Benki yabariki wizi fedha za chuo cha Kanisa la Biblia Moshi

Ndagullachrles

Senior Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
153
Reaction score
161
Mgogoro wa madaraka Katika kanisa la Biblia Tanzania Kanda ya Kaskazini ,Sasa umefikia pabaya baada ya kundi linaloongozwa na Legius Nchimbi kuwasilisha nyaraka za kughushi za mabadiriko ya watia saini kwenye benki moja hapa Moshi na kuchota kiasi kikubwa cha fedha.

Kundi hilo kwa kumtumia Askofu Samwel Manyata wa Kanisa la Biblia Kanda ya Kusini ,walitengeneza Bodi feki na kuwasilisha barua feki za utambulisho wa watia Saini ambao hawatambuliwi na Bodi halali iliyochini ya Askafu Ombeni Mmile.

Watia Saini feki ambao majina yao yalipelekwa Katika benki hiyo (jina kapuni kwa Sasa)walifanikiwa kuchota sh,Milioni tano kwa nyakati mbili tofauti .

"Nchimbi ameghushi nyaraka na kuondoa Saini Halali za wamiliki wa akaunti ya Chuo cha BEREA BIBLE COLLAGE ambacho kinamilikiwa na kanisa la Biblia Tanzania kanda ya Kaskazini".

"Nchimbi alivunja Bodi Halali ya Chuo hicho bila kufuata taratibu baada ya bodi hiyo kuonyesha nia ya kufanya ukaguzi kwenye masuala mbalimbali ikiwamo masuala ya fedha",anasema mtoa taarifa wetu.

Watia saini halali wanaotambulika na beki ni Legius Nchimbi mwenyewe,Elisante Yuston Tella na Mchungaji Bernald Elly.

Watia Saini feki ni Nchimbi mwenyewe ,Bukuri Alfayo Masago na Bruno Massawe.

Askofu Ombeni anataka vyombo vya Dola kuchukua hatua dhidi ya waharifu hao ikiwamo kufikishwa mahakamani.

Bukuri Alfayo anatajwa kuasi kanisa hilo na kuanzisha kanisa lake liitwalo World Revival Ministry Tanzania na waumini hao wanahoji iweje awe mtia Saini kwenye Taasisi ambayo yeye si msharika.

Kesho tutaweka hapa kiasi cha pesa kilichochotwa na watia Saini feki na jina la Benki baada ya kuwapata wahusika kwenye benki husika .kaa mkoa wa kula
 
Ili kubadili watiaji sahihi muhtasari wa kikao lazima uambatanishwe pamoja na barua ya utambulisho wa waweka sahihi wapya, kuambatana na waweka sahihi wa zamani kwenda kuwabadili kama wamefaliki hati za vifo au kifo kama anayenadilishwa ni mmoja.
 
😹😹kaskazini kwenye pesa wako tayari ata kumuuza yesu
 
Kwanini usubirie kesho ndo uendelee au uwatishia wahusika ili nawe upate mgao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…