Tumefika hapa kwasababu wapo wajuaji waliogoma kusahau yaliyopita, wayaache yaende, hawa wakajiona wamekaa juu wamefika, wao kila siku ikawa ni kumuimba marehemu mtangulizi, wala wasikumbuke nae alikuwa na wapendwa wake, wakajisahau wakidhani kifo kina undugu au urafiki, leo kifo kimewakumbusha hakina mwenyewe, sote tunapita.
Sio wakati wa kulaumiana tena, maisha ni fumbo, tujifunze kuyaacha yaliyopita yapite, lakini sio kujisahau na kujipachika majina ya ajabu kama wazuri hawafi, Mungu fundi, au kazikwe nae, leo majina hayo hayo yanarudishwa upande wa pili, ni vyema wahusika wakayapokea kwa mikono miwili kama ambavyo walianza kuwapa wenzao, time to feel a taste of your own medicine.