TANZIA Bernard Kamilius Membe afariki dunia
1683890697751.png
 
View attachment 2618772

Aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya Nje kwenye Serikali ya awamu ya nne, Benard Membe amefariki Dunia. Taarifa za awali zinaeleza Membe alipata changamoto ya Kifua na kupelekwa Hospitali ya Kairuki alfajiri ya leo May 12, 2023 na baadaye kufariki.

Benard Membe alipata kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia jimbo la Mtama na alihitimisha safari hiyo mwaka 2015 na kujaribu kuwania tiketi ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama cha mapinduzi(CCM), tiketi ambayo alipewa hayati John Magufuli.

Mwaka 2018 aliandikwa na gazeti la Tanzanite akituhumiwa kuweka ajenda ya kutaka Rais Magufuli asipewe nafasi ya kuwania Urais 2020, ambapo alifungua kesi ya madai ya kuchafuliwa na kushinda kesi hiyo, alikazia hukumu iliyomtaka mmiliki wa gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba alipe Tsh. bilioni 9 ndani ya siku 14.

Sijui Mzee Makamba atasemaje. Wema huwa hawafi. RIEP Mzee Benard Membe
Duh! Kitabu gani hicho ndugu mtanzania [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Anacho Mzee Makamba 😂 😂 😂 😂 😂 😂
 
Mbona unang'ang'ana sana na siku tano. Kwani Membe hakuwa na hela ya kula mpaka akadai hiyo hela ndani ya siku tano, au kuna sheria inalazimisha udai ndani ya siku hizo. Angesubiri hata mwaka angedai
Siku tano kwa sababu ndio zilitajwa
 
View attachment 2618772

Aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya Nje kwenye Serikali ya awamu ya nne, Benard Membe amefariki Dunia. Taarifa za awali zinaeleza Membe alipata changamoto ya Kifua na kupelekwa Hospitali ya Kairuki alfajiri ya leo May 12, 2023 na baadaye kufariki.

Benard Membe alipata kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia jimbo la Mtama na alihitimisha safari hiyo mwaka 2015 na kujaribu kuwania tiketi ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama cha mapinduzi(CCM), tiketi ambayo alipewa hayati John Magufuli.

Mwaka 2018 aliandikwa na gazeti la Tanzanite akituhumiwa kuweka ajenda ya kutaka Rais Magufuli asipewe nafasi ya kuwania Urais 2020, ambapo alifungua kesi ya madai ya kuchafuliwa na kushinda kesi hiyo, alikazia hukumu iliyomtaka mmiliki wa gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba alipe Tsh. bilioni 9 ndani ya siku 14.
Swali la msingi kabisa kwanini apelekwe Hubert Kairuki wakati alikuwa kiongozi mwandamizi wa serikali??? Je Hubert Kairuki ni nzuri kuliko Muhimbili?? Je na ile hospitali ya viongozi wa serikali kwa nini hawakumpeleka huko???? Je BM kafariki hana imani na serikali???? Haya ni maswali ya msingi sana. Kikubwa watanzania tuwe wamoja, naamini kabisa BM alikuwa mzalendo sana na kaitumikia nchi yetu kwa uzalendo wa hali ya juu, anahitaji heshima tuache dhihaka. Ni kama ilivyo kwa Dkt Magufuli, tusipende kulipiza kisasi, wote sisi ni wafiwa watarajiwa na kifo hakiepukiki.
 
Back
Top Bottom