Benki za Biashara Tanzania zinaogelea kwenye faida. Je, nini kimefanyika awamu ya sita?

Benki za Biashara Tanzania zinaogelea kwenye faida. Je, nini kimefanyika awamu ya sita?

Mnapambana sana kuonesha mama hawezi ila mmeshindwa hata kabla ya kuanza,
Nani kapambana mbona Nimesema atamwaga trillion 5 kufufua uchumi??

Nachosema ni timeline, yaani mafanikio ya sera zake yataonekana latest 2023 ila sio miezi 6!! Mama hta BOT ndio kwanza recruitment na reshuffle zinaendelea kuweka timu yake vizuri alafu ghafla ndio mafanikio ya kibenki ni sababu ya miezi 6 yake??

Hoja yangu ni kwamba hatua zilishaanza chukuliwa toka mwaka jana ikiwemo Mkopo wa Trillion moja kwa mabenki, sasa unapodai ni mafanikio ya mama je hyo trillion moja aliitoa yeye??

Embu tupende kuwa watu wa facts sio ushabiki
 
Si nasikia BoT wamepunguza riba kutoka 7% - 5%, na kutoa 1 T stimulus package kwa mabenki; ili hali benki zimebaki na riba zilezile za 17% - 20%
 
Ukiona benki inapata faida sana ujue kuna watu wameumia sana, benki ni taasisi za dhuluma, wanakupa fedha makaratasi afu wanakukopesha kwa bond ya kitu halisi kama mjengo, ardhi yako nk.
 
Yaap ndo ile unasikia serkali itaongeza mzunguko kwa kuzipa Bank fedha kwa riba ya asilimia 7%!Na baade serkali hiyo hiyo inaenda kukopa kupitia taasisi za kiserkali kama mamlaka za maji,tanesco n.k na inalipa riba ya asilimia 16%.Yaani kwa kifupi serkali inatoa hela kwenye benki kwa riba ya asilimia 7% then inazikopa na inalipa kwa asilimia 16%. Ndo maana Magufuli alikataa! Usishangae hiyo faida maana wakubwa ndo wanakula hapo maana ndo mashareholder wakubwa kwenye hayo mabenk!
Lakini hyo difference ya 7% na 16% ndio inaleta multiplier effect kuchochea uchumi. Coz benki zitaajiri zaidi, zitakopesha zaidi, wafanyabiashara kuongeza mitaji n.k

Hela hizo ni kodi zetu sio mali ya serikali maana haina shamba!! So kuigawa kwa private sector ni jambo jema kiuchumi
 
Ni kweli inaomgeza zaidi kwa watu wenye hisa kwenye mabenki! Pia ujue kabisa deni la taifa linaongezeka sana maana riba inakuwa kubwa!
Sasa mwenye hisa hizo pesa hatumii?? Hatoajiri watu kwenye uwekezaji mwingine atakaofanya? Hatolipa kodi akiuza hisa ama dividend anayopata haikatwi kodi??

Multiplier effect ndio muhimu kuangalia na hata ukifuatilia duniani kote ukwasi unaanzia juu ndio uje kwa makapuku hakuna uchumi wa bottom-up!! Ni uongo wa Ruto huo.
 
Mimi sio mchumi isipokuwa kwa akili yangu ya kawaida tafsiri yake ni kwamba uchumi unafunguka, uwekezaji unaongezeka vikiambatana na ongezeko la mzunguko wa fedha kupitia ajira na huduma kupitia uwekezaji utakaofanywa na mikopo hiyo iliyozaa faida hiyo.

Nadhani ni hatua nzuri kiuchumi.
upo sahihi sana... utawala wa mama umerejesha confidence kwenye uchumi. Matokeo yake investors wa ndani wana ari ya kufanya kazi.

Kwahiyo fursa za kiuchumi zinafunguka kwa kasi sana, na mabenki kupata faida maana yake ni kwamba wakopaji wake ambao ni sekta binafsi nao pia kwa sasa wapo vizuri.

Na hichi ni kiashiria kikubwa kwamba uchumi unaanza kupaa.. kuna viashiria vingi sana kwa sasa
 

Wachumi mtusaidie hili, Hivi mabenki yetu ya biashara kupata faida ya TZS 471B kwa miezi tisa tu,Wakati huko nyuma yalipata TZS 286B kwa mwaka ina maana gani kwa Uchumi wa nchi yetu?Je! ni Vyuma kulegea?​

===
Mtakumbuka kwa mara ya mwisho hapa Tanzania mabenki yetu ya biashara kurekodi faida ya kihistoria ilikuwa ni mwaka 2015 pale ambapo yalirekodi Jumla ya faida ya TZS 438BL hii ni baada ya kulipa kodi ya Serikali,
===
Mtakumbuka pia kwamiaka mitano mfululizo iliyopita mabenki haya hayajaweza kabisa kuivunja rekodi hii zaidi sana wakati flani faida zao zilishuka mpaka kufikia Jumla ya Tshs 286BL mwaka 2017 hii ilikuwa ni Jumla ya faida kwa mabenki yote ya biashara nchini kwa mwaka huo,
===
Leo chini ya Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan tena kwa kipindi kifupi cha Jan -Sept mabenki hayo hayo kwenye nchi hii hii yameivunja ile rekodi iliyowekwa na Dk Jakaya Kikwete kwa faida ya Tshs 438BL kwa zaidi ya 7.53% na hii ni kwa robo tatu tu ya mwaka,
===
Kwalugha rahisi miezi michache ya Rais Samia mabenki yamevunja rekodi ya faida ya tangu uhuru ambayo ilivunjwa kwa mara ya mwisho na Mzee Jakaya Kikwete kwa thamani ya faida ya Tshs 438BL leo Samia ameivunja kwa thamani ya faida ya Tshs 471BL na hii ni kwa miezi tu, tunaposema Rais Samia hakamatiki tunamaa hii,
===
Kwa tathimini iliyofanywa kwa mabenki 13 ya kibiashara nchini kati ya 14 yanayotengeneza faida kila mwaka ni NMB na CRDB tu ndio wamebeba 80% ya faida yote ya Tshs 471BL kwa kuwa na faida ya Jumla ya Tshs 379BL,Wakati huohuo NPL yaani Non Performing Loans au mikopo " Chechefu " ikishuka na kufikia chini ya 35.7% kwa baadhi ya mabank huku thamani yake ikupungua kutoka tshs 395.69BL mwaka 2020 hadi tshs 392.4BL kwa lugha ya kibenki (arrears -zimepungua )
===
Sababu kubwa yaongezeko hili kubwa la Faida kwa mabenki yetu ya biashara nchini zinatajwa kuwa ni Sera nzuri za ki-Uchumi za Serikali ya awamu ya Sita Chini ya Mama Samia Suluhu Hassan pamoja na miongozo mathubuti toka BOT kama mlezi wa mabenki haya hasa kwenye kupunguza vipimo vya risk kwenye utoaji mikopo ikiwa ni pamoja na kutoa fedha maalumu "Stimulating fund " kiasi cha Tshs 1trl ili kuziongezea Ukwasi baadhi ya Benki zetu za biashara zilizokaukiwa hii imesaidia sana kuinua sekta ya fedha ambayo utoaji mikopo kwa mujibu wa BOT umepanda toka 2.5% 2020 hadi 9.8% hivi sasa,
===
Kwamsiofahamu zaidi ya 80% ya faida yote ya mabenki ya biashara inabebwa na mikopo na Ukiona mabenki yanapata faida sana maana yake yamekopesha sana na wateja wao wameweza kurejesha mikopo yao ( EMI) kwa wakati na ndio tunasema NPL imeshuka au mikopo isiyolipika|chechefu imepungua na ndio sababu faida imepanda na kwa maana hiyo biashara mtaani inakua au inakwenda vizuri ndio maana mteja X aliyekopa katika benki Y ameweza kuchukua mkopo Benki na kununua bidhaa na kisha kuziuza na mwisho kupeleka marejesho ya Benki kwa wakati yaani ( Purchasing Power-Uwezo wa kununua kwa Watanzania ) umeongezeka , Hongera Sana Rais Samia hakika unaupiga mwingi,


Hizi taarifa zote zinazohusu mabenki kupata faida kubwa sana siyo za kweli kwa vile mabenki siyo maduka ya kuuza na kupata faida papo kwa papo, bali faida za mabenki hutokana mikopo ambayo hulipwa baada ya muda mrefu kwa faida (riba). Benki haiwezi kukopesha miezi sita tu na kupata faida kubwa sana, hizi taarifa ni za propaganda tu.
 
Na bado waongeze bidii , hizo faida sio kubwa kulinganisha na nchi nyingine zenye mabenki makubwa na imara Afrika.
Wafanye kazi kwa kiu , kwa ustadi na ubunifu.

Walegeze masharti ya kutoa mikopo.
 
Na bado waongeze bidii , hizo faida sio kubwa kulinganisha na nchi nyingine zenye mabenki makubwa na imara Afrika.
Wafanye kazi kwa kiu , kwa ustadi na ubunifu.

Walegeze masharti ya kutoa mikopo.
Nikweli kabisa naungana na wewe kwenye hili
 
Wachumi mtusaidie hili, Hivi mabenki yetu ya biashara kupata faida ya TZS 471B kwa miezi tisa tu,Wakati huko nyuma yalipata TZS 286B kwa mwaka ina maana gani kwa Uchumi wa nchi yetu...
safi sana
 
Back
Top Bottom