TANZIA Bernard Kamilius Membe afariki dunia
View attachment 2618772

Aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya Nje kwenye Serikali ya awamu ya nne, Benard Membe amefariki Dunia. Taarifa za awali zinaeleza Membe alipata changamoto ya Kifua na kupelekwa Hospitali ya Kairuki alfajiri ya leo May 12, 2023 na baadaye kufariki.

Benard Membe alipata kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia jimbo la Mtama na alihitimisha safari hiyo mwaka 2015 na kujaribu kuwania tiketi ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama cha mapinduzi(CCM), tiketi ambayo alipewa hayati John Magufuli.

Mwaka 2018 aliandikwa na gazeti la Tanzanite akituhumiwa kuweka ajenda ya kutaka Rais Magufuli asipewe nafasi ya kuwania Urais 2020, ambapo alifungua kesi ya madai ya kuchafuliwa na kushinda kesi hiyo, alikazia hukumu iliyomtaka mmiliki wa gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba alipe Tsh. bilioni 9 ndani ya siku 14.
juju
 
Wewe endelea kuishi kwa hisia, Mimi nimekupa fact za kisheria.
Unajua sio rahisi kama unavyotamani. Kisheria kabisa musiba alitakiwa kupata adhabu kwa kukataa wito wa mahakama.
Musiba alipokea wito wa mahakama, Ila akakataa kwenda. Unahisi kwa nini mahakama haikuchukua hatua kwa kudharauliwa na musiba?

Usifikiri bongo mahakama Ina nguvu kiasi hiko. Juzi hapa yule jaji mstaafu wa mahakama kuu alisema moja ya kitu kilichomtesa sana ni pale alipoona hukumu ya mahakama kuu inachanwa hadharani kabisa na aliyekua waziri mkuu lowassa. Na hakuna kitu walifanya
 
Kumbe aliyechana Hukumu alikuwa Lowasa?
 
View attachment 2618772

Aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya Nje kwenye Serikali ya awamu ya nne, Benard Membe amefariki Dunia. Taarifa za awali zinaeleza Membe alipata changamoto ya Kifua na kupelekwa Hospitali ya Kairuki alfajiri ya leo May 12, 2023 na baadaye kufariki.

Benard Membe alipata kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia jimbo la Mtama na alihitimisha safari hiyo mwaka 2015 na kujaribu kuwania tiketi ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama cha mapinduzi(CCM), tiketi ambayo alipewa hayati John Magufuli.

Mwaka 2018 aliandikwa na gazeti la Tanzanite akituhumiwa kuweka ajenda ya kutaka Rais Magufuli asipewe nafasi ya kuwania Urais 2020, ambapo alifungua kesi ya madai ya kuchafuliwa na kushinda kesi hiyo, alikazia hukumu iliyomtaka mmiliki wa gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba alipe Tsh. bilioni 9 ndani ya siku 14.
Mungu ameamua ugomvi alijisemea Nape
 
Ila ukweli ni kwamba siku yako ikifika hakuna wa kupinga, na tuamini kwamba kama haijafika hata unywe sumu, au upigwe risasi huto kufa, na tujifunze kwamba binadam inatakiwa ujiweke tayari kwa lolote litalotokea mbele yako, kwani huwezi jua kesho yako
 
Back
Top Bottom