya shughuli za kibiashara au una ajira wakati huna, wao wana mifumo ya kufuatilia uhalali wa chanzo/vyanzo vya mapato vya wateja wao na eventually forex traders huwa wanawatambua. So you better be honest from day 1 ili isikupe shida mbele ya safari.

Na ndio maana uzi wangu haukuwa wa kuuliza, au kuomba ushauri - kwasababu naamini vyote ninavyopaswa kujua nimeshavijua. Labda kama una jipya tuambie.
 
Labda muelekeze how do you receive your money from Forex trading account into your local bank account.
Kulipia kitu nje ya nchi ni rahisi unaruhusu kufanya online payment kutumia VISA au MasterCard kwenye hizo bank account zako za local banks..
Watanzania buana: Do you think sielewi kitu kidogo kama hicho? Ah.. ok; najua mmeelewa vibaya niliposema mimi ni newbie katika forex. Ila ambacho hamjaelewa ni kuwa nimekuwa nafanya online transactions for years, na nimeshafanya transactions from my trading accounts into my bank accounts for a while now. Nilikuwa natumia cash card ya Bank ABC na Mastercard ya CRDB.

Nikisema mimi ni mwanafunzi haimaanishi mwanafunzi wa chekechea; I might be a self taught Ph.D student. So, do not underestimate my abilities, boy.
 
Computer Virus,
Mkuu wewe ndio umenielewa vibaya, laiti kama ungetulia ungeona nilikuwa nipo upande wako namtaka huyo jamaa afafanue. Maana alikupondea haujui vitu rahisi kuhusu kufanya transaction online kitu ambacho mimi najua wewe unajua na yeyote mwenye account CRDB anajua toka miaka mingi iliyopita.

Kitu ambacho ni shida hizo VISA na MASTERCARD za local bank zetu ni one way transaction wise, yaani unaweza kununua tu na sio kupokea pesa, labda kwenye hiyo local account yako utumiwe kwa njia ya SWIFT, na wengi unao trade nao Forex wa nje hawaweki option ya SWIFT, labda paypal na njia zingine.
Na ndio maana wewe ulienda kuomba FNB wakufungulie accoun itakayowezesha zoezi hilo kirahisi kama ambavyo akina Ontario a.k.a Sir Jef walivyo kuwa na makubaliano na hiyo bank.
Au nimekosea?
Na ndio maana mimi nikataka aliye kupondea aje afafanue yeye anafanyeje kwa faida ya wengi sio wewe peke yako.

Sasa ulipokuja na maelezo kama vile nimekukosoa nimebaki nakushangaa kwanini hiyo PhD yako haikukusaidia kunielewa kirahisi?
Hayo yote ya PhD umekuwa na mihemko tu, humu kuna wenye hizo PhD zaidi ya tatu.

Tatizo ulikuja na dhana flani juu yangu ikakufanya usielewe ujumbe wangu.
 
Titicomb,
Safi, now that I have grabbed your attention with my 'Ph.D stunt' - nadhani sikuelewa comment yako ya mwanzo kama nilivyoielewa hii. Hapa sasa tuko pamoja. Hii mihemko kawaida tu, ndo ubinadamu wenyewe.
 
Pamoja mkuu.
Najua mihemko kwa vile walio nitangulia wamekushambulia sana badala ya kukuelekeza cha kufanya.
Watanzania tunapenda kulaumu na kuponda bila kutoa suluhisho au kusaidia kutatua tatizo, wasamehe tu mkuu.
 
Back
Top Bottom