Benki yapiga mnada nyumba ya mwandishi wa habari wa Gazeti la RAIA MWEMA kisa deni la Tsh. Milioni 5.2

1. Mama Mwandishi anasema deni analifahamu

2. Anasema ana kesi mahakamani na mumewe kwa kuwa alibadili nyaraka na kusema nyumba ni yake pekee na sio ya familia.
Kwa hiyo benki hawakuhitaji saini ya mke kwa kuwa jina lilikuwa linasoma la mume kama mmiliki pekee.

3. Mama mwandishi anakiri kuwa taratibu zote za mahakama na mnada zimefuatwa - sijui ataweka zuio kwa jambo lipi na ili iweje

4. Mahakama ya Rufaa ilikwishaamua kuwa kama mtu unaona una maslahi kwenye kiwanja - sajili, hakikisha jina lako linakaa kwenye makaratasi bila ya hivyo hutahesabika kama una mali.
 
Sasa fanya kuwa wakili wa mdaiwa kwa muda ukamtetee dhidi ya bank
Mimi sio wakili wala bush lawyer ungeuliza professional yangu kwanza naelezea uhalisia wa jambo kwani na mm ni mkopaji mzuri tu wa bank na terms and conditions za mikopo yao naisoma vzr kabisa
 
Siamini kuna wanaume wanashindana na sidiria
Watu wanafikia hadi kuuwana wwe unasema Nini! Kuna Ndoa Wana Ndoa wanapigana sana matukio! Ukipata wa kusomana nae somo moja wwe shukuru Mungu wako!!!
 
Mikopo ilivyokuwa ya kishenzi hata kama umebakiza laki wanauza nyumba yako na pesa wanakula kwa ufupi wanakutapeli
Sio Kweli, wakiuza wanachukua kinachowahusu tu,kingine wanakuachia kwenye account yako. Kwa hiyo kama ikiuzwa mil 30 na deni ni mil 5 maanake chenji yako mil 25 watakuwekea kwenye account yako. Usifananishe bank na matapeli wa mtaani
 
Sio Kweli, wakiuza wanachukua kinachowahusu tu,kingine wanakuachia kwenye account yako. Kwa hiyo kama ikiuzwa mil 30 na deni ni mil 5 maanake chenji yako mil 25 watakuwekea kwenye account yako. Usifananishe bank na matapeli wa mtaani

ni uongo kabisa na watu wamefilisika mpaka kuwa omba omba kabisa .kama ingekuwa hivo tusingesikia hayo
 
ni uongo kabisa na watu wamefilisika mpaka kuwa omba omba kabisa .kama ingekuwa hivo tusingesikia hayo

ni uongo kabisa na watu wamefilisika mpaka kuwa omba omba kabisa .kama ingekuwa hivo tusingesikia hayo
Huo ndio utaratibu mkuu, kufikia hatua ya kufilisika ni ambapo deni ni kubwa zaidi,mfano kama mkopo ni mil 40 halafu nyumba imepigwa mnada milioni 30 maana yake watauza vitu vingine zaidi hadi itimie. Ila mkopo ukiwa mdogo kuliko thamani ya nyumba wanakupa chenji yako bila shida kabisa hata kama hutaki maana wao wanachukua chao tu
 
Wewe mzazi wako wa kike angetelekezwa na madeni na weww uko nae hamna msaada ungejiskiaje?
Hamna MWANAUME.mpumbavu atajenga nyumba yake kwa mamilioni kibao afu aje kuitelekeza nyumba na familia nzima eti kwa kukosa pesa mil 5 tu.

Jaribu kufikiria kwa kutumia akili na sio hisia mkuu
 
Atafute msaada wa kisheria kwanza. Hizi nyumba za familia kuwekwa dhamana zina utaratibu wake.
 
si kwa ubaya au dhamira hasi ikitokea umeiaga dunia itakuwaje baba j?
Nikifariki
Wanangu na ndugu zangu wanajua kila kitu, kwanza tukianza kua na kuviziana kwenye Mali ndo Yale MKE anakutanguliza ili arithi Mali.

Huo Ujinga kwangu haipo
 
Hamna MWANAUME.mpumbavu atajenga nyumba yake kwa mamilioni kibao afu aje kuitelekeza nyumba na familia nzima eti kwa kukosa pesa mil 5 tu.

Jaribu kufikiria kwa kutumia akili na sio hisia mkuu
Unaniambia nifikirie au nikupe experience iliyopo kwa watu niliokutana nao? Mwanaume anajenga nyumba peke yake ataiacha?? Wengi wanajenga na wake zao wanakuja kukopa hela bank kwa kufoji spousal consent ili wapewe hela.

End of the day anaondoka na hela anamwachia deni mwanamke na watoto wanateseka. Wewe utatetea because you are a man ila kwa yaliyowakuta watakupa
Experience.
 
Ninaamini mashauri haya yanakwenda kubatilishwa ( bank na dalali wake kuna kosa la kisheria hapo)
 
Huu ni ugomvi wa mapenzi unaochochewa na visasi kutoka pande zote mbili ...mwanamke ana hasira na uchungu na kaona njia rahisi kwake ni kuamua kutafuta huruma ya watanzania kwenye social media .. kumbuka hapo mwanamke hatafuti msaada wa kisheria kama alivyoanisha bali ameutangazia umma hilo tatizo lake ili ampate mtu atakayeweza kumlipia hilo deni lililobakia ili nyumba ibaki kuwa yake.. hii vita haitaishia hapo huko mbele kuna mtu atarogwa au kuuwawa katika mazingira yasiyoeleweka, Mungu awasaidie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…