TANZIA Bernard Kamilius Membe afariki dunia
View attachment 2618772

Aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya Nje kwenye Serikali ya awamu ya nne, Benard Membe amefariki Dunia. Taarifa za awali zinaeleza Membe alipata changamoto ya Kifua na kupelekwa Hospitali ya Kairuki alfajiri ya leo May 12, 2023 na baadaye kufariki.

Benard Membe alipata kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia jimbo la Mtama na alihitimisha safari hiyo mwaka 2015 na kujaribu kuwania tiketi ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama cha mapinduzi(CCM), tiketi ambayo alipewa hayati John Magufuli.

Mwaka 2018 aliandikwa na gazeti la Tanzanite akituhumiwa kuweka ajenda ya kutaka Rais Magufuli asipewe nafasi ya kuwania Urais 2020, ambapo alifungua kesi ya madai ya kuchafuliwa na kushinda kesi hiyo, alikazia hukumu iliyomtaka mmiliki wa gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba alipe Tsh. bilioni 9 ndani ya siku 14.
 

Attachments

  • IMG_6742.MP4
    4 MB
mungu wenu ni dhaifu, amechelewa, alitakiwa ugomvi huu auamuwe kabla ya hukumu, lakini is too late mungu wenu dhaifu hawezi kubadili chochote, minada inaendelea na pesa lazima zilipwe.
Mungu wetu fundi sana tu!

Kesi ndio imeishia hapo!

Mbaya zaidi membe ni moja kwa moja motoni maana kaga akiwa na chuki kwa musiba hata baada ya kuombwa na maaskofu asamehe.
 
Back
Top Bottom